Insane Anahitaji Huruma, Kusaidiwa. Sio Kulaumiwa, Kulaaniwa na Kususwa! He Needs Help, Tumsaidieje?

Kwanza tuanze na kukanyana kwa unafiki,
Inaonekana mzee Shika siyo mwendawazimu kama watu walivyosambaza ujumbe kwamba ni mbovu wa akili,

Wengine wakasema hana nyumba anadaiwa kodi, kumbe watanzania unafiki tutauacha lini?
Mkuu Britanica, pole!. Nimemsikiliza the man is insane!, you can just tell by look, ila kwa sisi ambao tumefanya money transfer, hakuna malipo yoyote ya bima yoyote ku withdraw fedha zako kutoka benki yoyote, Zaidi ya kukatwa tax na kulipia bank charges ambazo zote zinakatwa, toka kwenye hiyo hiyo fedha yako!. Jamaa kasema anatakiwa kulipa bima ya us $ 150 ndipo alipwe.

Insane anatambulika just by look, the way he dresses, and his mode of life.

Hata Dr. Shika, ni insane anayehitaji kusaidiwa na sio kubezwa.
Pascal.
 
Acha kumuita Mwehu Mtu ambaye humjui! Usije onekana mwehu mwenyewe! Kwanza kwa Elimu yake tu na yako, tayari Mwehu keshajulikana!
Mkuu Pharaoh, pitia bandiko hili litakusaidia kujua aina tofauti za insanity, na baadhi ya maneno yana sound vizuri yakitamkwa kwa Kiingereza kuliko kutamka kwa Kiswahili.

Paskali
 
Matukio hufanywa na watu!
Idea ni zao la akili za watu!
Discussion hufanywa na watu!

Akili ya mtu imebeba megatones of power only to be derived and transformed. transformed. During that transformation some powers might become or seems to apear like impossible to originate from the person at the epicenter.

Hapo ndio tunajikuta kuwa tunapingana na usemi wako Pascal Mayalla (umeunukuu mahali) kuwa great mind discusses idea.

Idea, a megaton power from human brain can not be separated from the mighty body harbors it!

The idea is discussed together and alongside the initiator.

In that case huwezi kukwepa kumjadili mtu hata uwe na akili kubwa kiasi gani.

Kwa mfano kuna mtu mmoja muhuni anatoa tamko kuwa kujadili siasa ni marufuku!

Unajadilije wazo la kutojadili siasa bila kumjadili pia aliyetoa tamko hilo?

To me great minds discuss idea, events and people altogether as well as singular.

We all insane in different levels.

Wachizi wadhibitiwe na wachizi fresh wasipewe madaraka.
 
Matukio hufanywa na watu!
Idea ni zao la akili za watu!
Discussion hufanywa na watu!

Akili ya mtu imebeba megatones of power only to be derived and transformed. transformed. During that transformation some powers might become or seems to apear like impossible to originate from the person at the epicenter.

Hapo ndio tunajikuta kuwa tunapingana na usemi wako Pascal Mayalla (umeunukuu mahali) kuwa great mind discusses idea.

Idea, a megaton power from human brain can not be separated from the mighty body harbors it!

The idea is discussed together and alongside the initiator.

In that case huwezi kukwepa kumjadili mtu hata uwe na akili kubwa kiasi gani.

Kwa mfano kuna mtu mmoja muhuni anatoa tamko kuwa kujadili siasa ni marufuku!

Unajadilije wazo la kutojadili siasa bila kumjadili pia aliyetoa tamko hilo?

To me great minds discuss idea, events and people altogether as well as singular.

We all insane in different levels.

Wachizi wadhibitiwe na wachizi fresh wasipewe madaraka.
Mkuu Jogi, hizi levels za argument yako ni za juu sana kwa sisi watu wa kawaida kuelewa na kutenganisha kati ya kujadili watu na kujadili issues.

Mfano kuna baadhi ya viongozi wetu ni vichaa kabisa, ukiwajadili wao kama watu na kuwaita ni vichaa, utahesabika umewatukana viongozi wako hivyo kustahili adhabu, lakini ukiujadili ukichaa wao bila kuwataja, unakuwa umejadili issue ya ukichaa na sio kujadili watu hao vichaa.

Hivyo nasisitiza kwa mustakabali mwema wa taifa letu, sisi jf kama the home of Great Minds, tunapaswa kuwa Great Thinkers, hivyo tusi discuss watu, tunajadili issues na ideas.

