Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,535
Na Alastair Leithead
Mto Congo ni mmojawapo wa mito mirefu zaidi duniani.
Mto huu urefu wake ni 4,700km (maili 2,920) kutoka ndani kwenye kitovu cha bara Afrika hadi Bahari ya Atlantiki, ukipitia msitu wa mvua tele ulio wa pili kwa ukubwa duniani.
Mto Congo huyabeba maji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - taifa la kupendeza, lenye utajiri tele wa rasilimali na malighafi, lakini taifa lililokumbwa na misukosuko tele. Ukubwa wa DRC ni karibia Ulaya Magharibi.
Taifa hili ambalo wakati mmoja lilikuwa miongoni mwa mataifa tajiri zaidi Afrika limelemazwa na miaka mingi ya unyonyaji, na sasa raia wake ni miongoni mwa maskini zaidi Afrika.
Lakini katika maeneo unayopitia mto huo mkuu, kunapatikana madini mengi ya thamani kubwa, na wanyama pori tele wa kupendeza wasiopatikana kwingineko duniani.
Kwa miaka na mikaka ambayo maji ya mto huo yamekuwa yakitiririka kuelekea baharini, Mto Congo umechimba bonde lenye kina kirefu chini ya bahari, bonde la chini ya maji ambalo limeingia kwa mamia ya kilomita ndani ya Bahari ya Atlantiki.
Ukatumiwa vyema, Mto Congo unaweza kuzalisha karibu mara dufu ya umeme unaozalishwa katika bwawa kubwa zaidi la kuzalisha umeme duniani, Bwawa la Three Gorges nchini China, na kusambaza umeme maeneo mengi Afrika.
WAPELELZI WAZUNGU
Wareno walikuwa Wazungu wa kwanza kuugundua mto huo mwaka 1482, walipoyaona maji yaliyojaa matope na mchanga yakifika mbali ndani ya bahari. Waliyafuata maji hayo hadi wakafika kwenye pwani.
Walikutana na Ufalme wa Kongo - ufalme uliokuwa umepangwa ukapangika, na uliokuwa na mawasiliano na watu wa nje. Walikuwa wanajihusisha na biashara ya watumwa na pembe za tembo.
Lakini 100km (maili 62) ndani ukiufuata mto huo, kuna sehemu kubwa iliyojaa maporomoko ya maji ambapo huwezi kupita kwa kutumia boti au mitumbwi. Ilikuwa ni karne kadhaa baadaye pale mpelelezi maarufu Henry Morton Stanley alipokuwa Mzungu wa kwanza kusafiri umbali wa mto huo wote.
Henry Morton Stanley na, chini akiwa na usafiri kwenye maporomoko ya Mto Congo
Kutoka pwani ya Afrika Mashariki, ilimchukua siku 999 kufika pwani ya Atlantiki pwani ya magharibi - na kuwasili kwake katika mji wa bandarini wa Boma mwaka 1877 kulifungua njia ya watu kufika ndani ya Congo, na kulibadilisha taifa hilo daima.
Katika kipindi ambacho Wazungu walikuwa wakijitafutia himaya na koloni za kutawala, Mfalme Leopold II wa Ubelgiji aliifanya Congo kuwa mali yake binafsi. Alimwajiri Stanley kusimamia shughuli ya kuvuna utajiri wake, na pia kujenga reli kurahisisha usafiri.
Mfalme Leopold II
Kwenye kingo za Mto Congo, baadhi ya walioteswa zaidi na kufanyiwa unyama usioelezeka chini ya utawala wa Mfalme Leopold walikuwa ni watu wa jamii ya mbilikimo waliolazimishwa kuvuna raba kutoka kwenye miti msituni.
Mbilikimo bado huishi msituni wakiwinda wanyama, na kuchuma matunda ya porini.
KUPANDA NA KUSHUKA KWA MOBUTU SESE SEKO
Taifa hilo kubwa la Afrika ya kati linalofahamika kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) limekuwa likitumiwa kwa karne nyingi na watu kujitajirisha. Mwanzoni ilikuwa ni wapelelezi Wazungu, kisha Wabelgiji na mfalme wao katili na baadaye viongozi wa Congo waliojawa na ulafi na tamaa.
Mwaka 1960, taifa hilo ambalo kwa miongo mingi lilikuwa chini ya utawala wa Wabelgiji na kufahamika kama Congo ya Ubelgiji, lilijipatia uhuru wake.
Waziri Mkuu Patrice Lumumba (kushoto) na Waziri Mkuu wa Ubelgiji Gaston Eyskens wakitia saini hati ya uhuru, 1960
Baada ya uchaguzi kufanyika, waziri mkuu wa kwanza akawa Patrice Lumumba. Lakini baada ya misukosuko ya kisiasa, aliomba usaidizi kutoka kwa Muungano wa Usovieti.
