Iweje ili mjadala wa Richmond Ufungwe?

Wataalamu wa kujifunza wanatumbia kuuliza maswali kunajenga uwezo wa kuelewa.Mimi nauliza maswali ili nijenge uelewa wangu kuhusu suala lenyewe liivyo! Mimi nina wazo kwamba labda njia sahihi ya kulimaliza hili jambo ni kwa Lowassa kufikishwa mahakamani, lakini wanaosema kinyume najifunza toka kwao kwa kuuliza maswali. kuhitilifiana mitizamo ni jambo la afya kwenye mijadala.
 
Mjadala wa Richmond utakwisha pale wahusika ambao wanajulikana kama EL watakapofungwa kwa uhujumu wa uchumi. Hakuna namna hapo hili ni Jambazi Sugu sana
 
Jk alizungumza akiwa mwanza......kama unachafuliwa kwa nini usiende mahakamani kusitisha tuhuma hizo? Ikiwezekana kudai hadi fidia kwa kuchafuliwa jina? Mambo haya yanafanyika duniani....na ww unajua....
Hivi kwa haya yote yanayotokea hivi sasa nchi hii unawezaje kupata ujasiri wa kumuamini jk ?
 
Mjadala wa Richmond utakwisha pale wahusika ambao wanajulikana kama EL watakapofungwa kwa uhujumu wa uchumi. Hakuna namna hapo hili ni Jambazi Sugu sana
Ww ndie unamjua mh lowassa lkn tujiulize kwann mpaka sasa hawajampeleka mahakamani? Kama ameitia hasara gvt kwann aendelee kula bata?
 
Ww ndie unamjua mh lowassa lkn tujiulize kwann mpaka sasa hawajampeleka mahakamani? Kama ameitia hasara gvt kwann aendelee kula bata?

Kwa sababu amejiunga na CHADEMA.

BTW Chadema si mlikuwa naye kwenye list of shame mlimsafisha lini? Au ni kwa sababu anawapa peremende?
 
Mkuu hakuna haja kabisa ya mjadala wa aina hii. Tena hauhitajiki wala hauna tija yoyote. Tunachosubiri ni kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi kama tulivyoahidiwa na wale wote wanaotuhumiwa kufisidi nchi akiwemo Lowasa (kama inavyodaiwa) na kadhia nzima ya Richmond kufikishwa mahakamani. Hapo ndipo ukweli utajulikana.

Mengine yote ni porojo za mitaani zinazoenezwa na mashabiki na wapiga debe wa wanasiasa ili kujifurahisha nafsi zao kwa akili zao finyu. Nchi imeliwa na hadi leo inaendelea kuhujumiwa vibaya sana na viongozi wakuu serikalini halafu sisi tupoteze muda kuendesha mjadala wa Richmond na Lowasa badala ya vyombo husika kuchukua hatua stahiki? Seriously? What has become of us? Basi tusishangae Mkapa kutuongezea tusi juu naye baada ya kuwa katuibia kikubwa kwa kutuita malofa na wapumbavu.
 
Kikao cha baraza la mawaziri chini ya JK kiliazimia kupatikane ufumbuzi wa haraka kuhusiana na tatizo la umeme.....JK alikabidhi kazi hiyo kwa Lowasa huku akisisitiza taratibu za tender na za kimanunuzi zifuatwe.

Lowassa kwa kutumia ubabe bila kujali taratibu za utoaji wa tenda akauteka mchakato wote wa kupatikana kampuni itakayo tatua tatizo la umeme kwa dharula. Kamati ya mwakyembe ilijidhihirisha pasi na shaka waziri mkuu alihusika yy mwenyewe moja kwa moja katika kuipatia kampuni tata na hewa ya Richmond tenda hiyo, majenereta ya kufua megawati 100 za umeme hayakuja na kampuni haikuwepo......

Lowassa akajiuzuru kwa hasira sana....bunge kama mhimili wa dola lilitoa maazimio ambayo yalitekelezwa kwa baadhi ya viongozi kujiuzulu....

Serikali kama mhimili wa dola mwingine uliridhia maamuzi yale na raisi kuvunja baraza la mawaziri na kuunda serikali mpya ( pinda akaibuka).....

Mhimili wa dola ambao bado haujathibitisha madai haya ni mahakama pekee. Kwa mtazamo wangu mtu aliyechafuka kwenye kadhia hii ni lowasa na umma unajua hivyo.....mwenye nafasi ya kutumia mhimili huu ulobaki kujisafisha ni Lowassa, lakini yy pia hataki kwenda mahakamani kusafisha jina lake anabaki kuongea mtaani kama wengine tunavyofanya.....jamhuri ilishampa adhabu lowasa kwa kumvua vyeo.....Lowasa kama kweli hahusiki na Richmond aende mahakamani na vielelezo vyote kuthibitisha hayo....yy ndio muhanga mkuu....akikaa kimya ataendelea kuwa fisadi aliyefanikisha dili hilo.....maana tayari bunge na serikali vimethibitisha
tueleze kachafuka kivipi?na ukitaka kujua kama ulikua ni unafiki kwa nini mpaka leo mnailipa(symbion) sioni ajabu maana watz kwa unafiki si mchezo
 
Kumbe mtu akiwa chadema yy hapelekwi mahakamani!


Akipelekwa mahakamani si mtaanza kulia kimanga? zamu yake inakuja JPM atawaweka wanakotakiwa. Hasa baada ya hawa hapa kutoa ushahidi Mbowe, Msigwa, Lema na Tundulissu bila kukusahau wewe mwenyewe si unapokea peremende?
 
mkuu kusema kuwa 'lowaxa kama ni fisad kwann CCM hawampelek mahakaman', huo ni unafiki. kwa sababu CDM mmekuwa mkisema kuwa "CCM inawalinda mafisad" iweje leo uje useme kuwa 'kama CCM wana ushahid wampeleke lowaxa mahakaman' haraf pia mkuu kumbuka hli swala la RICHMOND lina2kamua moja kwa moja sisi walipa kodi kupitia tanesco, hii inamaanisha kuwa hata ww raia wa kawaida unaweza kwenda kuilalamikia mahakama na kuitaka iingilie kati hii mikataba mibovu inayo2nyonya cc wananchi wa chini, lakn ukingoja mpaka CCM au CDM ndo wawapeleke mafisad mahakaman hapo utakua unasubir kwenye HAMNA, kwa sababu CCM na CDM "wote wanapenda MAFISADI"
 
Back
Top Bottom