Refer
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa Wengi Kuliko Tunavyojidhania?!.
Paskali
 
Mkuu Jogi, hizi levels za argument yako ni za juu sana kwa sisi watu wa kawaida kuelewa na kutenganisha kati ya kujadili watu na kujadili issues.

Mfano kuna baadhi ya viongozi wetu ni vichaa kabisa, ukiwajadili wao kama watu na kuwaita ni vichaa, utahesabika umewatukana viongozi wako hivyo kustahili adhabu, lakini ukiujadili ukichaa wao bila kuwataja, unakuwa umejadili issue ya ukichaa na sio kujadili watu hao vichaa.

Hivyo nasisitiza kwa mustakabali mwema wa taifa letu, sisi jf kama the home of Great Minds, tunapaswa kuwa Great Thinkers, hivyo tusi discuss watu, tunajadili issues na ideas.

Refer
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa Wengi Kuliko Tunavyojidhania?!.
Paskali
Mia kwa mia, tusimuudhi mchinja mbwa maana imenenwa kuwa tutakiepuka kichaa au wazimu na pengine vyote kwa pamoja(kichaa na wazimu)

Kuujadili uchinja mbwa mchinja mbwa haponi kujadiliwa, usimtajie "wehu" wake kama ndio jina lake, bali utambue kuwa "wake" ndio yeye! na "yeye" ndio mtu mwenyewe.
Kwa mfano ukisema "mbeleko ya vyeti feki"
Automatically mwenye mbeleko atasubiria umtaje kwa jina lake na anayebebwa atatega sikio kama mke wa matala!
Mwishowe huwi ispokuwa umewajadili watu.
 
ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya, alifikishwa mahakamani jana. Ni matokeo ya tuhuma zinazomuandama kwa muda mrefu sasa.

Yameshasemwa na yanaendelea kusemwa mengi. Hisia ni tofauti kuhusu yanayomtokea Sabaya. Kila mtu anataka aseme kitu. Nami nimeshaulizwa kwa nini sisemi chochote. Ngoja basi nitoe neno. Nitachukua muktadha maalum, bila kuingilia uhuru wa mahakama.
Tuhuma za Sabaya ni nyingi, zinaogopesha. Zinashangaza kupita kiasi. Zinahitaji akili ya juu mno kuzichambua. Ukizichukua tuhuma za Sabaya na kuziweka kwenye kapu la uhalifu sawa na uhalifu mwingine, hilo ni kosa kubwa.

Tafakari, Sabaya ni binadamu. Kila binadamu ana ubinadamu, vinginevyo kuwe na shida kwenye ubinadamu wake.

Tafakari zaidi, Sabaya akateuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya. Kazi ya kutumikia wananchi. Binadamu wenzake. Kila binadamu anafamu wito wa ubinadamu ni kuwatendea haki binadamu wenzake. Vinginevyo ubinadamu wake uwe na upungufu.

Inafahamika, kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa kiongozi ni zawadi kubwa mno. Kuilipa hiyo zawadi si kufanya chochote isipokuwa kuwatumikia watu kwa upendo na uadilifu.

Sabaya akiwa mkuu wa wilaya, akawa anatuhumiwa kupora mali za watu, kuonea anaowaongoza. Kulazimisha mapenzi kwa wanawake na hata kubaka. Hizo tuhuma ukizisikia, kama una kichwa kizuri lazima kwa asilimia 50 utadhani anasingiziwa.

Ni kwa sababu, mtu mwenye akili timamu hawezi kufanya hata robo ya yale anayotuhumiwa nayo Sabaya.

Mtu mzima anawezaje kuteka wake za watu na kulazimisha mapenzi? Anaingiaje kwenye hoteli na kulazimisha aoneshwe chumba cha mteja mwanamke, ili iweje? Anawezaje kulazimisha wafanyabiashara wampe pesa bila kufanyia kazi? Anawezaje kuteka watu na kuwatesa? Anafyatuaje risasi hovyo? Mtu mwenye akili timamu kweli?

Kwa kiongozi, vitendo vyote hivyo kwa sehemu kubwa vinanajisi uongozi. Je, Sabaya kama mtu timamu, hakutambua uongozi ni upendeleo na ulinzi wake ni uadilifu?

