nchi ishauzwa na lakufanya hakuna
kilochobaki kila mmoja aangalie chake
DA
Mawazo kama yako yanahatarisha jamii kwa kukatisha tamaa.
Ndio mambo mengi machafu aliyosema IO yametokea na yanaendelea kutokea..lakini wananchi wana imani...IMANI ni kitu cha ajabu sana, bila hii tutarudi enzi zile za utumwa wa waziwazi..mambo yanabadilika sijui kama unaona hilo.
Mifano midogo midogo...
1. Nani leo alijua kuwa HakiElimu watakaa meza moja na PM kujadili mustakabali wao..?
2. Nani leo alijua JK atasema hadharani suala la kudai UK pesa ya Rada (ingawaje amechemsha..!!)..?
3. Nani leo alijua kuwa MTANDAO ndani ya CCM ungetokea..kwa mtazamo tu kama CCM ikiendelea hivi mwishowe wasambaratika na kuvunjika..makundi ndani ya chama yapo wazi wazi kuliko wakati wowote ule (Vita za Vyeo na Madaraka...damu inanuka ndani ya CCM..Je watakuwepo kama walivyo sasa miaka 10-20 ijayo..Je CCM ya leo ni ile ya miaka 10 iliyopita)..?
4. Nani leo alijua Ndesamburo angesema hadharani kuwa wabunge wamepewa rushwa..?
5. Angalieni miaka 10 TU iliyopita kulikuwa na shule ngapi za binafsi...fananisha na leo zipo ngapi zinazotoa elimu ya kweli...then weka maono yako miaka mingine 10 mbele..kizazi hiki tunachokisomesha leo by then kitakuwa kizazi kinachozalisha na kujua haki zao kuliko sisi wazazi wao leo..?
6. Nani leo alijua wazee wengi waliokuwa wanatanua maeneo ya O'bay na Masaki leo hii wamejenga vijumba vyao huko Pugu, Kimara, Mbezi n.k wengi wa watoto wao wakiwa ni wavuta bangi ambao wala hawawezi kuendeleza mali za wizi ambazo wazazi wao waliwatengea...?
7. Angalieni wazee/viongozi waliozulumu nchi enzi za Nyerere & Mwinyi wengi wao leo hii wapo wapi na wana mali kiasi gani...?
8. Kila kitu duniani kina LIFE CYCLE, nchi yetu hali kadhalika..hivyo kukata tamaa sio OPTION kabisa..hawa watoto na wajukuu wetu leo ni lazima tuwasaidie ili wakifikia umri wetu wasipitie haya tunayopitia sisi...Baba yetu Nyerere alituachia Uhuru (ambao kwa kweli hatujui tufanye nini nao...lakini tunao..!!) Vivyo hivyo bila kukata tamaa tunaweza kuwaachia Watoto/Wajukuu nchi yenye maendeleo. MIMI NINA IMANI