Wakati huo Vita Baridi vilikuwa vimepamba moto na Ubelgiji na CIA wa Marekani waliingilia kati na kumuunga mkono mkuu wa majeshi Mobutu Sese Seko.
Alimkabidhi Lumumba kwa waasi ambao walimuua na kuukata kata mwili wake, kisha kuuyeyusha kwa tindikali.
Mobutu Sese Seko (1984) na, chini, mabango Lubumbashi: “Asante rais raia. Mobutu Sese Seko tumaini letu pekee.” (1979)
Mwaka 1965, Mobutu alichukua uongozi kama rais wa nchi hiyo baada ya mapinduzi ya serikali yasiyokuwa na umwagikaji wa damu.
Mara moja, aligeuka kuwa dikteta, ambapo alitawala kwa kuwagawanya na kuwazozanisha wapinzani wake na pia kuwatesa na kuwaua. Na kupitia ubaguzi, mapendeleo na rushwa, alijitajirisha kutokana na utajiri wa taifa hilo, alilolibadili jina na likawa Zaire.
Katika mji wa Gbadolite alikotoka, alijenga kasri kubwa la kifahari na uwanja wa ndege ambao ndege za kusafirisha bidhaa za anasa kama vile mvinyo ghali kutoka Ulaya zilitua na kupaa. Njia ya kutumiwa na ndege kupaa na kutua katika uwanja huo ilikuwa kubwa kiasi cha kuweza kutumiwa na ndege kubwa ya wakati huo Concorde - ambayo aliikodi mara kwa mara.
Lakini alipotimuliwa madarakani mwaka 1997, kila kitu kilisimama. Sasa ni mahame.
USAFIRI NCHINI CONGO UPOJE?
Miundo mbinu nchini DR Congo imo katika hali duni - si katika kasri la Mobutu na mji wake wa kuzaliwa pekee, barabara zimo katika hali mbovu maeneo mengi.
Katika taifa hili la ukubwa sawa na wa Ulaya Magharibi, ni vigumu sana kusafiri mbali.
Njia kuu pekee ya kusafiri mbali nchini humo ni Mto Congo, lakini hata mito inayomwaga maji yake katika mto huo haitumiki kwa usafiri kama zamani, au kama inavyotarajiwa.
Huwezekana kusafiri kwenye mto huo kutoka Kinshasa hadi Kisangani umbali wa 1,600km (maili 990), na ndiyo njia kuu ya kuwasafirisha watu na bidhaa nchini humo.
Huwa kuna msisimko fulani ukiwa kwenye mto huo - ni pahali ambapo watu hufanya kazi, kusafiri, kuishi na pia kufanya biashara.
UTAJIRI WA TAIFA TELE
DR Congo ina utajiri mwingi - misitu mikubwa iliyojaa miti na rutuba, na madini tele chini ya ardhi.
Ina dhahabu, almasi, uranium, shaba nyekundu na cobalt - kiungo muhimu kinachotumiwa katika kutengeneza betri za magari, na simu.
Mkoa wa Katanga, kusini mashariki mwa nchi hiyo, ndicho kitovu cha sekta ya uchimbaji madini nchini humo. Takriban 60% ya madini ya cobalt duniani yanapatikana DR Congo.
Madini hayo yanayotolewa kutoka kwenye mawe yenye rangi ya kijani iliyochanganyikana na buluu ni muhimu sana katika utengenezaji wa betri. Umuhimu wake umezidi hasa siku hizi ambapo magari ya kutumia umeme yameanza kutengenezwa.
Zamani, ilikuwa inapatikana kama bidhaa mojawapo wakati wa kufua shaba nyekundu, lakini hitaji lake limeongezeka na bei yake imepanda sana miaka ya karibuni.
Inahitajika sana kiasi kwamba machimbo haramu madogo ya madini yanachipuka, karibu kila pahali. Wanawake na watoto ni miongoni mwa watu wanaofanyishwa kazi katika migodi hiyo chini ya mazingira hatari.
Wachimbaji madini wakitenganisha mawe
Familia zenye uhusiano wa karibu na viongozi, wanajeshi na wababe wa kivita waliigeuza Katanga kuwa uwanja wa kujitajirisha, kujipatia pesa nyingi haraka kupitia mikataba na rushwa.
“Ufisadi ni moja ya changamoto zinazotukabili... tabia bovu ambayo tuliirithi tulipojipatia uhuru," anasema Lambert Mende Omalanga, waziri wa habari na mawasiliano, ambaye ndiye msemaji wa serikali ya DR Congo.
“Hatuwezi kusema kwamba tumeshinda, lakini bado tunajaribu kuizuia kwa sababu hatuwezi kuendelea kuwa nchi tajiri tukiwa na raia maskini.”