Ndio maana nikasema, tuhuma za Sabaya kwa asilimia kubwa hukaribisha hisia kwamba anasingiziwa. Maana mtu mwenye akili timamu hawezi kufanya japo robo ya vitendo anavyotuhumiwa navyo Sabaya.

Sasa, hata baada ya kufikishwa mahamani, lipo eneo la kulisemea. Ni namna ya kuingia ndani zaidi kwenye tuhuma zake.

Nimeshasema, ni kosa kubwa kuziweka tuhuma za Sabaya katika kapu moja la uhalifu, sawa na uhalifu mwingine.

Kama yote ambayo Sabaya anatuhumiwa nayo ni kweli kayatenda, basi uhalifu mkubwa upo kwenye namna ubongo wake unavyofanya kazi. Inawezekana haupokei na kutafsiri mambo kama binadamu wa kawaida.

Kama ndivyo, hata sasa akiwa mahabusu, inawezekana akawa haelewi kwa nini amekamatwa, kwani yote aliyokuwa anafanya (ikiwa ni kweli), yeye anaona alikuwa sahihi. Tena, si ajabu anajiona anasingiziwa.

Watu wenye namna ya kipekee katika kupokea na kutafsiri mambo kijamii huitwa "psychopath". Ni tafsiri sawa na mgonjwa wa akili. Kwa kawaida psychopath huwa wana matatizo ya afya ya akili.

Kama kutakuwa na dhamira ya kumtendea haki Sabaya, basi itabidi kumpima afya ya akili. Maana, kama kweli alitenda yote anatuhumiwa nayo, maana yake atakuwa psychopath. Mtu timamu asingethubutu kufanya hata moja ya 10 ya anayotuhumiwa kufanya.

Binafsi ningetamani, kabla hata hajafikishwa mahakamani, wakati wa kumhoji Sabaya ili kukamilisha taarifa za mashitaka dhidi yake, kungekuwa na wataalamu wa afya ya akili katika mahojiano.

Hapa sipendekezi Sabaya apewe msamaha kama tuhuma dhidi yake zina ukweli, la, haki itendeke. Wahalifu wenye matatizo katika afya ya akili hufungwa, ila kuna namna ya kuwasaidia kipindi wanatumikia adhabu zao.

Kinachonishawishi kuona ulazima wa Sabaya kupimwa afya ya akili ni kwa sababu nataka kujua ubongo wake ulikuwa unawaza nini alipokuwa akitenda uhalifu alioutenda. Hii ni kama kweli alitenda.

Je, ubongo wake ulikuwa unawaza nini? Kwamba yeye ni mkubwa sana kwa hiyo angetenda chochote kwa watu bila lolote kumrudia? Alikuwa anaamini ni haki yake kutendea watu alivyowatendea? Alichokuwa anakitafuta ni kipi hasa? Aliwahi kufikiria kwamba kila tendo lake baya lingemrudia? Ni ni kama kweli tuhuma dhidi yake ni za kweli.

Hata sasa, je, anachukuliaje mashitaka dhidi yake? Anahisi anaonewa? Anachukulia kesi dhidi yake ni ya kisiasa? Anajua mahali alipo? Au kuna mtu alikuwa anamtuma, anampa kiburi, sasa hivi hayupo? Kuna ulazima mkubwa wa kumpima afya ya akili. Itasaidia pakubwa.

Mtazamo wangu katika tuhuma za Sabaya upo hapa, ama anasingiziwa, na kama hasingiziwi, basi kichwani sio mzima. Ni psychopath.

©Luqman Maloto
Naunga mkono hoja, kama tuhuma zote zinazomuhusu Sabaya tunazosoma kwenye gazeti la Raia Mwema na mitandao ya kijamii, ni za kweli, then Sabaya ni Psychopath, ni insane, alikuwa hajui atendalo, anahitaji kusaidiwa. Hatua ya kwanza ni kupata wakili mzuri, atakayecheza na defence ya insanity.

Kuna uwezekano Ole Sabaya ni Insane, hivyo anahitaji kusaidiwa kama nilivyo shauri hapa,

Na hiyo insanity inawezekana umetokana na hoja za bandiko hili.

