Ukitaka kwenda peponi baada ya kifo chako, basi, sali, tenda matendo mema na ISHI KIFUKARA! Ndio, namaanisha! Fanya kazi yoyote halali lakini sehemu kubwa ya kipato chako kitumie kutimiza wajibu wako na hakika kusaidia masikini!
Huwezi kutumikia mabwana ( masters) wawili, so they say! Itakupasa uchague moja kati ya Mungu na Mali_ambayo mara nyingi ni a recipe for doom!!
Hakuna ajuae waendao mbinguni, lakini 'tetesi' zinaonesha mbinguni wamejaa masikini_ walioishi kwa wema hapa duniani.. Tuelewane: umasikini pekee sio 'an automatic ticket' ya kuingia mbinguni!! Sisemi hivyo! Bali tujue mali na utajiri vyaweza kuwa njia pana ya kujongea motoni... Nadhani katika hili hata vitabu vimedokeza kiasi..
Mimi naamini watu kama 'masista' na baadhi ya makasisi ndio waliochagua kazi bora zaidi hapa duniani. Wanaishi kifukara na tabia ya kujinyima... Wameacha shughuli zote za kuhangaikia mali na utajiri ili waweze kumtumikia Mungu kikamilifu.. Masista wengi siku hizi ni wasomi wazuri tu! Wangeweza kupata kazi 'nzuri' zenye ujira wa kutosha hata kuwawezesha kuishi kifahari! Lakini kwa vile Mwenyezi amewajalia neema na akili, wameamua kuishi kifukara_ na kutumia karama zao kama udaktari, ualimu n.k kutoa mchango wao katika ustawi wa jamii zao...
Wako pia makasisi na masheik ambao wanaishi maisha ya kimasikini huku wakitumia muda wao mwingi kwa masuala ya dini tu... Nasema wamechagua njia sahihi.. Hawahangaikii mali na utajiri ambavyo mara nyingi huwa ni recipes for doom.
Kuna baadhi ya wachungaji wanahubiria waumini wao kuwa matajiri! Wenyewe pia huishi kifahari na maisha ya kujikweza! Hawana unyenyekevu wala unyoofu inavyowapasa kuwa kama Biblia inavyowataka.. Baadhi yao nia yao si kuwaokoa watu bali kuyatumia makanisa kujipatia pesa kwa njia ya sadaka!! Hawa ni matapeli tu na yatupasa kuwaepuka kama ukoma!
Si dhambi kuwapuuza wachungaji na manabii wa uongo! Ndio wa uongo_ kwani kwa mujibu wa maandiko mitume na manabii wengi waliishi maisha ya unyoofu, ufukara na kujinyenyekeza. Bwana Yesu alisema mtu akitaka kumfuata sharti achukue msalaba wake!! ... Siku hizi baadhi ya wachungaji wanafundisha watu kuikimbia 'misalaba'!! Bwana Yesu alifundisha pia wafuasi wake kujishusha na siku zote alikemea unafiki!
Kuna wimbi kubwa la wachungaji wa uongo siku hizi lakini baadhi ya waumini wamekubali kuburuzwa kama ngo'mbe!! Ilipaswa watumie akili zao kutafakari yote yanayosemwa na wachungaji wao lakini isivyo bahati wao wameamua kuwa wajinga.. wapumbavu? Ishi kwa kiasi..
Mwanadamu anaaswa juu ya tabia ya choyo na ulafi....
Kwa akina dada, mama na bibi jijengeeni tabia ya kutoa.. Acheni kujaza minguo kwenye makabati na 'shangazi kaja'.. Nguo zote ambazo huvai gawa kwa masikini au ndugu na jamaa wasio na uwezo.... Hayo makenzi, mabazee, miviatu na vitenge usione choyo kupeleka kanisani au msikitini.. Ni bora ukagawa nguo zako ungali hai ili usiwape vishawishi ndugu zako kuzipigia mahesabu!
Nanyi akina kaka, baba na babu hizo suti za toka enzi ya Mkapa za nini? Gawa zote pamoja na mashati na suruali zinazokubana! Gawa mwenyewe ungali hali usije wapa changamoto ndugu zako kuzipigia kura suti zako!
Nawe mkulima ukivuna mazao yako, tenga kiasi cha kutosha kutoa sadaka, hususan kuwapa masikini... Kamwe usitoe mahindi mabovu au maharage yaliyooza... Toa mazao bora na baki na kiasi kiasi cha kukusaidia wewe na familia yako!! Wewe si unamuamimi Mungu? Basi usijaze maghala na maghala ya mavyakula kwani waweza kufa wakati wowote!!!
Dini inataka simplicity, modesty and humility sio kupayuka, mbwembwe, utapeli, choyo, ulafi na unafiki!!
Binadamu tumeumbwa na utashi! Huwezi kupata vyote! Chagua kimoja mbingu au dunia! Huwezi kupata vyote... Never!!!
.......