- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Katika pita pita zangu, nimekutana na maada inayosema kwamba matunda kama nyanya yanaweza kushambuliwa na popo, au nyoka. Hivyo basi Ukiona nyanya ikiwa hivi(pichani) usipende kula mbichi au kuitumia kabisa kwa sababu Kuna wakati inakuwa imezuliwa na Nyoka, Popo au aina ya wanyama fulani wenye sumu kali inayoweza kudhuru afya yako.
- Tunachokijua
- Nyoka ni reptilia watambaao wasio na miguu. Kuna takriban spishi 3,000 duniani: wako kwenye mabara yote nje ya Antaktiki na Aktiki.
Kama reptilia wote wana damu baridi na ngozi ya magamba. Wote ni wala nyama na spishi mbalimbali hutumia sumu kwa kuwinda lakini nyoka walio wengi hawana sumu wanashika windo kwa miili yao au kwa mdomo tu.
Nyanya ni aina ya tunda linalolimwa sana ulimwenguni na hutumika kama mboga au kiungo kwenye mapishi mbalimbali. Nyanya ni tunda la mmea wa kisayansi unaoitwa Solanum lycopersicum, ambalo ni sehemu ya familia ya mimea inayojulikana kama Solanaceae au nightshade. Familia hii pia inajumuisha mimea mingine maarufu kama viazi, pilipili, biringanya, na tumbaku. licha ya ladha yake tamu au kidogo ya uchachu, nyanya ni chanzo kizuri cha vitamini C, vitamini A, na antioxidants.
Kumekuwa na picha inayosambaa mitandaoni ikimuonesha nyoka kang'ata nyanya huku ikiambatana na ujumbe unaodai kuwa Watu wakiona nyanya iliyotoboka(yenye vishimo) wasile nyanya hiyo kwani inaweza kuwa iling'atwa na nyoka na kuachiwa sumu na ivyo watu wakila watadhurika kwa sumu ya nyoka. Tazama hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa, hapa na hapa
Je, uhalisia ni upi?
JamiiCheck imefatilia Madai ya nyoka kula nyanya na kubaini kuwa Madai hayo Si ya Kweli kwani nyoka hawali mimea(majani) wala matunda kama nyanya au aina nyingine za matunda. Nyoka ni aina ya viumbe walao nyama (carnivores), chakula chao huwa ni wanyama wadogo kama panya, ndege, mijusi, mayai au hata nyoka wengine, kulingana na spishi.
Aidha, madai hayo yameeleza kuwa nyanya iliyoliwa na nyoka huacha sumu inayoweza kumdhuru Mwanadamu iwapo akila nyanya hiyo, Sumu ya nyoka huwa na madhara pale inapoingia kwenye mfumo wa damu, eidha kwa kung’atwa na nyoka au kupitia kwenye michubuko ya mwilini.
Sumu ya nyoka kwa kawaida haiwezi kudhuru mwili inapopitia kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kwa sababu inaharibiwa na asidi ya tumbo na vimeng’enya vya mmeng'enyo wa chakula(enzymes). Hata hivyo, haishauriwi kunywa au kula sumu ya nyoka kwasababu iwapo kuna vidonda au michubuko kinywani, kooni, au tumboni, sumu inaweza kupenya kwenye mfumo wa damu, na hapo ndipo inaweza kuwa na madhara.
Vile vile inategemea na aina ya Sumu ya nyoka kwani baadhi huathiri damu (hemotoxic) na nyingine huathiri mfumo wa neva (neurotoxic). Hata hivyo, sumu hizi huwa na madhara makubwa zaidi zinapoingia moja kwa moja kwenye damu kupitia kuumwa na nyoka. Hii ni kwa sababu sumu ya nyoka inaundwa kwa protini, ambazo huvunjwa kama protini nyingine yoyote katika tumbo. Hivyo basi madai ya sumu ya nyoka inayoachwa kwenye nyanya kuweza kudhuru binadamu atakayekula yanakosa nguvu kutokana na hoja hii.
Upi uhalisia wa Picha inayoonekana nyoka kang’ata nyanya? Ni picha halisi?
Jamiicheck imefatilia picha inayoonekana nyoka kang’ata nyanya na kubaini kuwa ni picha ni halisi na haijatengezwa.
Mnamo Septemba 20, 2024 ilipostiwa Video kwenye mtandao wa Instagram, video hiyo ilimuonesha Nyoka aking'ata nyanya. Video hiyo ilikuwa chanzo cha Madai ya nyoka kula Nyanya bila kutazama kwa nini nyoka alinng'ata nyanya, kitu ambacho kilisababisha Mwanzo wa Taarifa hii Potofu. (Fungua hapa kutazama Video hio)
Ukitazama video hiyo utaona nyoka huyo alikuwa amegandamizwa na ubao kwenye mwili wake hali iliyomfanya ashambulie nyanya zilizokuwa mbele yake sababu ya maumivu ya kugandamizwa na ubao na si kwa sababu yeye anakula nyanya au amedhamiria kutoboa nyanya.
Baada ya Video hiyo, Septemba 22, 2024 lilifanyika Jaribio la kuonesha kwa nini nyoka huyo alishambulia nyanya.
Kupitia Mtandao wa Youtube, Kwenye akaunti ya Jamal Al-Imwase alipost video ya jaribio la Nyoka aliyewekewa Nyanya mbele na kisha kugandamizwa ili kuona nini kitatokea, matokeo yalikuwa ni nyoka kuishambulia nyanya kama ilivyotokea kwenye video ya nyoka wa kwanza na kubainisha uhalisia kuwa Nyoka hali nyanya isipokuwa aling'ata nyanya kama sehemu ya kujilinda baada ya kugandamizwa na kuhisi maumivu. (Fungua kutazama video hiyo)
Aidha, Picha inayoonekana hapo Juu, ikimuonesha nyoka kang'ata nyanya kama ilivyowasilishwa na Mtoa mada ni Picha kutoka kwenye video hiyo ya jaribio ambalo lilifanyika ili kukanusha upotoshaji wa video ya awali kama ilivyoelezewa hapo juu.
Ambapo wapotoshaji walichukua Picha kutoka kwenye video hiyo na kuanza kusambaza tena upotoshaji kuwa Nyoka hung'ata nyanya na kucha sumu inayoweza kudhuru mtu akila kitu ambacho Si kweli. Aidha, Matundu kwenye nyanya husababishwa na wadudu, minyoo na magonjwa baadhi ya nyanya.
Uhalisia ni upi kuhusu Popo kula nyanya?
Popo ni wanyama aina ya mamalia ambao hutoka kwenye familia ya Pteropodidae ambapo chakula chao ni matunda, hasa yale yenye asili ya utamu kama vile mapera, nk. Kwa kawaida Popo hawawezi kula nyanya kwa sababu sio aina ya matunda ambayo popo hula.
Popo wanapenda matunda yenye juisi nyingi na ladha tamu, kwa hivyo nyanya sio miongoni mwa chakula chao cha kawaida.
Last edited: