Wiki tatu zilizo pita Kiongozi wa Mwenge kitaifa alitoa maagizo kuwa; Mabasi yote yanayo pakia na kushusha abiria nje ya Stendi ya Magufuli watoke huko na warudi ndani ya stendi.
Kumekuwa na utitiri wa vituo vya mabasi ya abiria maeneo mbalimbali ya jiji la Dsm haswa maeneo ya Shekilango hadi Urafiki. Mabasi hayo yanapakia na kushusha abiria katika maeneo hayo.
Kiongozi wa mbio za mwenge amesema kitendo hicho kinaikosesha mapato serikali, hivyo ameziagiza Mamlaka kuhakikisha kuwa Mabasi yote yanapakia na kushusha abiria katika kituo cha Magufuli.
Cha kushangaza hadi sasa bado mabasi hayo yanapakia na kushusha abiria katika maeneo ambayo sio rasmi, jambo hilo sio tu linaikosesha Serikali mapato bali pia usalama wa abiria ni mdogo sana
LATRA chukueni hatua haraka, ondoeni mabasi hayo kwenye maeneo hayo.