SI KWELI Pre GE2025 Jambo TV wamechapisha taarifa ikisema 'Maria Sarungi aitelekeza CHADEMA na hayuko tayari kuichangia kutokana na mgawanyiko

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu nimekutana na hii taarifa mtandaoni kwenye magroup ya facebook. Je, ni ya kweli?

===

𝗠𝗔π—₯π—œπ—” 𝗦𝗔π—₯π—¨π—‘π—šπ—œ 𝗔𝗧𝗒𝗔 π—§π—”π— π—žπ—’ π—žπ—”π—Ÿπ—œ π—–π—›π—”π——π—˜π— π—”

Mwanaharakati Maria Sarungi ameweka wazi msimamo wake kuhusu CHADEMA, akieleza kuwa kwa hivi sasa hayupo tayari kukichangia chama hicho.

Ameeleza kuwa sababu kuu ya uamuzi wake ni ukosefu wa mipango madhubuti ndani ya chama pamoja na mgawanyiko unaoendelea.

Kauli yake imezua mjadala mkali miongoni mwa wafuasi wa chama hicho na wanaharakati wa siasa, huku baadhi wakikubaliana naye na wengine wakipinga mtazamo wake.

Hili linakuja wakati ambao CHADEMA inaendelea kujipanga kwa ajili ya chaguzi zijazo na harakati zake za kisiasa.

1739510567495.png
 
Tunachokijua
Maria Sarungi ni mwanaharakati kutoka nchiniTanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia. Kadhalika Maria amekuwa akijihusisha na masuala mbalimbali ya siasa kwa kipindi kirefu sasa, ambapo amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kuendsha harakati zake ikiwemo X awali ukijulikana kama twitter.

Aidha hivi karibuni kumekuwapo upotoshaji ambao unamhusisha Maria dhidi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA hasa mara baada ya kufanyika uchaguzi ndani ya chama hicho na kumuweka madarakani Tundu Lissu kuwa mwenyekiti ambaye hapo awali alikuwa makamu mwenyekiti. Rejea hapa, hapa na hapa.

Kumekuwapo na chapisho linalosambazwa mtandaoni likidaiwa kuchapishwa na Jambo TV likiwa na taarifa inayosema 'Maria Sarungi aitelekeza CHADEMA na hayuko tayari kuichangia kutokana na mgawanyiko'


Je, ni upi uhalisia wa chapisho hilo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (keyword search) ulibaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli wala haikuchapishwa na Jambo TV kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Aidha JamiiCheck ilibaini kuwa Maria Sarungi kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii hakuchapisha tamko ambalo alidaiwa kulitoa likiwa na madai juu ya CHADEMA 'kukosa dira thabiti na kushindwa kuendesha siasa kwa ufanisi kutokana na mgawanyiko pamoja na ukosefu wa rasilimali fedha na yeye kushindwa kuchangia kutokana na kukosa ufadhili' ambapo madai hayo yakiwa na lengo la kupotosha.

Februari 12, 2025 kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X Maria aliweka ujumbe uliowataka viongozi wa Chama hicho kumpa kazi kujenga ushirikiano
screenshot-2025-02-14-152602-png.3236332


0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom