FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 2,022
- 4,127
- Thread starter
- #41
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 11
SONGA NAYO............
Mjira ya saa 2 za usiku tax ilikuwa inapaki maeneo ya Mbagala kwa Zizi Ally, alishuka Jason na kulipia pesa kwa huyo dereva na kumshukuru kwa kumfikisha salama, hakusahau kumshukuru mwenyezi MUNGU kwa kuweza kumfikisha salama ndani ya hilo eneo, aliitoa simu yake na kuangalia kwa umakini aliangalia namba ya nyumba ambayo alikuwa ameelekezwa akatingisha kichwa kuonyesha kwamba alikuwa anakubaliana na hicho kitu. Mbele yake apalikuwa na uwanja mkubwa wa uwazi ambao kuna watu wengi sana walikuwa wanacheza Baikoko hawana hata muda, wadada walikuwa wamevaa kanga moja moja tu huku wanamwagiwa maji halafu wanaendelea kuonyesha kile walicho pewa na mama zao, ilikuwa ni full kukata viuno huki vijana kibao wakiwa wanawashika shika wanawake hao kama namna ya kufurahi wala hao wanawake hawakuwa wakileta ubishi wowote.
“Hey mama shura ana laana, anavyolikata utasema hana mwana”
“Mimi ni nani mpaka nibishe bwana, siwezi kula mifupa na naiona nyama”
Ni sauti moja ya kijana ambaye alikuwa anawaimbisha wanawake hao na walikuwa wanakata viuno kwa kumfuatisha yeye hali iliyo pelekea hali ya sehemu za mbele za vipensi kutuna sana kwa hisia ambazo walikuwa wanazipata kutokana na kuyashuhudia maungo ya ndani ya wanawake hao. Jason alibaki anashangaa tu baada ya kuona hiyo hali hakuwahi kuyaishi maisha kama hayo hata wakati akiwa ni mdogo aliishi maisha ya kawaida sana ila hakuwahi kukutana na vitu kama hivyo.
“Kaka kwa usiku mmoja ninunulie chipsi tu nakupa kila unacho kihitaji hata ukitaka kuruka kiunzi ni wewe tu handsome boy” akiwa ameduwaa na hali ya hapo alishtuka kuna mwanamke anamshika shika, kutokana na mavazi yake na sura yake yenye mvuto ulio kithiri vilifanya yeye awe tofauti hilo eneo hivyo dada huyo ambaye kwa mwonekano alikuwa ni mzuri sana ni kwa vile tu alikosa matunzo mazuri ndiyo maana hakuwa katika mwonekano nadhifu sana, Jason alishangaa mwanamke kama huyo alitakiwa kuwa shule kama sio ofisini kufanya kazi basi hata awe kwake akiwa na familia yake cha ajabu alihitaji kutoa mapenzi tena akisema kwamba yupo tayari kutoa sehemu zote mbili kama mwanaume huyo angetaka kikubwa tu amnunulie chipsi, hakuelewa kama ni njaa ndiyo ilikuwa tatizo kwa mwanamke huyo au ni mambo ya uswahilini ambayo yeye hakuyazoea kabisa.
Basi alimvuta mpaka pembeni kidogo na hilo eneo
“Unaitwa nani?”
“Nayra”
“Huku ndiyo nyumbani?”
“Ndiyo ni nyumba kumi tu kutoka hapa unafika nyumbani”
“Una miaka mingapi?”
“24”
“Una elimu gani?”
“Nimemaliza chuo mwaka jana”
“Sasa mwanamke msomi kama wewe kwanini unajidhalilisha namna hiyo kuhitaji kulala na mwanaume kisa chipsi? Au kuna tatizo” swali hilo lilimfanya mwanamke huyo aanze kulia, mwanaume alihisi huenda lazima kutakuwa na tatizo sio bure.
“Ok una simu?” mwanaume aliuliza baada ya kuona mwanamke huyo anaendelea kulia
“Hapana” Jason alijiuliza mara mbili mbili kisha akazamisha mkono wake mfukoni, alitoa simu moja ambayo haikutumika sana na ilikuwa simu ya bei ghali mno
“Samahani sana nimetembea na simu mbili tu hapa na hii nimeitumia kidogo lakini inaweza kukufaa, tumia hii simu siku ukipata muda naomba unipigie” aliongea baada ya kuandika namba yake kwenye kioo huku akiwa anamkabidhi hiyo simu mrembo huyo ambaye alikuwa na vigezo vya mwanamke mzuri sana ila huenda ni matatizo ambayo alikuwa anayapitia maisha magumu ndiyo yalimfanya kuwa wa kawaida ila licha la kuvaa dera lililo choka ndani ya hilo dera lilikuwa likitikisika sana kuonekana lilibeba mali ambayo ilienda shule haswa. Binti huyo alipiga magoti huku akiwa analia na kumshukuru sana Jason na alishukuru mno MUNGU kumletea mtu huyo kwa wakati huo kwani hali ilikuwa si hali, mwanaume alimnyanyua na kumsimamisha.
“Usipende kuwapigia pigia magoti wanadamu wenzako hiyo ni ishara moja mbaya sana unaweza ukaishia kutumika sana, nimekuja huku namtafuta afisa mmoja wa polisi ambaye anaitwa Bakari Zalimo sijui kama utakuwa unamfahamu na unapajua kwake?” swali lake liliitikiwa na dada huyo kwa kutingisha kichwa chake kuonyesha kukubali hicho kitu basi mwanaume alimuomba dada huyo ampeleke huko hakuwa na hiyana alitangulia mbele na mwanaume akawa anafuata nyuma huku akishuhudia mitetemo ambayo ilikuwa ndani ya dera, mawazo yake hayakuwa kabisa hapo lakini alijikuta anasikitika tu kwa binti mzuri kama huyo kuhitaji kuutoa mwili wake kisa chipsi.
“Una muda gani unaishi huku?”
“Nimezaliwa huku ila nilikuwa naondoka tu wakati wa Kwenda kusoma na nikimaliza au likizo nilikuwa narudi huku huku”
“Huyu askari unamjuaje?”
“Huyu ni mtu maarufu sana huku hata ukimuita mtoto mdogo anakupeleka” wakiwa wanaendelea na maongezi hayo huku wakiendelea kutembea aneo ambalo halikuwa na uwazi mkubwa sana walisikia Kigoma kikipigwa hiki kilikuwa tofauti na kule ambako walikuwa wanacheza Baikoko walisikia sauti kali ya kijana ambaye alikuwa ana furaha sana.
“Nai naona umeokota dodo kwenye mpera umemtoa wapi leo mtu wa Masaki huyo?” hali hiyo ilimfanya Nayra acheke sana huku akimnyooshea mkono kijana huyo kumpa hai wala hakumjibu na ndo ilikuwa mara ya kwanza Jason analiona tabasamu la binti huyo alijikuta naye anatabsamu, kulikuwa na kiza sana lakini mwanga wa taa za nyumba ulimfanya aone vyema namna mashavu ya Nayra yalivyokuwa yanabonyea pale anapokuwa anacheka.
“Usimjali yule ni vijana wa mtaani hapa huwa wanapenda kunitania sana”
“Wala usijali ni vizuri sana kama unaishi na watu kwa upendo sana namna hii” waliendelea na maongezi wakati huo walikuwa wanakunja kona moja na Nayra akasimama baada ya kutembea hatua kama kumi, alijongea kidogo na kugonga geti moja jeusi hapo kwa nguvu
“Ndiyo hapa tumefika” alivyo maliza tu kuongea geti lilifunguliwa na alikuja kufungua mwanaume mmoja ambaye alikuwa ndani ya vest nyeupe
“Bila shaka wewe ndiye ASP Bakari” Jason aliuliza
“Ndiyo nikusaidie nini?” ASP aliuliza huku akiwa anamwangalia Nayra ambaye aliishia kumsalimia
“Shikamoo”
“Marhaba Nayra asante kwa kuniletea mgeni” Jason hakuhitaji kusubiri sana aliingiza mkono kwenye mfuko wake akatoa kibunda cha pesa na kumkabidhi binti huyo pesa zote ambazo zilimfanya abaki kama amepigwa na butwaa, ikabidi Jason amshtue
“Ukipata tatizo lolote nitafute kwa simu kama ukishindwa basi uje hapa umtafute huyu ASP atakukutanisha na mimi" maneno hayo yalimfanya binti huyo aanze kulia tena, hapo siyo maneno ambayo yalikuwa yanamliza bali ni hizo pesa ambazo yeye alipewa, ASP Bakari Zalimo alimuonyesha ishara binti huyo aende kisha yeye alimkaribisha mgeni ndani huku Jason akiishia kusikitika tu.
“Sijui nikusaidie nini?” ASP aliuliza wakati wamekaa kwenye kibaraza ambapo palikuwa na hewa safi sana
“Mbona ASP mzima unaishi maisha ya hovyo kama haya na una kazi nzuri tu shida nini mpaka umekuja kujichimbia maeneo kama haya?” swali la Jason lilimfanya ASP Bakari amshangae sana wakati huo yeye alikuwa anaendelea kuangaza maeneo ya hiyo nyumba
“Nadhani ni vyema zaidi kama ukijitambulisha kwanza wewe ni nani?”
“Ooooooh kichwa kina mambo mengi sana, mimi ni mdogo wake na jaji mkuu Markvelous Japhary ambaye ameuawa siku ya jana nadhani una hizo taarifa?”
“Yes, taarifa ninazo lakini kusema wewe ndiye mdogo wake na jaji mkuu sina hizo taarifa nasikia tu ana mdogo wake ila simjui hivyo sio rahisi sana kukuamini ndugu yangu nadhani kama ni shida ya kiofiosi inabidi usubiri mpaka kesho tukutane ofisini”
“Unavyo ongea kiwepesi hivyo unatakiwa kujua kwamba huko niliko toka nimepoteza muda wangu mpaka kufika eneo la mbali kama huku, mimi sio mjinga kuja kukufuata wewe huku kama sina ishu za mhimu mpaka uniambie kwamba nije ofisini kwani mimi sijui kama kuna ofisi? Hapa nimeelekezwa na IGP ndiyo maana sijahangaika sana kuweza kufika” aliongea huku akitoa picha ambayo alikuwa na kaka yake pamoja na familia yake na kumpatia Asp Bakari Zalimo ambaye aliishia kuitazama kwa umakini sana.
“Hiyo ni familia yangu ya pekee na ndiyo ambayo nilikuwa nimebakiwa nayo kwenye maisha yangu lakini nayo bila huruma imepotezwa na watu ambao sijui walikuwa na lengo gani, IGP amenielekeza kwamba wewe ndiye mtu ambaye ulikuwa wa kwanza Kwenda pale na team yako baada ya tukio kutokea sasa nahitaji unipe ABC ya kila kilicho tokea pale lakini kabla ya hilo naomba taarifa za huyo binti ambaye amenileta hapa” Asp alimtazama sana Jason alikuwa anaongea naye kiwepesi mno alielewa ni dharau za watu ambao ndugu zao ni watu wenye vyeo vikubwa au wenye maisha mazuri sana, aliitoa simu yake na kumpigia IGP ili athibitishe kama ni kweli huyo mtu alikuja kupitia yeye kwa sababu taarifa ambazo alikuwa anazihitaji zilikuwa ni nyeti sana ingekuwa ni mbaya na hatari kama angejichanganya kumpatia mtu ambaye alikuwa hahusiki kabisa na taarifa hizo.
“Msikilize na umpatie kila anacho kihitaji” ilikuwa ni sauti nzito ambayo ilisikika upande wa pili baada tu ya kuipokea simu hiyo na kisha simu ikakatwa kabla yeye mpigaji hajajibu chochote kile ni wazi IGP baada ya kupigiwa simu na huyo kijana wake alijua kwamba lazima alikuwa amekutana na Jason ndiyo maana hakuhitaji mambo mengi sana, Jason hakuwa na shaka alimsubiria mtu huyo amalize kutuliza huo wasi wasi wake huku akiwa makini sana kuiangalia saa yake ya mkononi, Asp alihema kwa nguvu sana na kuufungua mdomo wake.
“Kwanza nianze kwa kusema pole sana ndugu yangu kwa yote ambayo yamekupata najua ni ngumu sana kuyavumilia lakini siku zote wanaume tumezaliwa ili kuzivaa changamoto na hauna namna zaidi ya kukabiliana nazo ndiyo njia pekee ya kuzitatua. Kuhusu huyo binti ni binti mmoja ambaye ni mstaarabu sana japo sina taarifa zake nyingi sana maana anajulikana sana hii mitaa kwa ucheshi wake na adabu zake lakini ni binti ambaye anatokea kwenye familia yenye maisha magumu sana kwa kinacho daiwa kwamba baba yake mzazi huruma zake za kuhitaji kusaidia saidia sana ndugu zake zilimponza wakaishia kumtapeli mali zote alizokuwa nazo hali hiyo ilipelekea yeye kuugua ukichaa na hicho kilipelekea hata mkewe kupata matatizo ya moyo na presha zisizo isha na binti ndiye mkubwa kwao hivyo yeye ndiye anaye tegemewa na wazazi wake wote wawili pamoja na wadogo zake. Alifanikiwa kumaliza elimu ya chuo lakini nasikia kwenye kupata kazi ameshindwa kupata kwa sababu wanaume wengi huwa wanamuomba mwili wake ili wampee kazi ila hajawahi kuruhusu hicho kitu kwa sababu ni binti ambaye amelelewa kwenye maadili bora sana kwa taarifa ambazo ninazo” maelezo ya Asp yalimuacha Jason njia panda kwa sababu huyo binti sio muda ametoka kumuomba chipsi tu ili alale naye sasa kivipi akubali kutoa mwili kwa chipsi halafu akatae kutoa mwili ili apate kazi, alihisi huenda kuna tatizo kubwa sana nyuma ya huyo binti ambalo anapitia, aliamua kuiweka hiyo kiporo ili alifuatilie kwa umakini.
Asp alijikohoza kidogo ili kumpa ABC ya tukio ambalo yeye ndiye alikuwa askari kwa kwanza kufika akiwa na vijana wake baada ya mheshimiwa jaji mkuu wa Tanzania Markvelous Japhary kuweza kuuawa.
11 naweka nukta hapa tukutane sehemu ya 12.
Bux the storyteller.