Je, Kuna umuhimu wa kuanzisha mahakama ya mafisadi?

Wadau wa JF,

Napenda kuuliza pia kuelimishwa juu ya hili hivi kuna umuhimu gani wa kuanzishwa kwa mahakama ya kifisadi kama hali yenyewe ndio hii.

Hivi kweli mahakama imeeakuta na hatia Mh Daniel Yona na Basil Mramba wa kuliinguzia taifa mabilion ya fedha halafu leo tuna ambiwa wamepewa kifungo cha nje cha kufanya usafi hivi hii ina makesense kweli?

Sasa kuna haja gani ya kuanzisha mahakama ya mafisadi kama tutakuwa tunawaonea huruma mafisadi hii sio hakhi hata kidogo na haingii akilini kwa mtu yeyote leo tuna ona masikini anaiba kuku kwa ajiri ya kitoweo nyumbani anakamwata ana hukumiwa miaka 10 jela na lakini fisadi aliye iba mabilion ya watanzania eti ana hukumiwa miaka mitatu tena kwa kifungo cha nje wana kiita cha kufanya shughul za jamii.

Jamanai mahakimu mtende haki watanzani hawajaridhishwa na hukumu hiyo ya miaka mitatu tena ya kufungo cha nje maana ndani sijui walikaa miezi mitatu tu kwa kweli inasikitisha.
Umuhimu wa kuwapo mahakama ya wahujumu uchumi na mafisadi ni mkubwa sana, hasa kwa sasa maana kule hawata hukumiwa hao maskini na wezi wa kuku ulio sema ila kule utasikia watu wanene tu na hata hivyo ime chelewa majangili,majipu,watakatishaji fedha mle ndio mwao.
 
Unao ushahidi wa hicho unachokisema?. Mbunge mmoja alifungiwa asihudhurie vikao viwili vya bunge kwa sababu ya hizo hizo habari ambazo mtu anaziongea mbele ya kadamnasi halafu anashindwa kutoa ushahidi. Ukitakiwa kuongea kwa kirefu uelezee jinsi majaji wanavyopokea orders unao uwezo wa kuuthibitishia umma?. Ni tusi kubwa sana kusema eti majaji wataagizwa, ni hawa hawa ambao wewe unapopata shida na kwenda mahakamani, wanatumia elimu zao katika kutatua shida zako.
Acha vitisho. Kwani wewe speech ya rais hukuisikia? Aliwaambia majaji wahakikishe wanahukumu kesi haraka ili zipatikanr trillion moja ambapi katika hizo atawapa 250bn. What do have to say about that stayement. Remember a statement from a higher level is an order.
 
Mleta mada subira ya vuta heri, itakapoanza hiyo mahakama ya mafisadi yapo mengi tutakayokuwa kwenye nafasi ya kuyafahamu kwa undani. Yona na Mramba walifungwa enzi za JK. Wakati huo hata wazo la kuwepo kwa mahakama ya ufisadi halikuwepo. Wazo hilo tumeanza kulisikia wakati wa kampeni za rais Magufuli. Mfumo mzima wa uendeshaji wa mahakama hiyo kwa sasa upo kwenye mchakato ili baada ya miezi kadhaa mahakama hiyo ianze kazi.
lets keep waiting.....may be
 
Acha vitisho. Kwani wewe speech ya rais hukuisikia? Aliwaambia majaji wahakikishe wanahukumu kesi haraka ili zipatikanr trillion moja ambapi katika hizo atawapa 250bn. What do have to say about that stayement. Remember a statement from a higher level is an order.
Jaji Mihayo ametoa ufafanuzi wa kile alichokisema rais. Ujumbe wa rais ni kutaka mahakama iache kufanya kazi kwa mazoea, lazima iwe ni idara inayozalisha kitu kinachoonekana kwa taifa. Rais hana uhuru wa kuipangia mahakama au jaji wa mahakama jinsi ya kufanya kazi, ila anayo mamlaka ya kuwakumbusha kuwa uzembe wao na hasara za uzembe huo zina athari za moja kwa moja kwa maendeleo yetu sote.
 
