Iran yajaribu kupitisha Uranium Tanzania!

You guys are you forgetting RA, let us not go so far, he penetrated all way into the veins/arteries of CCM, his power of lobbying! Mind that we are the in a venerable situation, we fought the West and is a turn, as a trend goes on Asians are taking us! JF wakeup your country is going to the dogs!
 
IO, could this one person commands such an influence in the nation and in the party? how is that possible?
 
Nadhani haya mahusiano yanayozidi kati ya TZ na Iran, pamoja na ya Somalia na Ethopia ndio yanapelekea US kuweka kituo cha kijeshi Afrika.

Na mimi kwa upeo wangu huu mdogo, ninaziona kila dalili za balaa hili kumwaga ama kama sio TZ basi popote ndani ya EA, kuhakikisha kuwa TZ tunaendelea kupika mark time maisha.

Roho inanidunda kwelikweli maana 2008 is just around the corner.




NEWS zaidi hapa...

Marekani kuweka kituo cha kijeshi Afrika
WASHINGTON, Marekani

RAIS George W. Bush, juzi alisema kwamba ameridhia mpango wa kuanzisha kituo cha kijeshi cha Marekani kwa Afrika, hatua inayoashiria kuwapo mkakati wa kutaka kuongeza masilahi ya Marekani katika bara hilo.

Uamuzi wa Rais Bush umehitimisha mjadala mrefu juu ya wasiwasi wa Washington wa kuwapo kwa ongezeko la wapiganaji wa Kiislamu katika sehemu za Afrika huku pia ikivutiwa na utajiri mkubwa wa maliasili barani humo.

“Kituo cha mamlaka ya kijeshi Afrika kitachochea juhudi zetu za kuleta amani na usalama kwa watu wa Afrika na kuendeleza malengo yetu ya maendeleo, afya, elimu, demokrasia na ukuaji uchumi barani Afrika,” Bush alisema katika taarifa yake.

Nchini Ujerumani, msemaji wa jeshi la Marekani, Holly Silkman, aliliambia Gazeti la Stuttgarter Zeitung kwamba kituo hicho kitakachojulikana kama ‘Africom’ kitaweka makao ya muda huko Moehringen wilaya ya Stuttgart.

“Tayari tumeanza kuhama wiki hii. Kikosi hiki baadaye kitahamishiwa Afrika”, Silkman aliliambia gazeti hilo jana.

“Lakini huu ni mkakati wa muda mrefu,” alisema.

Bush amemtaka waziri wa ulinzi Robert Gates kuhakikisha kikosi hicho kipya, Africom kinaanza shughuli ifikapo mwishoni mwa Septemba 2008.

Marekani itashirikiana na washirika wake wa Afrika kutafuta kambi ya kikosi hicho, alisema.


Jeshi la Marekani limekuwa likiweka kambi za kijeshi sehemu mbalimbali duniani.


“Kikosi hiki kitatuwezesha kushiriki kikamilifu zaidi kuliko kupitia mpangilio wa sasa unaogawa Afrika kati ya kambi ya kati na Ulaya, mpango ambao umepitwa na wakati kutokana na kumalizika kwa vita baridi,” Gates aliiambia kamati ya kijeshi ya Baraza la Seneti Marekani.


Marekani imekuwa ikilipa kipaumbele Bara la Afrika katika miaka ya hivi karibuni kutokana na wasiwasi wa kuwapo kwa serikali dhaifu zinazoweza kuwa maficho salama ya wapiganaji wa Kiislamu.


Lakini pia Marekani imekuwa ikivutiwa na utajiri wa maliasili hususani katika kipindi hiki inachotaka kupunguza utegemezi wa mafuta kutoka Mashariki ya Kati kulikokithiri kwa machafuko.

REUTERS
 
MKJJ,
RA is not one man, for your information a buncvh of people are behind him, he controls big businesses in Tanzania, do you know that also he controls an offshore bank which operates in Tanzania? Who is behibd this? Amkeni.

Zinduka, wala usiwe na wasiwasi na Wamarekani, check our foreign policy and you will know what our destiny is!
 
MKJJ,
RA is not one man, for your information a buncvh of people are behind him, he controls big businesses in Tanzania, do you know that also he controls an offshore bank which operates in Tanzania? Who is behibd this? Amkeni.

Zinduka, wala usiwe na wasiwasi na Wamarekani, check our foreign policy and you will know what our destiny is!
 
IO, benki gani hii tena? this is getting more interesting, kwa sababu I have been looking for this one connection ya fedha kwa sababu I know for a fact not all the money wanaogawiana wakubwa zinaenda Uswisi kama watu wengi wanavyodhania.
 
