Ipi ni lugha sahihi katika ya marehemu alale mahali pema peponi au marehemu alale panapostahili ?

Zero Competition

JF-Expert Member
Sep 12, 2018
310
451
Mara nyingi tunapoondokewa na wapendwa wetu ambao wametangulia mbele za haki huwa naonaga kuna misemo ya aina mbili ambayo watu huitumia katika kuonesha kuguswa na tukio la msiba.

Wengine husema marehemu apumzike mahali pema peponi na wengine husema marehemu apumzike panapostahili

Nini hasa utofauti wa hisi semi mbili na nini mtazamo wako juu ya hizi semi ?
 
Alale mahali pema peponi ni kama maombi kwamba tunamuombea licha ya yale aliyokosea hapa duniani,Mungu amsamehe na amlaze mahali pema peponi.

Alale panapostahili,hii ni kauli ya kusindikiza isiyo na maombi ndani yake,zaidi ni kuacha Mungu aamue,kwa yale aliyotenda marehemu,basi apumzishwe mahali pale anapostahili.
 
Mara nyingi tunapoondokewa na wapendwa wetu ambao wametangulia mbele za haki huwa naonaga kuna misemo ya aina mbili ambayo watu huitumia katika kuonesha kuguswa na tukio la msiba.

Wengine husema marehemu apumzike mahali pema peponi na wengine husema marehemu apumzike panapostahili

Nini hasa utofauti wa hisi semi mbili na nini mtazamo wako juu ya hizi semi ?
Anuani yako ingekuwa hivi "Ipi ni kauli sahihi..." badala ya "lugha" sahihi ungekuwa umepatia.

Ama kuhusu swali lako,kwa mtazamo wangu zote si kauli sahihi.
 
Tunaposema apumizike mahali pema in kma umamuombea,sababu hakuna mkamilifu
Ila unaposema apumzke panapostahili yaan hkumu anahostahili ndo apewe hio hio

Zamani ilikuwa watu wa dini zote akifa mtu
Tunamuombea kwa kusema alale pema peponi...

Walokole ndo wakaja kuharibu hii
Wakiona mtu sio mlokole ndo wanasema alale anapostahili...
 
Mtu akisema alazwe mahali pema peponi, ni kama anawafariji wafiwa tu. Ila ukweli mahali anapo stahili, kwasababu wengine walikuwa wema wengine walikuwa wabaya(matendo yao) wanaosema peponi kama wana mlazimisha Mola wapi huyu mjaa aende wakati mtoa hukumu ni Mwenyezi Mungu pekee. Na wanaosema anapo stahiki maana yake wamemuachia Mwenyezi Mungu amu hukumu kwa mema au mabaya yake.

Lunatic
 
Wengine husema marehemu apumzike mahali pema peponi na wengine husema marehemu apumzike panapostahili

Nini hasa utofauti wa hisi semi mbili na nini mtazamo wako juu ya hizi semi ?
Ya kwanza ni kama sala ya kumuombea makazi mema, regardless ya matendo yake hapa duniani, ya pili ni kama kumzodoa sababu ya chuki.
 
Mara nyingi tunapoondokewa na wapendwa wetu ambao wametangulia mbele za haki huwa naonaga kuna misemo ya aina mbili ambayo watu huitumia katika kuonesha kuguswa na tukio la msiba.

Wengine husema marehemu apumzike mahali pema peponi na wengine husema marehemu apumzike panapostahili

Nini hasa utofauti wa hisi semi mbili na nini mtazamo wako juu ya hizi semi ?
Mara nyingi maneno haya hutumika kwa ajili ya faraja kwa walio baki maana mtu akishafunga macho hasikii tena
 
Mara nyingi tunapoondokewa na wapendwa wetu ambao wametangulia mbele za haki huwa naonaga kuna misemo ya aina mbili ambayo watu huitumia katika kuonesha kuguswa na tukio la msiba.

Wengine husema marehemu apumzike mahali pema peponi na wengine husema marehemu apumzike panapostahili

Nini hasa utofauti wa hisi semi mbili na nini mtazamo wako juu ya hizi semi ?
kwahiyo, kwa marehemu kama Hamza tusemeje?
 
Zote ni lugha za kujifariji tu, hazibadilishi chochote kuhusu anapoenda aliyefariki.
Kwakuwa ni lugha za kuwafariji wanaobaki, lugha inayostahili kutumika ni alale pema peponi.

(hiyo kuongeza alale panapostahili sio kazi yetu, watajuana na Muumba wake huko) Ikumbukwe mazishi ni kwa ajili ya walio hai, kama lengo ni kufarijiana, basi zitumike lugha za faraja.
 
Tukiwa hai tuna chaguzi KUMTII MUNGU na KUTENDA MEMA.. AU KUASI NA KUTENDA MABAYA.

Tukifa Mungu ameshatuwekea stahiki zetu kulingana na chaguzi zetu tungali hai.

Hivyo basi, Uchaguzi wako unapelekea Stahiki yako.. SISI TUNAOBAKI HATUWEZI KUBADILI STAHIKI YAKO.

Kwakua hatuwezi kubadili stahiki yako, ni vyema tukisema.. MUNGU AMLAZE PANAPOSTAHILI/PANAPOSTAHIKI.

Ukweli Mchungu, Tutubu tungali hai.. KUNA MAISHA BADA YA KIFO.. Peponi Au Motoni.

Mimi na Wewe hatujui kesho yetu, TUTUBU MADHAMBI YETU NA KUREJEA KWA MUNGU NAE KWAKUA Ni Mwaminifu Atatusamehe.. haijalishi Umeua wangapi, umedhurumu wangapi, umezini mara ngapi, haijalishi umeenda kwa waganga wa jadi mara ngapi.. wewe tubu tu, UTASAMEHEWA.

Ee Mungu Uturehemu.
 
Mara nyingi tunapoondokewa na wapendwa wetu ambao wametangulia mbele za haki huwa naonaga kuna misemo ya aina mbili ambayo watu huitumia katika kuonesha kuguswa na tukio la msiba.

Wengine husema marehemu apumzike mahali pema peponi na wengine husema marehemu apumzike panapostahili

Nini hasa utofauti wa hisi semi mbili na nini mtazamo wako juu ya hizi semi ?
Ya kwanza inastaha ila ya pili inafaa zaidi
 
Tambuwa kuwa Mtu akifa malaika wanakuja kumchukua, kuna malaika wabaya na wema. Malaika mbaya akija kukuchukua unapelekwa Kuzimu na Malaika wema akija kukuchukua unapelekwa sehem Nzuri ukisubiria ile Safari ya kwenda pepon
Hayo maneno huwa tunayatumia
 
Ukiona huelewi unaweza tu kusema 'Atajua mwenyewe' na bado atafika anapotakiwa kufika.
 
Mara nyingi tunapoondokewa na wapendwa wetu ambao wametangulia mbele za haki huwa naonaga kuna misemo ya aina mbili ambayo watu huitumia katika kuonesha kuguswa na tukio la msiba.

Wengine husema marehemu apumzike mahali pema peponi na wengine husema marehemu apumzike panapostahili

Nini hasa utofauti wa hisi semi mbili na nini mtazamo wako juu ya hizi semi ?
Kiutu ni alale mahali pema peponi lakini kiuhalisia ni alale anapostahili
 
Back
Top Bottom