Hakuna haja ya kutumia mabilioni ya Shilingi kuunda mahakama ya Mafisadi bali alitakiwa amuagize Jaji Mkuu ateue Jopo la Majaji wa kushughulika na kesi za Mafisadi. Mh.Rais ameshindwa kutofautisha Mahakama maalumu za Kimataifa na kibiashara, kwamba hizo zimewekwa hivyo kutokana na sheria zake kujitegemea. kesi za mafisadi ni za Jinai tu kama zingine. Haitaji kutumia pesa zote hizo kwa kuunda mahakama hiyo wakati mashuleni miundo mbinu mibovu, sera ya elimu bora ni uongo na wazazi wanaendelea kubebeshwa rundo la michango
 
Jaji Mihayo ametoa ufafanuzi wa kile alichokisema rais. Ujumbe wa rais ni kutaka mahakama iache kufanya kazi kwa mazoea, lazima iwe ni idara inayozalisha kitu kinachoonekana kwa taifa. Rais hana uhuru wa kuipangia mahakama au jaji wa mahakama jinsi ya kufanya kazi, ila anayo mamlaka ya kuwakumbusha kuwa uzembe wao na hasara za uzembe huo zina athari za moja kwa moja kwa maendeleo yetu sote.
Kwa hiyo wewe unaona kwa maneno yale alikuwa anawakumbusha kufanya kazi. We must be watching the same movie but unfortunately we are seeing different characters.
 
Kuanzisha mahakama ya mafisadi kwa dhana kuwa ndiyo utakuwa muarobaini wa ufisadi ni dhihaka na upotevu wa fedha. Hilo lingekuwa na faida kama tungekuwa na nia ya dhati ya kupambana na ufisadi. Nina shaka kama nia hiyo tunayo kwa sababu baadhi ya mafisadi tunaowajua tumeendelea kuwalundikia madaraka makubwa katika jamii. Lakini dhihaka nyingine ni kuwa mahakimu wale wale ambao wanaonekana hawajafanya vya kutosha kuwashughulikia mafisadi ndiyo watakaounda mahakama hiyo mpya ya mafisadi (maana haitegemewi kutoka nje ya nchi). Sasa weledi wao utaongezekaje kwa kuwepo kwao kwenye mahakama ya mafisadi. Hatari ile ya kuwashughulikia mafisadi itakuwa wakati huo imepungua? Wale waliopitisha makontena na ambao hawakuwa wamelipia makontena yao katika kipindi cha msamaha wa Raisi cha juma moja walifanywa nini? Mbona watendaji wengine wa serikali wanaoboronga wanapotimuliwa tunajulishwa iweje kuwe na usiri kwa wakwepaji hawa wakubwa wa kodi? Mahakama hii ikianzishwa itakuja kufa kama zilivyowahi kufa mahakama za wahujumu wa uchumi zilizoanzishwa kwa mtindo unaofanana na huu huu. Tuache maigizo
 
Kwa hiyo wewe unaona kwa maneno yale alikuwa anawakumbusha kufanya kazi. We must be watching the same movie but unfortunately we are seeing different characters.
Mimi naona kama vile lengo la rais sio kuwapangia majaji namna ya kufanya hukumu. Idara ya mahakama haijawahi kutokuheshimiwa na serikali kuu, unajenga dhana potofu kwamba rais magufuli anataka kuiburuza mahakama kitu ambacho sio kweli. Hana mamlaka hayo, amewakumbusha kuwa kuna kesi nyingi zipo pending na ndio sababu ya wao kupewa bilioni 12.5 ili fedha hiyo iweze kurahisisha utendaji wa kazi zao. Sio kweli kwamba rais anaingilia moja kwa moja maamuzi ya kesi, hapana, anataka wajipange upya, waachane na umwinyi na tabia za kuendeleza urasimu, tabia ambazo zinachangia katika mahakama kutoshindwa kufanya kazi kwa kasi kubwa. Kumbuka kuna mahakimu ambao wanashindwa kufikia viwango vya kesi wanazopaswa kuamua kwa mwaka mmoja, na hawa wanafukuzwa kazi. Kila idara lazima ijikite katika effectiveness na efficiency. Hapa kazi tu imejikita katika vigezo hivyo viwili. Ile kitu inayoitwa business as usual ilikuwepo katika awamu ya nne, hii ya tano haitaki kabisa uzembe.
 