P
 
Wewe unijui mm jf kuna mtu alikuwa na sifa bora hapa jf kapambana na mimi sikuizi sifa zimeporomoka kuwa ni zuzu tu sasa wewe mwache huyo Pascal Mayalla nimuonyeshe kazi na huu ujinga wake
Hiyo ni ndoto ... ni upumbaavu ,....ukweli ni kwamba japo Rais tuliye naye ni mpuuzi kichwani ila alikurupuka kushobokea chanjo
fanya,
SASA WEWE BOYA
Pascal Mayalla mwandishi zuzu mkuu unatuambia ujinga gani

Hivi wewe kweli ni muandishi au uliokotwa jalalani, tumefanya upumbavuu au upuuzi,mimi point zangu nazitoa kama msumali wa moto
Hadi kuna kipindi JPM alinifuata pm pale nilipo mchana wazi wazi kuwa amekosea na mimi nikamwambia kuwa huo ni upumbaaavu
Wewe bila shaka utakuwa ni mmoja wa wasomi wa vyoo vikuu tz ,maana unaongea mafiii mafiii tu
Wanabodi, huyu ni mwana jf mwenzetu, namhisi kama hayuko sawa upstairs, he is insane, naombeni tumsaidie, kwanza ni ukikutana na post yake yoyote anatukana watu ovyo, kwanza mkongolee kitufe cha thanks, kisha usimjibu kwa ukali au kumtukana, be gentle muonyeshe tunampenda na tunamjali, wazimu utamshuka.

Nimeamua kujitolea kumsaidia huyu dogo, maana watu wa type hii wanahitaji huruma, upendo na kusaidiwa, vinginevyo watakuja kuishia kuokota makopo!.

P.
 
Wanabodi, huyu ni mwana jf mwenzetu, namhisi kama hayuko sawa upstairs, he is insane, naombeni tumsaidie, kwanza ni ukikutana na post yake yoyote anatukana watu ovyo, kwanza mkongolee kitufe cha thanks, kisha usimjibu kwa ukali au kumtukana, be gentle muonyeshe tunampenda na tunamjali, wazimu utamshuka.

Nimeamua kujitolea kumsaidia huyu dogo, maana watu wa type hii wanahitaji huruma, upendo na kusaidiwa, vinginevyo watakuja kuishia kuokota makopo!.

P.

Good idea, but my Question "Je Ni wewe tu anakujibu hovyo au na watu wengine? Maana Mimi naamini Wewe Ni mtu wa hovyo"
 
Good idea, but my Question "Je Ni wewe tu anakujibu hovyo au na watu wengine? Maana Mimi naamini Wewe Ni mtu wa hovyo"
Duh...!. Nimeweka baadhi ya post zake nikidhani mtu unasoma kabla ya kujibu.
Mimi nakiri sio mtu wa maana, mimi ni mtu wa hovyo, sasa tuendelee na mada iliyo mezani.
P
 
Duh...!. Nimeweka baadhi ya post zake nikidhani mtu unasoma kabla ya kujibu.
Mimi nakiri sio mtu wa maana, mimi ni mtu wa hovyo, sasa tuendelee na mada iliyo mezani.
P
Hakika umedhihirisha kwamba wewe ni kaka mkubwa; kaka mkubwa kwa kawaida hawezi kumchapa viboko dogo; thanks brother, ukubwa sometimes ni JILALA, kila uchafu unatupiwa wewe and you have to handle it
 
Wanabodi,

Angalizo: Great Minds hawadiscuss watu, wana discuss ideas na kutafuta solutions to the problems.
Hili sio bandiko la kumsema mtu, bali ni bandiko la somo linaloitwa psychoanalysis ambalo linahusiana na kwa nini binadamu fulani, anafanya jambo fulani, au kutenda tendo fulani la ajabu, watu wanashangaa, bila kujua kuwa mtu huyo ana tatizo, na anahitaji msaada, hivyo hili ni bandiko la kutoa solution to the problem ya kitu kinachoitwa, pseudo insanity.

Pseudo Insanity ni Nini?.
Kabla ya kuzungumzia pseudo insanity ni nini, kwanza tuzungumzia insanity ni nini?. Kwa kifupi insanity ni wazimu, mtu anayeitwa insane ni mwenda wazimu, lakini hii pseudo insanity sio wazimu kama wazimu kabisa, bali ni hali ya mtu kurukwa na akili kwa muda, na kupandwa na wazimu wa muda, na kufanya kitendo cha ajabu, kisha akili zake zinamrudia na kujilaumu, kwa nini ametenda kitendo kile. Usually huwa anajuta. Wengi wa watu wanaukubwa na hii pseudo insanity wengi huishia kuwa ma psychopath ambao ni watu wa hatari sana!.

