Ipo sababu moja tuu itakayomfanya mwanaume amsamehe mkewe endapo atamfumania akiwa kwenye tukio

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
26,102
62,821
Anaandika, Robert Heriel

Vijana muache ubishi na ujuaji, oooh mimi siwezi msamehe mke wangu endapo nitamfumania amelala na njemba nyingine, hayo utayasema ukiwa timamu, unajiweza na nguvu za kutosha.

Mwanamke msaliti hata Shetani hawezi kumsamehe achilia mbali Mungu mwenye wivu mkali mno, sembuse sisi binadamu wenye mioyo ya nyama?

Hakuna mwanaume wa hivyo kwenye hii dunia atakayeweza msamahe mwanamke mchepukaji endapo akimshika. Lakini ipo sababu kubwa muhimu sana ambayo sisi wanaume kwa kweli tutakubali yaishe na kujifanya tumesamehe lakini kwa ndani inatula polepole.

Sababu hiyo ni kukosa nguvu za kiume.

Kukosa nguzu za kiume kupo kwa aina zifuatazo;

1. Kukojoa chini ya dakika mbili.

Ukiwa ni mtu wa kuwahi kumwaga, yaani ndani ya dakika moja umeachia, nakuhakikishia umekwisha, kivyovyote hauwezi kumridhisha mkeo. Likakuwa ni tatizo sugu, sasa utakuwa kazi yako ni kujipendekeza kwa mkeo ili aidha asikuache au asikutolee Siri zako, na hiyo ni siri kuu.

Uchunguzi wangu unaonyesha wanaume wengi wanaopelekwa pelekwa na wake zao wengi wao wanatatizo hilo. Hivyo hutumia namna ya kutetea haki za wanawake kama mwamvuli wa kuficha madhaifu yao.

Mwanaume kama unapiga kimoja chali tena cha dakika moja hata amfumanie mkewe kwenye tukio hana chakumfanya, zaidi ya kumsamehe! Atamuachaje sasa? Ili aumbuliwe? Maana mke atatoa hoja zake, na pia hawezi kuoa mwanamke mwingine ili aibu yake isisambae.

Hivyo atatafuta visingizio vya samehe saba mara sabini lakini kijeshi yapo makosa hata ufanyeje huwezi kusamehewa.
Kwenye mapenzi, kosa kubwa ambalo mwanamke atafanya ambalo hastahili msamaha ni kusaliti.

Na hata huyo atakayemsamehe kutokana na udhaifu wake, msamaha wake hautahesabika lolote kwani mwanamke yeye ndiye mwenye siri ya kambi kuwa kama asingekuwa hivi wala asingenisamehe.

Haliwezekaniki mwanaume anayejiweza kumsamehe mwanamke msaliti. Hiyo haipo na haitokuja kuwapo!

2. Kutokusimamisha.

Mwanaume anaweza akawa anasimamisha tangu akiwa mtoto mpaka anaoa, lakini zipo dharura zinazoweza kutokea katika maisha ambazo zinaweza kupelekea mwanaume apoteze uwezo wa kusimamisha, kuna ajali, magonjwa n.k.

Ukikutwa na dhahama kama hii kwa kweli hata umfumanie mkeo kwenye tukio, huna ambacho utafanya zaidi sana sana utamtetea au kumwambia afanye kwa stara ili kutunza heshima ya zamilia.

Ukweli wa wazi usiosemwa uliopo wa kwanini wanawake wa siku hizi wengi wanasauti ndani ya nyumba ni kutokana na wanaume wengi hatuwafurahishi wanawake zetu katika sita kwa sita.
Wewe ukiona mwanamke anamdomo sana, anajifanya ni mbabe, anakisirani, gubu, au kujifanya yupo sawa na mwanaume, wewe usihangaike naye, kaangalie mwanaume anayetoka naye.

Nakuhakikishia utagundua kuwa huyo mwanaume hana nguvu za kiume. Hafiki katika vilele vya huyo mwanamke ndiyo maana mwanamke anakuwa juu yake.

Na ukiona mwanaume anapenda sana kutetea na kuwapa mamlaka wanawake wawe nafasi sawa na wanaume, usihangaike naye wewe mtazame mkewe, halafu utakuja kuniambia. Wanaume wa namna hiyo wengi wao hawana nguvu za kutosha kutuliza hamu za wake zao.

Na mwanaume akishakosa sifa hiyo ndiyo hukimbilia kwenye mifumo hiyo ya kutetea haki sawa. Chunguza au hata kama ni wewe kama unatabia hizo lazima kitandani uwe sifuri, kama haupo hivyo nipo tayari unitukane kwa jina lolote lile.

Wazee wangu waliwahi kuniambia, ukitaka kujua nguvu ya mwanaume basi mtazame mkewe, na ukitaka kujua nguvu ya mwanamke basi mtazame mumewe.

Mwanaume kamili mwenye nguvu zake za kutosha, siyo pesa wala mali, bali nguvu za mwili kamwe hawezi kumsamehe mwanamke msaliti. Hiyo haiwezekaniki?

Wapo wamama wanaotoka kwa siri na kuwasaliti waume zao kwasababu waume zao wanaumwa labda ni Kisukari au Presha au magonjwa yoyote yanayoathiri mfumo wa damu na ubongo, yanayoathiri nguvu za kiume. Lakini hata waume zao wakijua uwezo wa kuwaacha ni ngumu kwa sababu nilizoeleza hapo juu.

Andiko hili, ni kwa mujibu wa mafunzo niliyopewa na babu zangu, ma-legendary.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
 
Kama na wewe unachepuka unahesabu ngoma draw, samehe tu.