Mleta mada subira ya vuta heri, itakapoanza hiyo mahakama ya mafisadi yapo mengi tutakayokuwa kwenye nafasi ya kuyafahamu kwa undani. Yona na Mramba walifungwa enzi za JK. Wakati huo hata wazo la kuwepo kwa mahakama ya ufisadi halikuwepo. Wazo hilo tumeanza kulisikia wakati wa kampeni za rais Magufuli. Mfumo mzima wa uendeshaji wa mahakama hiyo kwa sasa upo kwenye mchakato ili baada ya miezi kadhaa mahakama hiyo ianze kazi.
Ishu hapa sio majaji, ishu ni adhabu zilizotolewa kwa aina ya makosa wanayoshtakiwa nayo hao wanaoitwa mafisadi. Kisheria, hukumu inatolewa kwa mujibu wa sheria ikiwa na maana kuwa hukumu haitoki hewani, hakimu au jaji anahukumu kwa majumuisho yaliyotokana na ushahidi uliotolewa mbele yake lakini hukumu hiyo ni lazima iwe imetoka katika adhabu zilizowekwa kisheria! Mfano, kama sheria ya mazingira inasema mtu ataekaeshtakiwa kwa kosa la kuchafua chanzo cha maji, akikutwa na hatia atafungwa miezi 9 mpaka 12 basi hakimu atatoa adhabu kwa mtuhumiwa kifungo cha miezi 9,10,11 au 12 hata kama uchafuzi huo ulisababisha madhara makubwa mno, ndicho kilichofanyika hata kwa hawa kina Mramba, sheria ni mbovu, hazitungwi kuwabana watu wakubwa ila kuwabana wananchi wa kawaida. Kibaya zaidi ni kuwa wabunge karibu wote wanadream kushika nafasi kubwa serikalini ili wazitumie kujinufaisha kwa namna moja au nyingine hivyo hawathubutu kujiongezea adhabu pindi sheria kama hizi Zinapopelekwa bungeni kujadili. Majaji tungewalaumu kama wangekua wanatoa adhabu at their own descrition
Mleta mada subira ya vuta heri, itakapoanza hiyo mahakama ya mafisadi yapo mengi tutakayokuwa kwenye nafasi ya kuyafahamu kwa undani. Yona na Mramba walifungwa enzi za JK. Wakati huo hata wazo la kuwepo kwa mahakama ya ufisadi halikuwepo. Wazo hilo tumeanza kulisikia wakati wa kampeni za rais Magufuli. Mfumo mzima wa uendeshaji wa mahakama hiyo kwa sasa upo kwenye mchakato ili baada ya miezi kadhaa mahakama hiyo ianze kazi.
Mleta mada subira ya vuta heri, itakapoanza hiyo mahakama ya mafisadi yapo mengi tutakayokuwa kwenye nafasi ya kuyafahamu kwa undani. Yona na Mramba walifungwa enzi za JK. Wakati huo hata wazo la kuwepo kwa mahakama ya ufisadi halikuwepo. Wazo hilo tumeanza kulisikia wakati wa kampeni za rais Magufuli. Mfumo mzima wa uendeshaji wa mahakama hiyo kwa sasa upo kwenye mchakato ili baada ya miezi kadhaa mahakama hiyo ianze kazi.
 