Iran hawa jamani sijui hata la kusema . JK anataka nini hasa ?Lakini ukichukua deni kulipa ni lazima wacha tuone sasa anataka kulipa vipi .
 
nadhani MKJJJ angefanya na jinsi tunavyowafurahisha WAINGEREZA,WASWEDSH,WAJERUMANI, WAJAPANI,WACHINA,WAAMERIKKKA,WAFINISH bila kuwasahau WASAUZI AFRICA basi mjadala ungekuwa mzuri zaidi au mnasemaje?


nasikia bongo maconsultants wote ni wazungu kuanzia NORCONSULT mpaka huko kwengineko
 
MJJ,
Hii nchi ilivyoibiwa, na inavyoibiwa, siyo kama wewe unavyofikiri, it is an ernomous loss of wealth kama WaTanzania wangejua sijui vita gani ingeamka: Ask yourself huko KJJ kwako who benefits from the following:
1. Korosho zilizokuwa zinaibwa kwa kunuliwa kwa printable madafu, who were behind this? Since 1990s uptodate
2. Gold Sands which are being exported to "unknown countries" said to contain contaminated copper/chrome/ and platinum; do Tanzanians know the value of such wealth!
3. The deals between RA and Debeers(Anglo American) to accumulate sands from the gound for debeers: a dubous deal, do you know of unaccounted unpolished diamonds going out?
4. Tanzanites - A precious commodity only found in this country, but benefits India, Thailand, Hong kong. Why can't we refine them ourselves? The Indian trade association flew to Dar that year when a policy on mineral benefication was passed. Sumaye sat with these guys on the table, then next day was another story, Tanzanite are still flowing to India, Thailand and now Hong Kong (China) to be refined!
5. Are we really benefitting on construction projects? Our Enginners and architects are they getting the share of these huge funds?? Even if the money is paid in local currencies it will go in dollars and being cashed abroad. Let alone those projects funded by international organisations by foreign currencies!
6. Do we have any policy in wealth protection in case of retailing? Domestic market, export oriented economy? Who benefits from these?
7. Procurement benefits, Richmonduli, and all sorts, we even here that foreigners get tenders and also are given guarantees from the same government!

Mlolongo ni mrefu mrefu sana!!!!!!!!!

Aibu!
 
nchi ishauzwa na lakufanya hakuna

kilochobaki kila mmoja aangalie chake


DA

Mawazo kama yako yanahatarisha jamii kwa kukatisha tamaa.



Ndio mambo mengi machafu aliyosema IO yametokea na yanaendelea kutokea..lakini wananchi wana imani...IMANI ni kitu cha ajabu sana, bila hii tutarudi enzi zile za utumwa wa waziwazi..mambo yanabadilika sijui kama unaona hilo.

Mifano midogo midogo...

1. Nani leo alijua kuwa HakiElimu watakaa meza moja na PM kujadili mustakabali wao..?

2. Nani leo alijua JK atasema hadharani suala la kudai UK pesa ya Rada (ingawaje amechemsha..!!)..?

3. Nani leo alijua kuwa MTANDAO ndani ya CCM ungetokea..kwa mtazamo tu kama CCM ikiendelea hivi mwishowe wasambaratika na kuvunjika..makundi ndani ya chama yapo wazi wazi kuliko wakati wowote ule (Vita za Vyeo na Madaraka...damu inanuka ndani ya CCM..Je watakuwepo kama walivyo sasa miaka 10-20 ijayo..Je CCM ya leo ni ile ya miaka 10 iliyopita)..?

4. Nani leo alijua Ndesamburo angesema hadharani kuwa wabunge wamepewa rushwa..?

5. Angalieni miaka 10 TU iliyopita kulikuwa na shule ngapi za binafsi...fananisha na leo zipo ngapi zinazotoa elimu ya kweli...then weka maono yako miaka mingine 10 mbele..kizazi hiki tunachokisomesha leo by then kitakuwa kizazi kinachozalisha na kujua haki zao kuliko sisi wazazi wao leo..?

6. Nani leo alijua wazee wengi waliokuwa wanatanua maeneo ya O'bay na Masaki leo hii wamejenga vijumba vyao huko Pugu, Kimara, Mbezi n.k wengi wa watoto wao wakiwa ni wavuta bangi ambao wala hawawezi kuendeleza mali za wizi ambazo wazazi wao waliwatengea...?

7. Angalieni wazee/viongozi waliozulumu nchi enzi za Nyerere & Mwinyi wengi wao leo hii wapo wapi na wana mali kiasi gani...?

8. Kila kitu duniani kina LIFE CYCLE, nchi yetu hali kadhalika..hivyo kukata tamaa sio OPTION kabisa..hawa watoto na wajukuu wetu leo ni lazima tuwasaidie ili wakifikia umri wetu wasipitie haya tunayopitia sisi...Baba yetu Nyerere alituachia Uhuru (ambao kwa kweli hatujui tufanye nini nao...lakini tunao..!!) Vivyo hivyo bila kukata tamaa tunaweza kuwaachia Watoto/Wajukuu nchi yenye maendeleo. MIMI NINA IMANI
 
RA ni hatari. Iran inataka uranium. Iran inataka sphere of influence. Kalagabaho!
 
RA ni hatari. Iran inataka uranium. Iran inataka sphere of influence. Kalagabaho!