Hakuna Draw inapotokea vita baina ya Mwanamke na Mwanaume, aidha mwanaume ashinde au ashindwe.
Draw inatokea Kwa watu au variable zenye Sifa zinazolingana.

Huwezi toa Draw kwenye Giza na Nuru,
Juu na chini,
Kushoto na kulia,
Wema na ubaya
Lazima kimoja kishindwe.

Mwanamke Kwa mwanamke wanaweza toa Draw,
Mwanaume Kwa mwanaume wanaweza kutoa Draw.

Alafu kingine mwanaume hachepuki.
Kumheshimu mwanamke kama Mke mmoja haimaanishi itaondoa nature ya mwanaume kuwa na wanawake wengi.
Hiyo mke mmoja tuu ni kujilazimisha na kumheshimisha tuu Mkeo lakini hata wao wanajua kuwa Mwanaume hawezi kuishi na Mke mmoja.
Ila wao wanaweza
 
Sasa taikoni, kwaio unataka kusema yule kaka mchungaji wa fili-firii chachi ana kasoro ndo maana kasamehe lile tunda kumegwa?🤔

Nimeeleza sababu moja tuu ambayo Sisi wanaume tunaweza kusamehe wenza wetu endapo tukiwakuta Red-handed na njema.
 
Si kweli, ni uwongo kabisa walahi
Sababu kuu ni mwanamke akiwa na pesa nyingi kuliko mwanaume! That’s it walahi
 
Si kweli, ni uwongo kabisa walahi
Sababu kuu ni mwanamke akiwa na pesa nyingi kuliko mwanaume! That’s it walahi

Hizo ni sababu namba mbili.
Ila haina uzito Kama hiyo hapo juu.
Hiyo mtu anafikiri nikimwacha tutagawana Mali alafu akicheki uwezo wa kujenga nyumba nyingine Hana au muda umeisha.
Noma Sana
 
Unauliza maswali ya kijinga wakati majibu nimeshakuwekea hapo juu.
Andiko hili halimkwepi yeyote, hata Mimi mwenyewe.

Ujinga ni huu unaoanika upumbavu wako hapa... kwamba watu waachane bila kujali consequence kwa familia na jamii... idiot unaedhani bilblia ndio mwongozo wa maisha kwa kila mtu
 
Kwa hiyo inawezekana Bishop naye ana matatizo tajwa hapo juu? maana alisema hata akimkuta red handed atamsamehe
 
Naona unaogopa kuongelea UCHUMI hasa ukiwa umeshikiliwa na waziri wa mambo ya ndani ktk ngazi ya familia(mama).
 
Unapaswa kuelewa kwamba swala la kusamehe au kutokusamehe ni very subjective. Simple.

Huwezi ku-generalize kwamba wanaume wote hawawezi samehe, hata kwa jicho la kisayansi hoja yako haiwezi kuwa na mashiko.

Wanawake wasio-samehe wanaume zao baada ya kuwafumania na wanawake wengine na wenyewe unawaweka kundi gani? Wanaume?

Kwa hiyo mwanaume anayezini Mungu hana shida naye sana?

Mwanaume tu aki-cheat ndo anapaswa kusamehewa? Mwanamke? Foundation ya hii hoja umeitolea wapi?

Mwanaume mwenye tatizo la nguvu za kiume ndiyo anaweza kusamehe, wewe unajua unobservable characteristics za wanaume wote? Na wanawake wanaoachwa na wanaume wenye matatizo haya ya nguvu za kiume baada ya kufumaniwa umewaweka kundi gani?

Mtiririko wa mada yako ulipaswa kuandika kisomi zaidi kwa kuangalia angle zote na siyo kihisia.
 
Ujinga ni huu unaoanika upumbavu wako hapa... kwamba watu waachane bila kujali consequence kwa familia na jamii... idiot unaedhani bilblia ndio mwongozo wa maisha kwa kila mtu

Nionyeshe kwenye andiko hilo ambapo nimeandika kuhusu Biblia?

Binadamu pasipo kuwa na kitabu cha Muongozo Hana tofauti na Mnyama.
Tuambie kitabu kinachokuongoza wewe ni kipi?
Ambacho hakisemi mtu akishikwa anafanya zinaa na ni Mke/ mume WA mtu Ndoa haitakiwi kuvunjiwa?
Ili ujue Mimi na Wewe Nani ni mjinga.

Sidhani Kama hata unazijua sheria za nchi yako kumaanisha kuwa wewe akili yako ipo chini.
Hujui kushikwa Ugoni ni moja ya sababu ya mtu kupewa Talaka kisheria?

Embu niambie unatumia kitabu gani kama Muongozo, ili watu wa Aina yako muone mlivyokuwa wajinga
 
Unapaswa kuelewa kwamba swala la kusamehe au kutokusamehe ni very subjective. Simple.

Huwezi ku-generalize kwamba wanaume wote hawawezi samehe, hata kwa jicho la kisayansi hoja yako haiwezi kuwa na mashiko.

Wanawake wasio-samehe wanaume zao baada ya kuwafumania na wanawake wengine na wenyewe unawaweka kundi gani? Wanaume?

Kwa hiyo mwanaume anayezini Mungu hana shida naye sana?

Wewe ndio unakosa mashiko,
Unaleta Sayansi kwenye mapenzi,
Sayansi haiwezi kuthibitisha Hisia za viumbe/binadamu. Sayansi haiwezi kuthibitisha Imani za watu.
Mapenzi ni hisia, ni Kama Imani, hasira, chuki wivu.

Sasa ukileta Sayansi kwenye mapenzi sidhani Kama tutakuwa tunajadili lolote.

Imani pekee ndio huamua vitu vya mwilini, Rohoni, akilini, hisia n.k,
 
Back
Top Bottom