Insanity ni Ugonjwa Kama Ugonjwa Mwingine Wowote, Isane Anahitaji Tiba.
Insanity ni ugonjwa, ni tatizo la kisaikolojia linalohitaji ufumbuzi wa kisaikolojia. Mtu insane ni mgonjwa, ni mtu asiyejielewa, asiyejitambua, hivyo anahitaji msaada wa matibabu kwa kusaidiwa kujielewa na kujitambua, anahitaji kutibiwa ili apone, kwa sababu insane yeye hajijui kuwa ni insane, na sio kulaumiwa, kulaaniwa na kususwa!. Insane is someone who seriously needs help and not ridicule!, hivyo badala ya kumlaumu na kumlaani, tujiulize, tumsaidieje?. Insane is a problem, Watanzania tujifunze kutafuta solutions to the problems sio kulaumu, kulaani, kushutumu na kulalamika tuu. Jee sisi kama Watanzania, tufanyeje kuwasaidia insane wetu?.

Tukio lolote la ajabu likitokea, simple minds wao wana discuss people, watalizungumzia kwa kuuliza nani kafanya nini, ordinary minds wao wana discuss event, tukio, limetokea wapi, limetokeaje tokeaje, limetokea vipi etc, lakini great minds, wao wata discuss ideas, ilikuwaje hadi tukio kama hili litokee, nini chanzo kilichopelekea tukio hilo kutokea?, what was the motive behind na the underlying facts and causative agents, zilizosababisha tukio hilo?.

Kila mtu mzima mwenye akili zake timamu, akifanya jambo la ajabu, watu wenye akili hawaanzi kulaani na kulaumu, bali huanza kwa kujiuliza, inawezekana vipi mtu mzima na akili zake timamu akafanya tukio kama lile, au kituko kama kile?, hivyo unafanya kitu kinaitwa a quick psychoanalysis assesment, ili kubaini chanzo.

Kulipotokea uvamizi wa studio za Clouds, mimi nilifanya a quick psychoanalysis assessment na mara moja tuu nikagundua kuna kila dalili za insanity. Mtu insane akifanya tukio la ajabu au kituko, sio jambo la kushangilia au kulipigia kelele, kushutumu kulaani na kulaumu, na kumsusia au kumtenga, bali ni jambo la kuhurumiwa, kusaidiwa na kutafutiwa tiba kwa sababu wakati akitenda kitendo kile, masikini wa watu hakujua atendalo!. Hata watu wote wanao commit suicide, by the time anaamua kujiua, anakuwa under insanity, akitokea mtu kumstua au kumgutusha, akili zinamrudia, hivyo msifanye masikhara kabisa na watu insane, huanza hivi hivi wasiposaidiwa, huishia kufanya mambo makubwa ya ajabu na mengine ya hatari!.

Kuna watu wengi katika hali ya kawaida kabisa, wanaonekana kama ni wazima na wako timamu kabisa, wala huwezi kuwadhania kuwa ni insane, lakini pindi insanity ikiwaingia, vituko wanavyofanya under insanity, ndivyo vinawatambulisha kuwa sio wazima bali ni vichaa!. Hii inaitwa kughafilika. Kuna wabakaji wengi haswa wale wabakaji wa next of kin, au vitoto vidogo, hawa wote ni vichaa kwa ukichaa wa kughafilika.

Kuwa kichaa sio lazima mpaka mtu aokote makopo au kula majajalani, lakini kuna ukichaa unaitwa "pseudo insanity" ambapo mtu ni mzima kabisa, anarukwa na akili kwa muda mfupi, anaghafilika, anafanya tukio, au kituko, kisha akili zinamrudia, anakuwa haamini kuwa ni yeye aliyefanya tukio hilo au kituko hicho!. Lakini wengi wa insane hawa, akili zikiisha warudia, kwanza watanyon'gonyea, kisha watatahayari, na mwisho hujuta na kuomba msamaha!.

The best thing to do kwa mwenye akili timamu, ni kujutia na kuomba msamaha!. Ukiona insane ametenda jambo la ajabu na hajutii, ujue huyo sii mzima, ni mtu anayehitaji msaada, its a temporary rightmove kwa media kumuepuka ili kumstahi asizidi kujiaibisha, yaani shun him out temporarily, lakini sio kumsusia habari zake, huku ni kuwasusia wananchi anaowatumikia. Hili la viongozi vichaa, nimelisema hapa
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa ...

