figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,661
- 55,497
Salaam Wakuu,Leo nimepita maeneo ya Mahakama ya Kisutu, Nikakuta Mkurugenzi wa kampuni ya VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL, James Rugemalira anatabasamu akiwa na ndugu zake wakipeana hugs na kuchumiana. Inaashilia kuna dalili nzuri leo Mzee wa Henken akaliona jua. Langu Dua.
Tarehe 19 Jun, 2017 TAKUKURU wawafikisha mahakamani Seth Na Rugemalila kwa uhujumi uchumi. walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu wakishtakiwa kwa makosa sita ya uhujumu uchumi, likiwamo la kuisababisha Serikali hasara ya jumla ya takriban Sh358 bilioni.
Wakili wa Serikali, Paul Kadushi aliyataja mashtaka mengine yanayowakabili wawili hao kuwa ni kula njama, kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kughushi, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na kuisababishia hasara Serikali.
Zaidi Soma:
1). TAKUKURU yawafikisha mahakamani Harbinder Sethi na James Rugemalira kwa kosa la Uhujumu uchumi
UPDATE:
Rugemalila yupo huru!
Mashtaka yake yameondolewa chini ya kifungu cha 91(1) cha Mwanendo wa Makosa ya Jinai