Mimi naona kama vile lengo la rais sio kuwapangia majaji namna ya kufanya hukumu. Idara ya mahakama haijawahi kutokuheshimiwa na serikali kuu, unajenga dhana potofu kwamba rais magufuli anataka kuiburuza mahakama kitu ambacho sio kweli. Hana mamlaka hayo, amewakumbusha kuwa kuna kesi nyingi zipo pending na ndio sababu ya wao kupewa bilioni 12.5 ili fedha hiyo iweze kurahisisha utendaji wa kazi zao. Sio kweli kwamba rais anaingilia moja kwa moja maamuzi ya kesi, hapana, anataka wajipange upya, waachane na umwinyi na tabia za kuendeleza urasimu, tabia ambazo zinachangia katika mahakama kutoshindwa kufanya kazi kwa kasi kubwa. Kumbuka kuna mahakimu ambao wanashindwa kufikia viwango vya kesi wanazopaswa kuamua kwa mwaka mmoja, na hawa wanafukuzwa kazi. Kila idara lazima ijikite katika effectiveness na efficiency. Hapa kazi tu imejikita katika vigezo hivyo viwili. Ile kitu inayoitwa business as usual ilikuwepo katika awamu ya nne, hii ya tano haitaki kabisa uzembe.
I am not reffering to 12bn but to 250 bn that will be given to them after collecting 1tn. That was a promise.
 
KWANI Kwa Hizi Mahakama Tulizonazo Wamepelekwa Mafisadi Wangapi Hadi Leo!!!?? Tatizo Sio MAHAKAMA Zilizopo, Bali Mfumo Wao Wa Kuchukuliana HATUA KALI Za Kisheria!! KULINDANA!!! Wengine Wamefungwa Miaka 3 Gerezani, Matokeo Yake Wamekaa Miezi 7 Tu Waneachiwa!!!
 
Jamaan mi naomba msaada hivi kwanini hizi mahakam zinawekwa kuwa maalum kwa mfano hii ya mafisadi,kwanini mahakama hizihizi zisiwe zinasikiliza kesi zote ili kubana bajeti maan zitaanzishwa na hukumu yao utasikia kifungo cha nje huku kukiwa zimetumika pesa nyingi za uendeshaji wa mahakama hizi.
 
Uanzishaji wa mahakama bila sheria ya maana ni upotezaji wa muda na rasilimali. Mfano ni PCCB ilianzishwa lakini haikupewa uwezo wa kupambana na Rushwa in real sense ndio maana unaona rushwa inazidi tu kupamba moto wakati ttaasisi ya kuzuia ipo na ina watumishi wanaokula bure tu pesa za wananchi kupitia mishahara na allowances zao na kazi wanayoifanya haionekani na hata ingekuwepo ingeweza tu kufanywa na ofisi ya DPP na jeshi la polisi.
Mahakama zilizopo zinatosha sana, sheria zilizopo zirekebishwe ili adhabu kali ziwepo na pia makosa yaongezwe maana mpaka sasa sidhani kama ufisadi unatambulika kama ni kosa la kisheria, sanasana nadhani kosa ni matumizi mabaya ya ofisi ambayo ataetumia hovyo 5m za ofisi adhabu yake sawa tu na alietumia 11b!
 
I am not reffering to 12bn but to 250 bn that will be given to them after collecting 1tn. That was a promise.
Rais na jaji mkuu wote kwa pamoja wanazo taarifa kuwa mahakamani kuna kesi za madai ambazo kama zikisikilizwa vizuri fedha hiyo 1bn itapatikana. Rais anataka kesi hizo zisilale, zianze mara moja kushughulikiwa. Hivyo mahakama wanayo changamoto ya kufanya kazi as flexible as they can, ili waweze kupata hizo 250bn. Hakuna suala la kuinfluence hukumu, kama haki itakuwa ni kwa upande wa wale wanaodaiwa serikali haitapata kitu, kama itakuwa kwa serikali basi fedha zitaingia serikalini. Mimi nadhani lengo la speech kali ya rais kwa wadau wa mahakama, ni kujenga tabia ya mahakama kutolaza viporo, ujumbe wa rais ulikuwa ndio huo, kuondoa mazingira ya kizembe katika sekta ya mahakama. Hata kama kusingekuwa na matarajiio ya kupatikana 1bn bado rais angekuwa na haki ya kusisitizia mabadiliko ya utendaji kazi wa majaji na mahakimu.