Japo mimi sio mtaalamu wa hii psychoanalysis lakini nimepitia juu juu kwa kusoma maandishi ya Sigmund Freud na kusomea Jung Psychology, hivyo kuna vitu vya ajabu binadamu anavifanya ambavyo vinasabishwa na msongo wa mawazo ya mateso ya utotoni na kusababisha kitu kiitwacho "deep rooted neurosis" ya kumbukumbu ya maumivu na mateso ya utotoni, au kupigika kimaisha yaliyohifadhiwa kwenye subconscious mind, sasa ukijumlisha na "karma" affects za mapito ya maisha ya mtu aliyopitia, pressure za kazi, maisha, ndoa, utajiri wa ghafla, kupendwa sana na mfalme, bad media publicity, siri za kuiba jina na kufoji vyeti vya watu ambazo mwanzo zilikuwa ni well kept secrets, sasa ziko to an open,etc, etc, hivyo mtu hujikuta anapata depression, anafanya mambo ya ajabu ajabu, watu wanashangaa na kumlaumu, wengine kumlaani, bila kujua chanzo, kisababishi na the motive behind, laiti wangelijua, wangegundua ni mtu anayehitaji zaidi kuhurumiwa na kusaidiwa kuliko kulaumiwa, kulaaniwa, kushutumiwa na kususiwa!.

Kitendo alichokifanya mtu isane kuvamia Clouds Media lengo ni kumflict pain kwa mtu insane mwingine kutokana na maumivu aliomsababishia. Hii ni sadism, hufanywa na ma sadists. Kile kitendo cha kulia madhabahuni ni some form of pain release, ila kwa pain za deep rooted neurosis haziishi kwa kulia tuu au kumwaga chozi madhabahuni kwa kumlilia Mungu, bali mtu anakuwa kama mdudu nge, nge akichachamaa huinua mkia juu na ku sting, chochote anachokutana nacho, ndipo pain zinakuwa released kwa kuinflict pain kwa wengine, hivyo mtu mmoja alimtumia huyo mzazi na mtoto aliyetelekezwa ambaye nae ni insane, kuinflict pain kwa mtu insane mwingine, ili na yeye aumie kama yeye alivyoumia, hivyo yeye kupata gratification kwa maumivu yake ya ndani. Hili nimelizungumza kwenye
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta ...

Katika sakata hili, muathiika mkubwa kabisa ni yule mtoto an innocent victim anayelelewa na insane mother aliyetelekezwa ambaye ni an innocent victim!. Sijui kama mama yule alijua anatumika na alilipwa kiasi gani?!, ila kwa nguvu alioitumia kuvamia Clouds, wale vijana wa shilawadu, watakuwa nao walidakishwa mtonyo wa nguvu kwa ahadi ya kuitangaza habari hiyo ili kumkomoa fulani, na usikute hata kwa huyo mdada pia ni insane ndio aliwalengesha, ndio maana alikwenda pale kwa hasira with full force na makirikiri ili kufidia mtonyo wake, watu wavute mtonyo, waseme watatoa, halafu hawajatoa, hata ningekuwa mimi, ningekasirika!.

Kwa vile muathirika mkuu ni kale kachanga, kwanza kama ni kweli mchungaji ndie mhusika, then he has to be responsible kutoa matunzo kupitia ustawi wa jamii, na ikibidi kisheria kwa kuhusisha vipimo vya DNA.

Kwa sisi tuliopitia hiyo psychoanalysis, kwa kumsikiliza tuu huyo mwanamke, utagundua, she is insane!, mtu asiye na mahali pa kuishi, anayelala kanisani, can do anything with anyone, hivyo you never know ni watu wangapi wengine aliwahudumia!. The bottom line ni mtoto asaidiwe!. Mtu anaemtumia mtu mwingine insane ili kuinflict pain kwa adui yake, pia ni insane, anahitaji kusaidiwa, ila pia mtu anaemsupport huyo isane na kunyamazia vitendo vya insanity, nae need his head, seriously be examined!.

Tupo tuliolaani, tuliolaumu, tulioshutumu, tulio beza, lakini tunaweza kuwa tulifanya yote haya kwa kutojua kuwa tuna deal na a mental case ya insanity, baada ya kujua hili, Watanzania tuingiwe na huruma ya shauku ya kuhurumiana na kusaidiana, na mimi pia nitasaidia.

