Je, ni halali 80% ya madereva wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Kenya na Rwanda?

ARIZ

Senior Member
Apr 1, 2017
102
79
Wadau naombeni ushauri,najua kuna Sheria zinazozuia kuajiri raia wa nje Kwa kazi zinazoweza kufanywa na watanzania.

Hili la MADEREVA wa EAC na EALA karibu MADEREVA 20 waliopo pale ni kama watatu tu ndo watanzania.

Je, ni Sheria ya mikataba?
Je, watanzania si MADEREVA wazuri?
Je, hatuna MADEREVA wa kutosha?

Naombeni ushauri na pia mumfikishie ujumbe wazuri husika.

Pia kuna MADEREVA wapo pale Kwa zaidi ya miaka kumi pamoja na Sheria kutaka wageni wasizidi miaka hiyo.
 
Kuna vitu lazima tukubali ukweli ni madereva wangapi wa Tanzania ambako udereva ni kazi ya walioshindwa kila kitu anajua Kiingereza kwa Ufasaha, nani anajua Kifaransa ? Hakuna chuo cha Chauffeur hapa vipo vya kuendesha gari tu
 
Reactions: y-n
Kama
Unachangamkiaje fursa kwenye uwanjani usio sawa?Kwa hiyo tuhamie KENYA NA RWANDA ?
Kama hujui maana hutoambiwa maana. Jiongeze. Use the opportunities available to move forward
 
Kuna vitu lazima tukubali ukweli ni madereva wangapi wa Tanzania ambako udereva ni kazi ya walioshindwa kila kitu anajua Kiingereza kwa Ufasaha, nani anajua Kifaransa ? Hakuna chuo cha Chauffeur hapa vipo vya kuendesha gari tu
UNHCR, WFP, IOM,UNiCEF,ILO mbona madereva wao 80-90% ni watanzania...
 
Ngoja tumtumie yule mama wa uhamiaji utasikia mrejesho kwa awo madereva.
 
watanzania tunatakiwa tujiongeze, ukweli ni kuwa hatuna viwango kwenye kazi nyingi sana hata hizo za udereva, upishi, kwenye mahoteli n.k. Wakenya wana viwango vya juu sana kazini.
 
Huu ndio uzalendo, halafu tuhoji hao jamaa wanaotoka kenya na rwanda wanaishi vipi Tanzania isiwe kwamba wameshaanza kujichanganya na wazawa, hao watu hawatakiwi kukaa nchini kwetu.
 
Kuna vitu lazima tukubali ukweli ni madereva wangapi wa Tanzania ambako udereva ni kazi ya walioshindwa kila kitu anajua Kiingereza kwa Ufasaha, nani anajua Kifaransa ? Hakuna chuo cha Chauffeur hapa vipo vya kuendesha gari tu
Kwani bunge la Afrika mashariki wanatambua hiyo lugha? Lugha inayotumika ni kiswahili, msituletee ujinga Tanzania.
 
Si halali na mimim ningegombea bunge la EA ningeanza lao lazima uwekwe uwiano tena kwa base ya population!
 
Nafikiri maana ya EALA na EAC hujatafsiri vizuri, huwezi kusema ni madereva wa kigeni wakati wanatoka nchi wanachama

mbona mabinti wakazi mnapenda kuwatoa sehemu zingine na wakati kuna ndg zenu hawana kazi?
 
Nadhani ufahamu hafifu wa lugha za kigeni kama kiingereza na kifaransa ni sababu mojawapo.
 
Wanaowaendesha mabosi hapo utakuta ni hiyo 10-20% hiyo ya Watanzania ni kutumwa peleka hapa waswahili au mzigo
Mkuu hao ni madereva wa kawaida kabisa wanaendesha staffs wa kitanzania..kibongo bongo watu wengi hawana exposure za kua apply hizo kazi, wengi wa hao madereva ni wahaya..ambao exposure wanazo kiaina...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…