Sokwe
Harakati za kuchimba madini na kuutwaa utajiri ulio chini ya ardhi huwa zinaenda kinyume na juhudi za kuhifadhi misitu - ambayo ni makao kwa aina ya sokwe wanaopatikana DR Congo pekee duniani. Ni sokwe wa nyanda za chini za mashariki mwa Afrika.
MISUKOSUKO MASHARIKI MWA KONGO
Vita vimekuwepo mashariki mwa nchi hiyo kwa miaka 20 iliyopita. Watu takriban milioni tano wamefariki kutokana na vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe.
Vilianza pale wanajeshi wa Uganda waliokuwa wakiwaandama waliokuwa wamehusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 kuvuka mpaka na kuingia Congo.
Huku macho yao yakiwa kwenye utajiri wa madini wa DR Congo - na wakisaidiana na Uganda - walisaidia kumuondoa madarakani Rais Mobutu.
Lakini haikuchukua muda mrefu kabla ya mtu waliyemsaidia kutwaa madaraka - Laurent Kabila - kukataa uwepo wa majeshi hayo ndani ya nchi yake.
Juhudi za kumuondoa madarakani zilisababisha vita vilivyofahamika kama Vita Vikuu vya Afrika, ambavyo wakati vilikuwa vimechacha zaidi vilikuwa vinashirikisha mataifa tisa.
Makundi ya waasi waliokuwa wanavuka mipaka ya nchi yalizuka na mengine kugawanyika. Wababe wa kivita na watu wenye ushawishi walifadhili makundi ya wapiganaji, na hadi leo vita huendelea. Kinshasa haijafanikiwa kabisa kudhibiti maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa sasa kitovu cha vita ni Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini ambapo kundi la waasi limekuwa likiwashambulia na kuwaua raia, wanajeshi wa serikali na walinda usalama wa Umoja wa Mataifa. Waasi hao wameifanya vigumu kukabiliana na kuenea kwa virusi vya Ebola eneo hilo.
SIASA ZA MIAKA YA SASA
Joseph Kabila ametawala siasa za DR Congo kwa miaka 17 iliyopita.
Alichukua hatamu baada ya babake kuuawa na mlinzi wake mwaka 2001.
Uchaguzi mkuu uliokuwa umepangiwa kufanyika mwaka 2016 ulicheleweshwa kwa miaka miwili. Lakini sasa unafanyika akiwa hayupo kwenye karatasi za kupigia kura. Kwa hivyo, uchaguzi ukiendelea kutakuwepo na kiongozi mpya.
Upinzani una wagombea wawili wakuu, na Kabila naye ana mgombea wa chama chake. Na ingawa kwa muda kulikuwepo utata kuhusu kutumiwa kwa mashine katika shughuli ya kupiga kura, mitambo hiyo itatumiwa.
MUSTAKABALI
DR Congo ni taifa kubwa na la kupendeza ambalo limekwamishwa na historia ya uporaji, unyonyaji, utawala mbaya na pia ufisadi.
Wakoloni walioitawala walikuwa katili na wakandamizaji, na uongozi wake baada ya uhuru ulikuwa na ubinafsi na uliangazia zaidi kujitajirisha, raia wengi wakisalia fukara.
Tangu kuondolewa madarakani kwa dikteta Mobutu Sese Seko mwaka 1997, taifa hilo limegubikwa na vita na misukosuko ya kisiasa, ambayo kila wakati hutishia kugeuka na kuwa vita. Mamilioni ya watu hulazimika kuyakimbia makazi yao kila vita vinapozuka.
Makundi ya waasi, mibabe wa kivita na watu wenye ushawishi hutumia tofauti za kikabila kujifaidi kusiasa.
Taifa hilo ni maskini sana - na Umoja wa Mataifa unasema takriban watu 13 milioni kati ya raia wake 85 milioni wanahitaji usaidizi wa aina moja au nyingine kwani huishi katika ufukara uliokithiri.
Lakini ni taifa lenye vijana wengi na lenye nguvu na msisimko. Theluthi mbili ya raia wake wana chini ya miaka 25. Wana matumaini na ndoto kuu, na wanasubiri fursa kujiimarisha na kulikuza taifa lao.
Rais wa sasa ametuhumiwa kwa kuitajirisha familia yake kwa kutumia mali ya taifa na kwa kujaribu kunga'ngania madaraka, tuhuma ambazo amezikanusha..
Lakini sasa amekubali kwamba ataondoka madarakani, na uchaguzi unatarajiwa kufanyika.
Mabadiliko yanasubiriwa na DR Congo ina fursa kuu ya kujiimarisha na kurejesha hadhi yake na ustawi barani Afrika.