Jakaya Kikwete analima lakini Graduates kutwa na bahasha za khaki kutafuta Sehemu za Kujitolea

Mkuu hio biashara nilishaiacha muda mrefu wa kutembea na bahasha za kaki na begi mgongoni vijana tuamke sio lazima kuajiriwa unaweza ukaanza kujiajiri na Mimi nawashauri kama utajiajiri na kujituma kwenye kilimo Cha mbogamboga utabadilisha maisha kwa muda mfupi
Hongera kwa Kulitambua Hilo Mkuu Graduates wa Bongo it's had to admit kuwa Ajira hazitawatosha na wanaona Kua ni Kazi ya Kuwadhalilisha

Na Ndo wako busy na Kufungua Saluni Unakuta Mtaa Mzima Umejaa Saluni
 
Kilimo kinahiyaji uwe na mtaji. Kwanza kulipata shamba lenyewe, pili kuandaa shamba lenyewe, tatu hela ya kulimia, nne mbolea au dawa za kuuwa wadudu. Ukipata shamba la bure, ujue kuyasafirisha mazao itakugharimu na kupata shamba lililopo karibu na mjini ni ghali sana.

Sidhani kama utaweza kulima na kupata mazao ya kueleweka kwa kutumia nguvu zako mwenyewe bila kuweka hata hela kidogo
 
hongera mtoa mada mm binafs nafuga kuku asee n good life pia natak kulima tangawizi na manjano baad ya 2020....nafungua tunakopesha kwaajili ya wale wa baasha ya kaki njian
Good idea mkuu kaza Watu wana panic kwa sababu hiki Kitu ni Kipya kwa Tanzania Ni tofauti na Maisha tuliokua tunasimuliana Shule kuwa ukisoma utaajiriwa na Kuwa bosi
 
Wewe mbona hulimi kutwa JF kupost upuuzi na kwenda Lumumba kuchukua book 7
Mkuu ni vema ukachukua ninayokuhusia Kuliko Kuyafata ninayoyafanya.

Imamu akizini nje ya ndoa usiukimbie msikiti
Padre akilala na sista haibadilishi ukatoliki
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwanza inabidi mtambue kuna mkulima alaf kuna mchuuzi ...mtoa mada ni mchuuzi na sio mkulima. Hongera mtoa mada kwa elimu nzuri kwa vijana lakini usijiite mkulima mkuu
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Tuamke tukaanze Kilimo wakuu hali ni mbaya siyo lazima wote mkaajiriwa. Mimi Roho huwa inaniuma Mtu anavyokuja na Kuandika thread nataka Sehemu ya Kujitolea bila Malipo hebu Imagine Sehemu hiyo unayojitolea vipi kama ungekua umeanzisha Kilimo cha Ekari Mbili za Vitunguu au ungekua unamiliki mgahawa kwa Pesa ulivyotumia kununulia Galaxy S7


Si sifa Asubuhi kuvaa Kiminini na high heels au Kuchomekea shati tayari kwenda kutumwa tena bure kuna Projects ulipiga Mara Mbili Kipato cha Mfanyakazi wa Halimashauri anayeanza Kitakua Mara Mbili

Nakumbuka mwaka 2016 Mfanyakazi wa Halimashauri mwenye Degree za Kawaida kama Uhasibu, Sheria ilikua ni 716,000/= before statutory deductions

Hapo Piga
NSSF= 10%
NHIF=3℅
Workers Comp=1℅
HESLB=15℅
Tax=25 Plus 14℅ ya Level 3

Aisee huyu Jamaa anaweza Kujikuta kwa Mwaka anapokea Tsh. 6,500,000 kwa mwaka kama Mshahara

Kuna Project sitazitaja ukizikodolea Macho unaweza kupiga Mara 3 ya hizo Pesa kwa mwaka wa 1.


Mimi mwenyewe nataka Niache Kazi tukapambane nimechoka Kutumwa.

Leo Rais Jakaya Kikwete alikua anakagua shamba lake Msoga.
View attachment 510659 View attachment 510660 View attachment 510661
Aiseeee I'm inspired.....ngoja ninoe panga niende zangu shamba miee
 
Back
Top Bottom