Investigative Journalism in Tanzania:Tatizo ni Umasikini, Katiba na Vitisho!-Jicho Letu Star TV.

Hizi sababu zote walizotoa ni kisingizio tu! Investigative Journalism inahitaji will and courage ya journalist tu! Hayo mengine ni ziada!
Mkuu Macho Mdiliko, nakubaliana na wewe, where there is a will there is a way, hivyo hiyo will itaopen doors za resources.

Kwenye magazeti wanaweza, lakini kwa sisi wa TV, zaidi ya will na courage, pia unahitaji resources na mwisho wa siku unahitaji huruma ya wakubwa vinginevyo hicho kipindi kitarushwa na TV gani? .

Paskali
 
Bulendu akacrush hoja ya resources, akasema mbona tulikuwa na Stan Katabalo na aliweza kwenye Kashfa ya Loliondo bila resources?, mbona Jerry Muro aliweza kwenye rushwa ya matrafick bila resources, mbona mwanahalisi waliweza kwenye kutekwa kwa Ulimboka, sio kila uchunguzi unahitaji resources kivile.

Bulendu akatolea mfano sakata vyeti feki la Bashite, limetokea hapa hapa Mwanza, waandishi wameshindwa kwenda Kolomije, Nyanza Primary, Pamba Secondary, Chuo cha Nyegezi, Kumfuatilia Paul Christian Original, etc etc, wameshindwa nini na walihitaji resources gani?!.

Bulendu akazishangaa media zetu kwenye selectivity ya prominence, na kutolea mfano wa hotuba ya Waziri Mkuu yenye mambo muhimu kitaifa na kiuchumi iliyochukua zaidi ya saa nzima kuwasilishwa, haikupewa umuhimu kama story ya Spika kumuita Mbowe na Mdee kwa kumtukana! . Uzalendo uko wapi?.

Hapa Doto Bulendu alitoa hoja na majibu sahihi..

Waandishi acheni kujificha nyuma ya kichaka cha resources na kutishwa...kwani wakati Mwanahalisi (Naizungumzia mwanahalisi ile ya kipindi kile kabla ya Richmond, sio hii ya sasa) inaandika habari za ufisadi na kuwa gazeti pendwa la wazalendo ilikuwa na resources gani na leo inakosa nini?

Wakati Jerry muro anafanya kile kipindi chake cha habari maalum alikuwa kituo gani?

Tatizo, wengi wenu mmekosa Creativity na mmekubali kununulika aidha na chama tawala au upinzani na mmeacha ethics zenu, Hivyo mmekosa Legitimacy ya kufanya investigative journalism.

By the way kutokana na kuchumia tumbo mmegundua kuwa kuandika matukio kila siku kunawalipa kuliko kufanya tafiti
 
Tatizo letu hapa si KATIBA, VITISHO, na UMASKINI.
Tatizo la issue nzima INVESTIGATIVE journalism hapa Tanzania ni WOGA na UMBEYA na UZUSHI.
Kuna tofauti kati ya Real investigative journalism na UZUSHI.

Hata huyo Mohamed Alli wa Kenya amewahi KUTISHWA si mara moja. Na si SERIKALI bali ni wale watu he WRONGLY rubbed shoulder with.

Maana yale anayoibuaga huwagusa wasiogusikaga kirahisi.
Na yale aliyokuwa akiatoa mengi yalijaa UKWELI.

Penye KWELI huwezi KUKAMATWA lakini penye UONGO hapo simpi mtu yeyote guarantee!
Ukisema ukweli wanakuulimboka au kukubensaanane tu.hata Ben alisema ukweli na full evidence ila kilichomkuata daaah
 
Back
Top Bottom