JamiiForums: Unaweza kuwa VERIFIED, fuata hatua hizi

Poleni sana.

Hakuna aliyewalazimisha. Hao unaoona wako Verified hawakombwa bali waliomba wenyewe.

Sisi tunaitikia hitaji lao kwa kuweka utaratibu rafiki. Tunatambua wapo wengi wasiotaka kuwa verified, nao ni haki yao!

Msitie shaka, unavyoamua kuwa JF ndivyo utavyohudumiwa
Faida ya kuwa verified ni nini?
 
Maxence Melo
Ikitokea Kesi kama ile uliyolazimishwa kumtaja memba nadhani utalazimika kumtaja kama yupo na Verified anonymous ID. Hii ni kwa sababu mamlaka zitajua unaifahamu Hiyo ID.

Je Nikiverify ID yangu nawajibika Sasa kwa ninachokiandika? Kama nikifichua ufisadi wa Siro (mfano) nitalazimika kutoa ushahidi ee.
 
kwa maoni yangu
1.kila mtu atajiheshimu zaidi na atawaheshimu wenzake.

2. itapunguza ban kwa sababu kila mmoja ataepuka kutumia lugha zisizo faa.

3. tutafahamiana zaidi.

4. tutaaminiana zaidi ktk kupeana michongo/fursa.
n.k
kabla hujachangia mjadala wowote naamini kila mtu atajitafakari kwanza kama anaweza kuchangia kuliko ilivyo sasa kila mmoja anakurupuka tu!
sio lazima kila mjadala kila mtu achangie, unaweza ukafuatilia tu na ukapata faida na ikakusaidia sana.
Taja tena faida au umuhimu wa kila point/hoja uliyotoa hapo.
 
Mkuu Maxence Melo hii budge rudisha blue ya awali labda hapo upunguze ukubwa wa budge tu.
Haka karangi kapya hakajakaa mkao.
Nawasilisha
 
Hahahah, aagh wapi, kuwa verified ni kujilimit, mtu inabidi uteme nyongo bhana 😂😂😂😂
We angalia mtu kama Pasco na mwanakijiji topic zao ni zile za kuibia mpaka uwe na jicho la tatu ndipo utagundua kapigwa mtu, vinginevyo hawawezi kupiga misumari ya nguvu hasa!.
 
Wakuu,

Kumekuwa na maombi kadha wa kadha ya watu kutaka kuwa verified.

Tumeona vema tuweke urahisi wa mtu kuomba kuwa verified badala ya utaratibu wa awali. Kuwa verified kwako ni kwa hiari yako. Unaweza kusoma Sera yetu ya Faragha kama una concerns zozote > Privacy policy ambayo ina ufafanuzi wa kina.

Kwa wanaotaka kuwa verified, utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:

Utabonyeza (ukiwa kwenye web browser) sehemu imeandikwa Account, kisha fuata utaratibu huu:

View attachment 1897917

Utabonyeza "Request Verification Badge". Utaweza kuona sehemu inakuja na eneo la kuweka ujumbe wa kuwasiliana nasi ukiambatanisha na copy ya ID inayothibitisha majina unayotaka yawe verified ni yako

View attachment 1897898

Ukishatuma request, vumilia kidogo kwani itakuwa processed na ikiwa ina changamoto progress itaonekana kwako baada ya sisi kuwasiliana nawe kuhusu ombi lako.

Profile yako au ya mdau mwingine, ukipeleka cursor itaonyesha maandishi haya (mfano):

View attachment 1898044

ILANI:
1) Kwa waliokuwa verified awali, huna ulazima wa kufanya mchakato huu, lakini ikikupendeza kujaribu - UNAKARIBISHWA
2) Unaweza kuwa verified ukiwa na ID yako ya JF (not a real name) endapo tutajiridhisha kuwa ID ni mtu tunayefahamiana naye na maudhui ya akaunti yake hayashushi hadhi ya badge husika; mfano wa waliokuwa verified kwa IDs kawaida ni Bujibuji na Madame B.

Wanachama ambao ni VERIFIED wataonekana hapa: Verified Members

NB: Napokea requests nyingi za kubadili majina, tafadhali fanya hivyo mwenyewe kwa kutembelea https://www.jamiiforums.com/account/username

Asante
Mkuu Melo inachukua wastani wa siku ngapi mtu kuwa verified?, maana naona bado nipo 'pending'
 
kwa maoni yangu
1.kila mtu atajiheshimu zaidi na atawaheshimu wenzake.

2. itapunguza ban kwa sababu kila mmoja ataepuka kutumia lugha zisizo faa.

3. tutafahamiana zaidi.

4. tutaaminiana zaidi ktk kupeana michongo/fursa.
n.k
kabla hujachangia mjadala wowote naamini kila mtu atajitafakari kwanza kama anaweza kuchangia kuliko ilivyo sasa kila mmoja anakurupuka tu!
sio lazima kila mjadala kila mtu achangie, unaweza ukafuatilia tu na ukapata faida na ikakusaidia sana.
Sasa hii si itakua Facebook au Instagram? Ukimfahamu mtu atataka kutuma mapicha weekend alikua wapi.

Mkuu Maxence Melo, tunashukuru kwa hili. Hoja kuu mezani kwa sasa ni katiba mpya ya Jukwaa la Wakubwa, mchakato unaanza lini?
 
Back
Top Bottom