Jamani kuna niliyemkosea mbona kila mara radi inapiga tu mkabala na dirisha langu ghetoni?

Unakumbuka uliweka thread hapa kuhusu "KELELE ZA WALOKOLE USIKU" haya sasa................ malizia hapo
hahahahahhaha
mbe!
 
Hayo Makabila uliyoyataja sio wataalam wa Radi, hao ni wataalam wa Mamba, unaweza kuliwa na mamba kutoka kwenye kikombe cha chai
Wataalam wa radi wapo Lyamba la Mfipa, wala hakuitajiki Mvua na vingu kubwa, inawezekana kukawa na jua kali tu, kikaja kivingu size ya sahani ya chakula na likafumuka radi la kuunguza Nyumba
Noo mamba ni malagarasi na kusini kigoma ila mjini na kasulu kibondo full kutumiwa vitu
 
Kama ni Uchawi basi nadhani huu sasa umezidi. Tokea mvua ianze kunyesha asubuhi hii hapa jijini Dar inayoambatana na Radi kali kabisa nashangaa hii radi haizunguki mbali na dirisha langu na hata ikianza tu kutoa ule mwanga wake unamulika ndani mwangu na ikipiga inapigia hapa hapa tu mkabala na dirisha langu kitendo ambacho kimenitisha na kuniogopesha mno.

Kuna Mtu kaniambia kuwa yawezekana nimembandua Mwanamke wa Kiha au Mkara au Mkerewe ( ambao ndiyo wenye aina hii ya Uchawi ) halafu sijamtoa mtonyo wake hivyo wanataka kunimaliza lakini kwa bahati mbaya sana sina kumbukumbu yoyote juu ya hili.

Naombeni msaada wenu tafadhali nifanyeje ili hii Radi ihame kuwa karibu na dirisha langu au kama kuna Member pengine yupo humu nimemkwaza hivyo anataka kunimaliza na hii Radi ajitokeze tu nimpigie magoti nimwombe radhi upesi.

Sidhani kama aina hii ya Radi ninayoiona ni ya Kisayansi bali nahisi ni ya Kiutamaduni zaidi.
 
sema Mungu katuahidi miaka 70 ukiwa na nguvu 80 .. mi nasimama na ahadi yake
Yote ni siri ya Mungu miss chaga, hakuna mwenye mkataba na Mungu, mtoto anazaliwa leo na anakufa leo, kesho itabakia kuwa ni siri ya Mungu.
 
Watu wa JF hebu kuweni serious. Mwenzenu anahitaji msaada nyie mnamkebehi? Kwanza Genta jiweke karibu na Mungu. Ukiwa karibu na Mungu utakuwa na uhakika kwamba atakulinda
Jambo la pili: Hata kama hizo radi ni za kutumwa (which I doubt very much because if it were so you would now be DEAD), kama ni za kutumwa basi anayezituma anakutishia tu. Jini la radi lisingekuacha. Ondoa hofu. Sali ukimpa Mungu shukrani kwa kukulinda. Labda Mungu anataka uache njia yako fulani mbaya. Tafakari ni baya gani umefanya kisha utubu kwa Mungu ukiweka ahadi kwamba hutarudia tena. Utaona mambo yataisha
 
Hiyo radi unayoiona na kuisikia inapiga mbali sana na hapo ulipo.Fahamu kua apigwae na radi hua haisikii Kama ukipona utashtukia uko hospitali tu.Usicheze na radi ndg.Ila Kama una tabia Mbaya uache Mara Moja.
 
Watu wa JF hebu kuweni serious. Mwenzenu anahitaji msaada nyie mnamkebehi? Kwanza Genta jiweke karibu na Mungu. Ukiwa karibu na Mungu utakuwa na uhakika kwamba atakulinda
Jambo la pili: Hata kama hizo radi ni za kutumwa (which I doubt very much because if it were so you would now be DEAD), kama ni za kutumwa basi anayezituma anakutishia tu. Jini la radi lisingekuacha. Ondoa hofu. Sali ukimpa Mungu shukrani kwa kukulinda. Labda Mungu anataka uache njia yako fulani mbaya. Tafakari ni baya gani umefanya kisha utubu kwa Mungu ukiweka ahadi kwamba hutarudia tena. Utaona mambo yataisha

Amina Mtumishi.
 
Back
Top Bottom