Je kuna ulazima kwa kuwatoboa pua na masikio watoto wachanga?

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,326
7,350
Hii ni moja ya mada inayozungumzwa sana baina ya watu, na ina maoni tofauti kutokana na mtazamo wa mtu na mtu.
images - 2025-03-08T010305.626.jpeg


Tunafahamu kuwa ni wazi suala la malezi ya watoto katika kipindi hiki yamebakia kwa wazazi wenyewe huku athari zikiwa ni kwa jamii, tofauti na zamani ambapo mtu mwenye umri na rika sawa na wazazi wako basi naye ni mzazi na anaweza kukuadhibu bila jamii ya wakati huo kuona ni jambo la ajabu.
images - 2025-03-08T010405.609.jpeg


Kwa wale waliokulia miaka ya 1990 wanaelewa shughuli ya kutoroka shule muda wa mapumziko, ukikatiza mtaa wa kwanza ile unaongia mtaa wa pili unakutana na wadau wanakutia nguvu na kukucharaza bakora barabara na kukurudisha shule muda huo huo.
images - 2025-03-08T010945.706.jpeg


Ni katika kipindi hiki tunaamini kuwa kila mzazi ana machaguo na matanio yake kwa kizazi chake. Wapo wazazi ambao hupenda sana kuwachora watoto wao wa kike tattoo mapema kwa sababu ya msukumo wa kijamii, au kwa sababu wanadhani ni ishara ya uzuri na umaridadi ili kuendana na mitindo husika kwa dunia.
images - 2025-03-08T010453.735.jpeg


Wapo wale ambao huona ni vyema kichaga chake kikapendeza zaidi endapo kikiwa na tundu tano za kuweka here hereni kwa sikio la kulia na kushoto. Pia hufika mbali na kuwatoboa na pua ili wawe nadhifu zaidi wakiwa bado ni wachanga.
images - 2025-03-08T010518.754.jpeg


Wapo wengine hununua shanga za kutosha kisha uwavalisha watoto wao wa kike kwenye viuno vyao, na wapo wengine huwavalisha vikuu vichanga hivyo kwa muktadha wa kuongeza urembo kwa watoto wao.
images - 2025-03-08T010405.609.jpeg


Mwezi Januari nilipata kukaa mitaa fulani ndani ya jiji la Dar es Salaam, kwa hakika nilishangaa kuona watoto wadogo wenye umri usiozidi miaka 2 wakiwa na viuno vimejaa shanga huku pia masikio yakiwa na hereni za kutosha.
images - 2025-03-08T010518.754.jpeg


Ningependa kuuliza kwenu wadau kuhusu hili: Je, mnafikiri ni sahihi kwa wanawake kuwa na utamaduni huu kwa watoto wa kike mapema kiasi hiki?, na hususani kutoboa masikio au pua na kuwavalisha hereni na mapambo mengine?
images - 2025-03-08T010305.626.jpeg


Wapo wanaodai kuwa hii ni kutokana na kutokuwepo kwa baba na kuna kundi jingine ambalo hudai kuwa ni mtindo wa kisasa unaohitaji kuzingatiwa kwa makini?

Ningependa kusikia maoni yenu kuhusu hili.
 
Mara ya kwanza hata Mimi nilikuwa nashangaa sana lakini baade nikaja kugundua ni tamaduni na mazoea ya kijinsia pia kumfanya Mtoto wa kike kujua urembo ni sehemu ya maisha yake mfano kuna Mkoa flani nimewai kukaa yaani kila mwanamke ametoboa pua
 
Mara ya kwanza hata Mimi nilikuwa nashangaa sana lakini baade nikaja kugundua ni tamaduni na mazoea ya kijinsia pia kumfanya Mtoto wa kike kujua urembo ni sehemu ya maisha yake mfano kuna Mkoa flani nimewai kukaa yaani kila mwanamke ametoboa pua
Kitoto kichanga kinavalishwa shanga za kazi gani Mkuu!?
 
Back
Top Bottom