Waje wachukue wanachokitaka ili mradi na sisi tuchukue tunachohitaji kutoka kwao. Iwapo viongozi wetu wanaendelea kutusaliti basi kwa mwendo huu huu wa kinyonga tutawatambua na kuwamulika...mishowe tutafika. British Empire walitawala India na kuchukua malighafi zao kwa miaka 300 mfululizo lakini angalieni leo hii India ipo wapi...HAKUNA KULALA.
 
Naam, enzi zile kweli tulikuwa maskini hasa, lakini tulikuwa na uhuru wa kweli. Kidogo kidogo sasa tunazidi kuwekwa mifukoni mwa wajanja kwa visingizio vya kutafuta maendeleo.
Kidogo kidogo, tutaanza kuonekana wababaishaji wakubwa na tutaanza kudharaulika mbele ya mataifa mengine.
Miaka ile chini ya utawala wa Mwinyi kulikuwepo na miradi fulani iliyoanzishwa na hawa waIran huko Mkuranga; hivi hiyo miradi ilifikia wapi leo hii?
Misaada ya akina Bush na hawa wengineo itatutokea puani siku moja kama hatutakuwa waangalifu!
 
Interested observer,

Naomba nipe kwenye PM hiyo bank. Naelewa miradi ya jamaa kama Caspian na nyinginezo hiyo sijaipata.

FD
 
RA ni hatari. Iran inataka uranium. Iran inataka sphere of influence. Kalagabaho!

Hili ndilo jibu lenyewe. Nashangaa wengi wamekuwa wanalizunguka. Wenzetu wanaangalia masilahi yao ya muda mrefu, wakati sisi tunafurahia viini macho au mazingaombwe ya kupita. Irani wanataka nguvu za nyuklia kusudi wawazime nguvu marekani na ikiwezakana wawafyatishe mkia waisarael.

Kuhusu utaalmu kweli Irani wanao wa kutosha ingawa vile vile wengi wao wanakimbia nchi yao. Hakuna chuo Marekani, Canada, na Australia ambacho hakina muirani. Sijui sawasawa huko Ulaya
 
Wajameni,
Mengi yalizungumzwa Tangu BCStimes na bado yanaelezwa hapa JFna njia nyingi mbadala za kuleta maendeleo kupitia mageuzi ya uchumi na utawala na kufikia lengo la maisha bora kwa watanzania Lakini watawala hawasikilizi na hata kujifunza hawataki na kuyafanyia kazi ndiyo kamwe ni usiku wa kiza.
Kabla tulikuwa na mkoloni mgeni na sasa tunawakoloni wazawa ambao bado tunawaona ni wenzetu kwa kila baada ya miaka mitano kutujia na vitenge na sukari tuwape dhamana ya uongozi au tukoloniwe kihiyari.Katika mataifa mengi hakuna sehemu ambayo mkoloni ameweza kuiacha shibe ya kuchota mali bila ya kuondolewa kwa Nguvu,NADIRIKI KULISEMA HILI pamoja na kwamba naelewa litaleta hisia tofauti LAKINI kama kweli ni wakweli na tunataka mageuzi ya kiuchumi wa kweli basi tunahitaji mabadiliko ya sera nzima za kiuchumi ,uongozi bora chini ya katiba iliyo imara , kwenye uwekezaji na ugawanywaji wa hizo rasilimali na hao tunaowaita wawekezaji angalau kwa uwiano wenye kuleta hauoni kwa taifa ,udhibiti wa rasilimali na matumizi yatakanayo kwazo.Swali la msingi hawa waliopo madarakani wanalitaka hili?Nafikiri halipo kwenye matokeo chanya kwa upande wao kwa misingi ya wao kufaidika matokeo ya kuwepo kwa hao wanaoitwa wawekezaji.Hivi leo hii kuna mwananchi wa kawaida anaweza kutoka kifua mbele na akasema kwamba anafaidika na kuwepo kwa wawekezaji mbali na wale ambao wapo kwenye WANAWATEULE?
kama wapo ni vyema ,Lakini kama hakuna sasa kuna Faida gani ya kuwa nao?Kwa kifupi nguvu ya Umma inahitajika kuwaondoa hawa wakoloni wenza au wakoloni wazawa na hili litawezakana tu si kwa nia ya chaguzi zinazofanyika sasa kwa katiba inayotumika sasa, Bali kwa njia ya vyama mbadala kuanza kazi ya kutoa elimu kwa wananchi wote ngazi zote juu ya haki yao ya msingi ya kuwa na maisha bora katika nchi yao ,ambayo si masikini kama inavyodaiwa bali umasikini umesabishwa na dhulma inayofanywa kupitia kundi fulani la watu tuliowapatia dhamana ya kutuongoza na kufanya maamuzi kwa niaba yetu.Hawa wanaojiita vyama mbadala wanafanya nini kuhakikisha wana nguvu ya umma au wanasubiri chaguzi zianze ndiyo tuanze kuwasikia?Nafikiri wakiweza kufanikisha kutoa ufahamu na kupata ushawishi wa nguvu ya umma wanaweza kuleta mabadiliko ambayo yatafanya watawala wazinduke na kuwatumikia vyema wananchi.
 
Back
Top Bottom