Wakuu, Kuna kitu sio cha kawaida ninapitia, Siku hizi JF haikidhi mahitaji yangu ya habari, burudani na maarifa. Miaka michache nyuma JF ilikuwa kila kitu. Mijadala ya kuvutia, kisima cha maarifa mapya, simulizi za kusisimia. Awali nilikuwa naweza kumaliza siku nzima JF pekee na nisitake site nyingine,siku hizi hata nusu saa nashindwa kumaliza. Kwanini nafeel hivi siku hizi? Siku, wiki, miezi inaweza kupita sijapata kitu cha kuelimisha au kuburudisha. Hii hali ni mimi tu napitia au na wengine?