Insanity ziko za aina nyingi na levels tofauti, kati ya inanity zote, pseudo insanity ndio the hardest to detect kwa sababu ni kichaa cha muda tuu, kinapanda mtu anafanya tukio kisha kinayeyuka anakuwa normal kabisa and you can't tell. Ma sex maniacs na ma psychopaths wako kwenye kundi hili. Usually insane hajijui ila walio sane ndio wanaobaini mwenzao ni insane, sasa ikitokea mtu ni insane na kuna watu wanaviona hivyo vitendo vya insanity as just normal na kumpongeza, then they might be insane as well ila hawajijui.

Ziko pseudo insanity zinazosababishwa na alcohol intoxication hivyo kutenda vitu vya ajabu ukilewa, ukiwa sober, inajuta.

Kuna insanity ya groups psychology ambapo kundi la watu wanampiga mwizi wa kuku hadi kumuua kwa kumwagia mafuta na kumchoma akiwa hai, halafu watu hao hao wanashangilia mafisadi kama ya EPA kusamehewa!.

Pia kuna pseudo insanity ya daredevils kafanya jambo la hatari, likifanikiwa unaonekana shujaa likibumba unaonekana kichaa kama watu wanaohudhuria mikutano na maandamano yasiyo na vibali.

Kama katiba imetoa haki hizo na zile, na kuna taratibu, sheria na kanuni za kudeal na kila situation halafu mtu akaibuka na kwenda kinyume cha katiba au kutaja taja tuu majina ya watu na kuwatuhumu bila ushahidi, japo ni ushujaa lakini ni insanity.

Situations za matukio ya everyday events kwenye familia zetu nayo ni insanity. Mtu yoyote anayepiga mke wake, wanaume anayetelekeza família, mwanamke anayetelekeza kichanga chake, ulevi wa kupindukia, wizi na udokozi, tabia za u play boy. Wadada wanaojiuza, umbeya, ufukunyuku, kupiga chabo, etc etc vyote hivi ni insanity.

Hata mimi binafsi nikitumia usafiri wa boda boda kwa sababu unafika haraka kuliko gari, nilipoutumia kwenda rough and very fast, sikujua nilikuwa under insanity hadi yaliponikuta ya kunikuta, hivyo hata hili bandiko linaweza kuwa ni la insanity, only the sane ones ndio watatambua na insane wenzangu na mimi hatuwezi kutambua. Insane huwezi kumrekebisha insane mwenzake, hivyo naomba ukiliona hili bandiko ni too offensive, unaweza kuwa wewe ndio uko sane, liripoti kwa mode lifungwe.

Namalizia kwa kusisitiza, mtu insane anahitaji kuonewa huruma, kusaidiwa, kufarijiwa na sio kulaumiwa, kulaaniwa kulaumiwa, kususiwa na kutengwa!, this man needs help seriously, Jee tumsaidieje?. Naombeni tushirikiane kutoa mawazo positive jinsi ya kuwasaidia insane hawa, tufanyeje?!.

N.B tunaomba mawazo na ushauri tuu, please hakuna kutaja majina!, hatuzungumzi watu hapa tunazungumza ideas.

Jumatano Njema
Paskali
Update 1. Iwapo tatizo la insanity litamtokea mkuu wa nchi, katiba yetu imeweka utaratibu ufuatao kushughulikia tatizo hili endapo litatokea.

Update 2: Huu ni ushauri wa kidakitari wa jinsi ya kusaidia

Mkuu Magafu, asante sana kwa bandiko hili ambalo ndio msaada mkubwa wa kwanza very objective katika kumsaidia huyu kijana mwenzetu.
Wengine tuendelee kuchangia objectively kwa lengo la kusaidia.

Paskali
Ni ugonjwa ambao unaweza kurithiwa?
 
Ni ugonjwa ambao unaweza kurithiwa?
Yes insanity ni heredity, yaani kuna kichaa cha ukoo na wazimu wa ukoo, na kuna kichaa cha ugonjwa, kama ugonjwa mwingine wowote. Ndio maana kabla hujaoa ukoo fulani, unafanya a due diligence report kuujua ukoo huo kama una magonjwa ya kuambukiza ya kiukoo, sisi Usukumani, hadi wanapima virility!.
P
 
Back
Top Bottom