Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 2,215
- 3,819
Tanzania kwa siku za hivi karibuni imedhihirisha kile ambacho Naibu waziri wa Afya Dk. Mollel aliwahi kusema; kwamba Tanzania wajinga ni wengi.
Kwa bahati mbaya sana hata viongozi wakubwa na wasaidizi wa Rais, nachelea kusema kwamba na wao wamejidhihirisha kwamba ni wajinga. Hii pamoja na mambo mengine, imekuja baada ya Mkataba wa Kimangungo-mangungo wa DP World.
Hivi kama kweli siyo ujinga na umbumbumbu, utaingia mkataba ambao hauna kikomo na wenye masharti ya kuondoa uhuru wa nchi na wananchi wake katika kutumia rasilimali walizojaaliwa na Mwenyezi Mungu?!
Hivi kama kweli hatuongozwi na wajinga, mtatuleteaje mkataba ambao tayari Rais alishasaini yapata mwaka mzima huko nyuma, eti tuujadili (kupitia wawakilishi wetu wabunge ambao pia wamedhirisha ni wajinga wa kutupwa!?)? Kama siyo ujinga huu, nini basi??
Viongozi wengi wa Tanzania ni waoga!
Wengi wako kwa ajili ya maslahi ya matumbo yao wenyewe na familia zao.
Na huwezi kuutenganisha uoga na ujinga. Wengi wanajidhalilisha kwa kutetea mambo ya kijinga ili tu waendelee kuwepo kwenye nafasi zao au wapewe promotion!
Hivi kweli hadi lini tutaendelea kuongozwa na wajinga wa aina hii?!
Mwisho, japo siyo kwa umuhimu; mjinga huwa hapendi kukosolewa, maana utashangaa baada ya ujumbe huu kusomwa na wanajamvi (ambao pia wajinga ni wengi), utashangaa uzi unatoweka kwenye mazingira ya kutatanisha na kumfuatilia mwandishi badala ya kuhangaika na kuondokana na ujinga!
Hatuwezi kuendelea kushuhudia mambo ya kijinga yakifanywa na viongozi wajinga yakiendelea katika nchi yetu.
Yaani kina Nyerere walifanya juhudi za kututoa utumwani, halafu wajinga wachache wanataka kuturudisha huko tena kwa bei chee kabisa; HAIWEZEKANI.
Amandraaaaaaaa..................
Aluta continua.