Mwizukulu wa Buganda
Member
- Nov 19, 2024
- 60
- 157
Jaji Warioba akiongea na waandishi wa habari leo Desemba 4 amesema haya
Ukiona mjadala wote uliofanywa tangu 2019 mpaka sasa, na imani iliyokuwapo kwamba uchaguzi wa mwaka huu (2024) hautofanana na ule wa mwaka 2019, lakini matokeo yake ni vilevile. Uchaguzi wa mwaka kesho (2025), kama hatutachukua hatua, utakuwa kama huu uliopita (Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024).
Tume itakayosimamia uchaguzi wa mwaka kesho, ni ileile iliyosimamia uchaguzi wa mwaka 2020, maana sioni dalili pamoja na sheria kupitishwa kwamba kuwe na tume tofauti, sioni dalili kama tume hiyo itaanzishwa kabla ya uchaguzi, kwahiyo ni tume hiihii ndiyo itakayoendesha uchaguzi wa mwaka kesho.
Watakaosimamia ni walewale ambao wapo chini ya TAMISEMI, uongozi wa kisiasa ni uleule ndani ya TAMISEMI, hawakusikiliza yote yaliyosemwa katika kipindi chote wakarudia ya zamani, hata mwaka kesho watafanya vilevile, tutakuta watu wanaenguliwa wengi tu, tutakuta kura za bandia na mengineyo.