Jamaa yangu na mkewe wamejikuta kwenye group moja la kutafuta Wachumba huko FaceBook

Iwe na maziwa isiwe na maziwa vyovyote vile utachangamka
16072008ad32659a101fa3e503add0f0-3507751988.jpg
 
Ni matumaini yangu kila mmoja wetu ni mzima wa afya.

Kuna issue moja jamaa yangu kanisimulia na kuniomba ushauri nikashindwa hata pa kuanzia kumshauri asee.

Jamaa na mkew wako kwenye ndoa huu ni mwaka wa 5 wanaishi pamoja na wamejaaliwa kuwa na watoto wawili.

Jamaa anasema juzi jumapili wakt anaangalia angalia mtandaoni akaingia FaceBook akukutana na group moja linaitwa wanaotafuta wachumba, jamaa anasema yeye akaona aingie kuangaza macho, ila cha ajabu akakuta mkewe nae ni member wa hilo group.

Jamaa ni kama hajaelewa lengo la mkewe huyo kuwa kwenye group kama hilo wakt ni mke wa mtu.

Anaomba ushauri, achukue hatua gani?
unajua kwenye haya magroup kuna watu wana tabia ya kuchukua picha za watu wakapost, unakuta picha ya mdada mkali anasema anatafuta mchumba kumbe mhusika hata habari hana huenda ndicho kimempata mkewe.
Nakumbuka miaka 2016 kuna dada jirani yetu ilitumika picha kwenye group fulani la madada wanajiuza. Dada akaanza pigiwa simu eti anajiuza. Dada alihangaika polisi sijui wapi ili picha zake kuona kama zitaondolewa lakini juhudi zake hazikuzaa matunda.
 
Mnapata wap muda wa kupekuchua simu za wake zenu..

Kama mke anatimiza majukumu yake yote kwa mumewe hauna haja ya kupekuana pekuana & vice versa is True.
 
Hamnaga kuangaza macho huko, alikua kwenye process za kumcheat na kumkana mkewe.

Sasa nae kamkuta huko anataka kuleta zogo
 
Labda ali-join kipindi ambacho bado hajaolewa, facebook ni ya miaka mingi. Kama anaona ilo ni tatizo amuulize ilikuaje aka-join uko vile vile ajipange ikitokea na yeye akaulizwa alifuata nini uko.
 
Back
Top Bottom