Jamani mbona michango ya huyu mwanasiasa imekosa wachangiaji?

Bado anakimbizana kujaribu kila kitu ktk hii dunia ambayo kila single na album inachuja haraka sana.....ni ngumu sana kudeka, kujifanya mpinzani wa kweli bila kumuumiza mtawala halafu ukawin..
 
Dhambi ya usaliti mbaya sana,hatuna muda naye! Cdm ndo baba wa kili kitu! Wenye uwezo njooni hapa PLAZMA Nyegezi Mwanza mpate kilaji kwa bili yangu,mimi c wale njaa kali buk 7!
 
Najiuliza sana sana sana sipati majibu. Ni dhahiri mwanasiasa Zitho Z Kabwe alikuwa akipost chochote kinachohusiana na siasa wachangiaji walikuwa wengi tofauti na ilivyo sasa. Kuna post imewekwa hapa kuonesha mchango wake kwa bajeti inayojadiliwa sasa lakini siamini response iliyopo. Jamani ni kwa nini? Hata wale watetezi wake kutoka ccm hawaonekani kuchangia na kumpongeza kama ilivyo ada yao. Natoa rai tuendelee kuwa nae na tuendelee kumuunga mkono pale anapotoa hoja zenye maslahi kwa taifa. Au mnasemaje wadau?
khaa!! Nyie bado mnawashwa tu nyenye zenu mkisikia jina la zito. Uzalendo wa zito huwezi kuulinganisha na uzalendo wa dr mbowe au dr slaa. Dr lisu na dr mnyika walikuwa majembe zamani lakini sasa hivi nao wameolewa tu wanapelekeshwa kwa sababu ya ulevi. Zzk bado hakuna wa kumlinganisha nae kutoka katika genge la wahuni
 
Kajishushia heshma aliyojijengea kwa kipindi kirefu.Ni aghalabu kwa wanasiasa wenye mpango wa muda mrefu kuangukia pua kama yalivyo mkuta Mh.amejiharibia ndani mda mfupi sana.Pole Mh.
 
Hakyanani usiombe ukachukiwa na wale waliokupenda, hebu jaribu kufuatilia Thread za mdada wa PM7 zipo hapa ndani. Yaani nimakombora tu yanapishana utafikiri tuko Bengazi ni shida sana

Kwa upande wa kamanda wangu Zitto kinacho mgharimu ni UMIMI umemtawala mno hata akiwa na jambo ambalo linahitaji umoja ktk kulishughulikia yeye anataka kuliwakilisha peke yake ili kununua sifa kwa Umma hiyo haifai ndio maana wenzake humzilia baadhi ya hoja azimalizr mwenyewe

Ukiondoa mapungufu hayo jamaa bado yuko vizuri anahitaji kutuliza kichwa ili ashughulikie baadhi ya mambo ikiwemo na mgogoro na viongozi wenzake ndani ya chama, Kikubwa alenge kupata amani na wenzie hata kama hatarudi au kurudishwa kundini basi wawe tayari kushirikiana kwa mambo yahusuyo Taifa ili kuimarisha nguvu ya upinzani hasa kwa wakati kama huu tunaojiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu hapo mwakani

BACK TANGANYIKA

Mkuu tatizo ni kwamba watu wamekosa imani nae. Kila analosema/kufanya zito hata kama ni zuri anaonekana kama ametumwa na wale wanaomtumia ili either kuwamaliza watu flan, kumjenga zzk mwenyewe au kuua upande wa pili. Hana namna ya kujiaminisha tena kwa watu.
 
Bado anakimbizana kujaribu kila kitu ktk hii dunia ambayo kila single na album inachuja haraka sana.....ni ngumu sana kudeka, kujifanya mpinzani wa kweli bila kumuumiza mtawala halafu ukawin..

amuumize anaempa ulaji!? Haiwezekan kwan bila ccm zzk na chama chake vitakuwa hoi.
 
''Siwezi kukataa wala kukubali kama nipo ACT'' unatoa kauli za kipuuzi halafu watu waendelee kukuamini
 
khaa!! Nyie bado mnawashwa tu nyenye zenu mkisikia jina la zito. Uzalendo wa zito huwezi kuulinganisha na uzalendo wa dr mbowe au dr slaa. Dr lisu na dr mnyika walikuwa majembe zamani lakini sasa hivi nao wameolewa tu wanapelekeshwa kwa sababu ya ulevi. Zzk bado hakuna wa kumlinganisha nae kutoka katika genge la wahuni

tulitegemea watu kama nyie muwe mnatokea kumuunga mkono japo kwa kuchangia mada zake kumbe tofauti. Hadi mshtushwe kama mandolin ya mjerumani!?
 
Kajishushia heshma aliyojijengea kwa kipindi kirefu.Ni aghalabu kwa wanasiasa wenye mpango wa muda mrefu kuangukia pua kama yalivyo mkuta Mh.amejiharibia ndani mda mfupi sana.Pole Mh.

Wewe ni ----. Kati ya zitto na chadema nani aliyeanguka?
 
Chadema zitto ndio alikuwa anawapa airtime ndio maana hadi leo bado mnahangaika naye. Wapuuzi wakubwa nyie
 
Tatizo la Zzt ni ubinafsi umemtawala, mpaka anataka mambo yake ndo yapewe kipaumbele kuliko mambo ya kitaifa (rejea msiba wa Bi. Shida)

Pili jamaa anajiona anaakili sana kuliko Mtanzania yoyote yule.

My take: akipandacho mtu ndicho akivunacho.
 
Njia nyepesi ya kurudisha imani ni kutogombea uongozi wowote ndani ya chama na ubunge pia. Kisha kutumia muda huo kujenga chama ikiwa ni pamoja na kuwapigia kampeni mahasimu wake. Or else tupa kule siasa na akafanye kitu kingine tofauti na siasa ikiwezekana nje ya nchi!!
Lakini kwa hali ya sasa ni ngumu kuaminika tena. Japo ni yule yule aliyetembea nao kwa miguu toka ubungo mpaka jangwani akiwa amevishwa taji la ushindi huku wakinyeshewa mvua pamoja (rejea janga la buzwagi) ukweli ni kwamba imani ya chama chake kwake imeporomoka saaaaana tena mno.
 
Chadema zitto ndio alikuwa anawapa airtime ndio maana hadi leo bado mnahangaika naye. Wapuuzi wakubwa nyie

Mpuuzi ni yule aliekuzaa, jieshimu kijana sio unaleta kauli zenye ukakasi humu. Akuna aliemtuma Zzk kufanya usaliti hivyo asira zako usituletee sie.
 
Najiuliza sana sana sana sipati majibu. Ni dhahiri mwanasiasa Zitho Z Kabwe alikuwa akipost chochote kinachohusiana na siasa wachangiaji walikuwa wengi tofauti na ilivyo sasa. Kuna post imewekwa hapa kuonesha mchango wake kwa bajeti inayojadiliwa sasa lakini siamini response iliyopo. Jamani ni kwa nini? Hata wale watetezi wake kutoka ccm hawaonekani kuchangia na kumpongeza kama ilivyo ada yao. Natoa rai tuendelee kuwa nae na tuendelee kumuunga mkono pale anapotoa hoja zenye maslahi kwa taifa. Au mnasemaje wadau?
Unafiki unakuwasha
 
Back
Top Bottom