JamiiForums ni moja ya sehemu nzuri ya kupima IQ ya watanzania wengi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,347
149,047
Nilichojifunza hapa JamiiForums ni kuwa unaweza kabisa ukafanya sampling ya watanzania na ukafanya research yako kuhusu uwezo wa akili ya mtanzania katika kufikiri, kujitambua, kujenga hoja na zaidi uwezo wa mtanzania kufanya reasoning ya mambo ya msingi kama vile kwanini Mr.X awe kiongozi wangu na si Mr.Y.

Kupitia JF Jukwaa la siasa, unaweza gundua kwanini watanzania hatuendelei, kwanini watu wanafeli mitihani, kwanini elimu yetu inashuka, kwanini Tanzania ni masikini, kwanini tunachagua viongozi wabovu, kwanini watanzania wengi ni watu wa kuburuzwa na wanasiasa na watu wengine wenye umaarufu au majina makubwa.

Watanzania wengi mpaka sasa hatujitambui ni wapi tulipo, wapi tulipaswa kuwepo na wapi tunataka kufika kama Taifa na wala hatujui tupite njia gani na badala yake tumebaki tunababaika mithili ya mtu aliepotea njia huku tukihangaika kupata mwenyeji(kiongozi) wa kutuonyesha uelekeo sahihi ili hali mwenyeji/wenyeji wapo na tunapishana nao humu humu bara barani tunamopita.
 
Nilichojifunza hapa JamiiForums ni kuwa unaweza kabisa ukafanya sampling ya watanzania na ukafanya research yako kuhusu uwezo wa akili ya mtanzania katika kufikiri,kujitambua,kujenga hoja na zaidi uwezo wa mtanzania kufanya reasoning ya mambo ya msingi kama vile kwanini Mr.X awe kiongozi wangu na si Mr.Y.

Kupitia JF Jukwa la siasa,unaweza gundua kwanini watanzania hatuendelei,kwanini watu wanafeli mitihani,kwanini elimu yetu inashuka,kwanini Tanzania ni masikini, kwanini tunachagua viongozi wabovu,kwanini watanzania wengi ni watu wa kuburuzwa na wanasiasa na watu wengine wenye umaarufu au majina makubwa.

Watanzania wengi mpaka sasa hatujitambui ni wapi tulipo,wapi tulipaswa kuwepo na wapi tunataka kufika kama Taifa na wala hatujui tupite njia gani na badala yake tumebaki tunababaika mithili ya mtu aliepotea njia huku IQ yetu ikishindwa kutuonyesha uelekeo sahihi.
Kwa mawazo yako unatupa ushauri wa aina gani? wewe uliyesoma zaidiyetu sisi Mkuu Salary Slip
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli
Iingine ushabiki maandazi watz wanaupenda sana

Kupitia JF Jukwa la siasa,unaweza gundua kwanini watanzania hatuendelei,kwanini watu wanafeli mitihani,kwanini elimu yetu inashuka,kwanini Tanzania ni masikini, kwanini tunachagua viongozi wabovu,kwanini watanzania wengi ni watu wa kuburuzwa na wanasiasa na watu wengine wenye umaarufu au majina makubwa.
 
Angalizo zuri. Unashauri tufanye nini sasa? Wabongo tu mabingwa sana wa kuainisha matatizo yetu lakini linapokuja suala la kutoa masuluhisho kusema kweli tunapwaya sana. Yes Watanzania ndiyo hawa hawa wenye IQ ndogo unaotuona hapa JF. TUFANYEJE ili tujikomboe?
 
Angalizo zuri. Unashauri tufanye nini sasa? Tuko mabingwa sana wa kuainisha matatizo yetu lakini linapokuja suala la kutoa masuluhisho kusema kweli tunapwaya sana. Yes Watanzania ndiyo hawa hawa wenye IQ ndogo unaowaona hapa JF. TUFANYEJE ili kuwakomboa?

"TUFANYEJE ILI KUWAKOMBOA....." Hii inamaana wewe Shimba ya Bunyenze haumo? Salary Slip hayumo? Basi nyie tukomboweni sasa
 
"TUFANYEJE ILI KUWAKOMBOA....." Hii inamaana wewe Shimba ya Bunyenze haumo? Salary Slip hayumo? Basi nyie tukomboweni sasa
Hapana. Bila shaka na mimi nimo mkuu. Nimesharekebisha kauli yangu hapo juu. Hata hivyo sikubaliani na kipimo cha IQ. Ni kipimo cha kibaguzi kilichowekwa na wazungu kwa minajili yao wenyewe. Ndiyo maana ukimpima mzee wa kule kijijini pengine atapata maksi za chini kabisa lakini je ni mjinga?
 
Wewe pia umejidhihirisha huna IQ kabisa. Msomi angetoa way forward.
Wewe ndo walewale
 
Tatizo sio tanzania tu, afrika yote. Hata ulaya na Marekani walikuwa hawajitambui,hadi 1650 up to 1800 ambapo yalifanyika mapinduzi ya fikra THE ENLIGHMENT ERA yakianzia uingereza na ujerumani (utafuatilia),Uthibitisho Benjamin Franklin alijitambua baada ya kwenda uingereza kikazi akiwa under 20 na kukfanya maamuzi magumu akiwa kwenye mashua wakati anarudi, baadae alikuja kuwa baba na muasisi wa taifa la Marekani.
englightenment-hero-H.jpeg

Wengi wetu tatizo ni mental programming yetu bado 75% ni negative imejaa poverty mentality na hata ufanye muujiza gani haiwezekani tukabadilika ila kitu kimoja tu.

Matokeo yake ni taifa la watu wabishi,wavivu,waongowaongo,wanaopenda mambo ya juujuu, wenye kupenda kurudishana nyuma, wivu na kila aina

suluisho;
wakati tunasubuli mabadiliko ya kitaifa ambayo wenda usiyaone hadi unakufa, anza mwenyewe na famila yako. Rekebisa bongo yako/rewire/reprogram fikra zako.

Unaanzaje? usidanganye na vitabu vya SUCCESS, Get rich in a second, Jinsi ya .....1,2,3,nk

anzia hapa ndio chanzo cha tatizo letu wengi.
Download hiki kitabu free, tafuta muda soma, hutabaki kama ulivyo, http://manniyati.weebly.com/uploads/2/1/7/2/21729006/what_to_say_when_you_talk_to_your_self.pdf
 
Amen! Nimekipata hicho kitabu. Nikimaliza kukisoma nitaleta mrejesho!
 
Wengi mnamshambulia mtoa mada bila sababu kwaani yeye ametolea mfano kwenye jf unavyo weza kugundua upeo wa mtu ktk kujenga hoja.Kwa jinsi tulivyo watz sitegemei taifa letu kupiga hatua ya kimaendeleo japo tuna kila kitu hapa nchini tutakachobaki kujisifia ni utulivu na hata kama haki zetu hatuzipati tunaridhika kwa mambo madogo huku mambo makubwa yakichukuliwa na welevu
 
Nilichojifunza hapa JamiiForums ni kuwa unaweza kabisa ukafanya sampling ya watanzania na ukafanya research yako kuhusu uwezo wa akili ya mtanzania katika kufikiri,kujitambua,kujenga hoja na zaidi uwezo wa mtanzania kufanya reasoning ya mambo ya msingi kama vile kwanini Mr.X awe kiongozi wangu na si Mr.Y.

Kupitia JF Jukwa la siasa,unaweza gundua kwanini watanzania hatuendelei,kwanini watu wanafeli mitihani,kwanini elimu yetu inashuka,kwanini Tanzania ni masikini, kwanini tunachagua viongozi wabovu,kwanini watanzania wengi ni watu wa kuburuzwa na wanasiasa na watu wengine wenye umaarufu au majina makubwa.

Watanzania wengi mpaka sasa hatujitambui ni wapi tulipo,wapi tulipaswa kuwepo na wapi tunataka kufika kama Taifa na wala hatujui tupite njia gani na badala yake tumebaki tunababaika mithili ya mtu aliepotea njia huku tukihangaika kupata mwenyeji(kiongozi) wa kutuonyesha uelekeo sahihi ili hali mwenyeji/wenyeji wapo na tunapishananao humu humu bara barani tunamopita.

Kama IQ ingepimwa kwa kigezo cha jinsi watu walivyopiga kura,basi miji mikubwa nchini hasa DSM ina watu wenye IQ ndogo sana
 
Back
Top Bottom