Ungekuwa wewe ni rais magufuli halafu kuna fedha shilingi 1bn ambayo ipo tu lakini inaweza kuisaidia nchi, ila upatikanaji wake ni lazima watu wabadilishe mindsets zao, ungechukua maamuzi gani?. Kumbuka hizi fedha nyingi ambazo zinakuwepo tu, huchangia katika kuwafanya wakuu wa sekta nyingi wakatengeneza mazingira ya ufisadi. Nadhani unaikumbuka EPA.
 
Bila shaka ni maneno ya kutaka kuziteka akili zetu ili tuwachague coz ishu cio mahakama za kifisadi kuanzishwa ishu ni hao mafisadi kuchukuliwa hatua stahiki ikiwemo kufilisiwa na kufungwa jela.
 
Rais na jaji mkuu wote kwa pamoja wanazo taarifa kuwa mahakamani kuna kesi za madai ambazo kama zikisikilizwa vizuri fedha hiyo 1bn itapatikana. Rais anataka kesi hizo zisilale, zianze mara moja kushughulikiwa. Hivyo mahakama wanayo changamoto ya kufanya kazi as flexible as they can, ili waweze kupata hizo 250bn. Hakuna suala la kuinfluence hukumu, kama haki itakuwa ni kwa upande wa wale wanaodaiwa serikali haitapata kitu, kama itakuwa kwa serikali basi fedha zitaingia serikalini. Mimi nadhani lengo la speech kali ya rais kwa wadau wa mahakama, ni kujenga tabia ya mahakama kutolaza viporo, ujumbe wa rais ulikuwa ndio huo, kuondoa mazingira ya kizembe katika sekta ya mahakama. Hata kama kusingekuwa na matarajiio ya kupatikana 1bn bado rais angekuwa na haki ya kusisitizia mabadiliko ya utendaji kazi wa majaji na mahakimu.

Ungekuwa wewe ni rais magufuli halafu kuna fedha shilingi 1bn ambayo ipo tu lakini inaweza kuisaidia nchi, ila upatikanaji wake ni lazima watu wabadilishe mindsets zao, ungechukua maamuzi gani?. Kumbuka hizi fedha nyingi ambazo zinakuwepo tu, huchangia katika kuwafanya wakuu wa sekta nyingi wakatengeneza mazingira ya ufisadi. Nadhani unaikumbuka EPA.
Walijuaje kabla ya hao watu kushtakiwa na kusikilizwa?
 
Kukurupuka unlimited. Hii ndio tabu ya kuwa na serikali ya mtu mmoja aka serikali ya magufuli badala ya kuwa na serikali ya wananchi.
 
Walijuaje kabla ya hao watu kushtakiwa na kusikilizwa?
Jaji mkuu anampa taarifa rais kabla ya mkutano mkubwa. Kumbuka kuwa kila sekta nchini inaripoti kwa Rais. Kiongozi mkuu wa nchi hufanya kazi kwa kutegemea ripoti za walio chini yake. Anapoambiwa na jaji mkuu kwamba kama kesi zote za madai zikisikilizwa, zinaweza kupatikana shilingi 1bn, yeye anao wajibu wa kujenga mazingira ya upatikanaji wa fedha hizo.
 
Kama aliwasamehe watu waliokwepa kodi za kontena, usitegemee hiyo mahakama ikafunga mtu

Hakuna aliyesamehewa, kesi zinaendelea baada ya uchunguzi. Wazo lake kuu ni kwamba, mahakam hii itashughurika na kesi za namna hiyo tu. Kama ilivyo mahakama ya ardhi na ile ya biashara.

Kesi zikiwa specific na majaji specific zitaenda haraka kwa muda unaotakiwa, kwani hawa watakuwa wamespecialize. Tofauti ya kipindi kilichopita, uwajibikaji wa mahakama ulikuwa haufuatiliwi, na ndivyo ilivyokuwa dhana kuhusu hii taasisi kwamba hawawajibiki popote na hivyo kuwa miungu watu. Kwa sasa, kila mmoja atafanya kazi kwa sababu tulipofika (theory X) ni mpaka waone kuwa kuna anayefuatilia na anamaanisha.

Hakutakuwa na gharama kama inavyofikirika kwa sababu miundombinu ipo, ni kuset muundo tu na mambo yataenda.
 
Back
Top Bottom