Je, mfalme Haile Selasie wa Ethiopia ni mtoto wa mfalme Daudi wa kwenye ukoo wa Yesu?

Nash mjamaica

Member
Jun 11, 2011
57
16
Habari wanaforum,kuna kitu kinanitatiza ningeomba ufafanuzi kuhusu hili,mwaka 2013 nilipata kuishi bagamoyo ambayo mpaka sasa naamini ni sehem pekee tanzania yenye watu wengi sana jamii ya rastafarain na dreadrocks wengi sana na wengi wenye kuifatilia imani hiyo ya kirasta kupata kuona tz hii,

Kuna kitu nilikisikia kutoka kwa jamii iyo ya marasta kwamba kiimani yao wanaamini baada ya yesu kuondoka na kusema ataleta msaidizi basi msaidizi uyo ni haile selasie ambae alikua ni mfalme wa ethiopia kutoka afrika.

Wanaamini bibilia hii tunayoisoma imeficha mambo mengi ikiwepo la haile selasie kuwa ni mtoto wa daudi babake na joseph ambaye ndie baba wa yesu Kristo.

Inasemekana kuna malkia wa ethiopia kipindi kile alikua mrembo sana ila kilema wa miguu,kuna kipindi alisafiri kwrnda israel kisiasa na kukutana na daudi mfalme na daudi kumtamani na kulala nae ambapo alipata ujauzito wa haile selasie mfalme wa ethiopia.

NB:wanajamvi nimejaribu kuelezea kifupi nilivockia kipindi kile kwa iyo jamii ya kirasta ila sijaijua kiundani zaidi na ningependa kwa mwenye ufaham kuhusu ili atufafanulie kwa faida yangu na wengine zaidi

Nadeclare interest napenda kuwa rasta one day so ningependa kufaham mengi kuhusu iman iyo nikiamin jf inteligence hakukosekani kitu ntashukuru kwa mrejesho chanya kuhusu ilo.

Asanteni.
 
Kwanza kabisa Haire Selesie. ni mtu wa juzi sana miaka 60 iliyo pita alikuwa hai kabisa kwahiyo kwaushahidi huwo tu niuwongo. Huyo mfalme mwenye hakuwahi kuwa nahiyo imani bali alikuwa ni Mkristo waki Othodox.
Niuzushi ulio tukuka kwani mfalme mwenye huko aliko hajui kama duniani anaitwa mtume kwani Marasta waliamuwa kumuita mtume baada yakuona niyeye tu ndie mtu maarufu na mwenye sauti huku Afrika kumbuka dini yaki rasta nidini ya wanaharakati wa Afrika.
 
Ngoja nikueleweshe mkuu...miaka ya mfalme daudi iliisha alipofikia uzee sana na mwanae Suleiman akatawadhwa kuwa mfalme, malkia Bilqis au Sheba alikua malkia wa ethiopia au kush akaskia sifa za hekima za mfalme suleiman kwa hiyo akaenda hadi israel akiwa na zawadi lukuki kutoka Afrika..
Sasa hapo ndio inasemekana alitembea nae na kuzaa nae kabisa na mtoto huyo alikua mrithi wa ufalme wa ethiopia

Na huyo malkia alirudi ethiopia wala hakupata tena kurudi israel.
Sasa uzao ule ukaendelea Hadi miaka ya juzi ya 60 ndio utawala wa kifalme ukaishia kwa mfalme Haile Selasie baada ya kupinduliwa na kuuliwa na waziri mkuu Mengistu Haile Mariam.

YESU alizaliwa na Joseph aliekua wa ukoo wa Daudi, ila wao ni mtiririsho wa kizazi hicho ambacho kilibaki israel.

Kutoka daudi hadi YESU ni miaka 2000 na kutoka YESU hadi Haile Selasie ni miaka 1935

Kama ni kweli kuhusu habari ya Malkia wa Sheba basi Haile Selasie Babu wa mababu zake walikua Daudi na Suleiman..

Karibu
 
Ni sahihi kabisa kwa habari zaidi unaweza soma kitabu cha wafalme1 na 2 katika biblia na unaweza kusoma pia kitabu cha samweli. 1&2. Ukiweza soma vyote utajifunza mengi zaidi..kuhusu mfalme Daudi,na Suleiman.. Lakini pia ukisoma kitabu injili ya yohana katika biblia Agano jipya utaelewa vizuri habari za yesu kristo na Hugo msaidizi anayezungumziwa(roho mtakatifu) wakiwa wanaagizwa wanafunzi au wafuasi wake.wasiondoke Jerusalem mpaka wamepokea nguvu au huo uweza Wa roho mtakatifu... Japo kumekuwepo na upotoshaji mkubwa sana Wa habari hizi.
 
asante kwa picha mkuuu
 
Msaada wa majina ya hao simba wa africa ktk picha tafadhali
 
Sina tatizo kabisa na maelezo yako mkuu, ila hapo kwenye 'era' walizoishi Yesu na Selesie umenitatiza kidogo, yani sijakubaliana nacho kama kigezo

Yesu hakuwahi kusema huyo atakaekuja baada yake atakuja lini na ataishi wakati gani

Lakini pia hata yeye mwenyewe alipata kuishi kizazi cha mbali sana cha Yakobo japo anatabiliwa baada tu ya mwanadamu kuasi

Hivyo Selesie kupata kuishi hapa karibuni haiondoi dhana ya kwamba yeye sie aliyesemwa kua atakuja
 
Kuhusu Suleiman na Queen of Sheba Ni Kweli, na walizaa mtoto, lakini huyo mtoto Hana uhusiano wowote na Haire Selasie, Haire Hana uhusiano wowote na kizazi cha kifalme cha Enzi ya biblia!
 
lazima nikiri tu kwakweli kayaman wana namna yao ya kuelezea hasa chimbuko lao ambayo kwa kweli japo sina uhakika nayo sana ila inafurahisha sana kuna kaukweli nilikasikia story kama hizi wanadai ni mafunuo yanayowajia punde wanapokuwa wamepuliza na kukoka lile jani la Kondeni ndipo utakuta wanapotafuta uhalali wa kutumia jani la kondeni katika visa vya biblia hutumia kitabu mwanzo 1...ya kwamba Mungu anapotoa maagizo ya vyakula vya mwanzo vya binadamu
....''tazama nimewapa kila mche utoa mbegu ....zitakuwa chakula chenu"hapa bila kutafakari hukurupukia kwenye cannabis Sativa (bangi) hili la haille sellaise ni mwendelezo wa fafanuzi za ajabu za watu wa imani ya rasta!
 
Kuhusu Suleiman na Queen of Sheba Ni Kweli, na walizaa mtoto, lakini huyo mtoto Hana uhusiano wowote na Haire Selasie, Haire Hana uhusiano wowote na kizazi cha kifalme cha Enzi ya biblia!

Haile Selassie (Ras Tafari Mackonnen) is a direct descendant of King Solomon. He is descended from the line of Menelik 1 who was the product of Solomon and Queen Makeda of Sheba.

Ras Tafari's recognition as the 'Messiah' came after the prophesy of Marcus Garvey who said the blacks will find their salvation when 'a black king shall be crowned' and it happened that a few years later Ras Tafari was crowned Emperor Haile Selassie. The Rasta movement was born out of this occurence and they believe he is the saviour.

Rastas base a lot of the rules and practices of their religion on the book of Numbers in the bible.
 
Hakuna ushahidi was DNA unaothibitisha madai hayo. Inawezekana Haile selasie alizaliwa na vizazi vingine tu vya Ethiopia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…