SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 8,504
- 13,812
Mara nyingi utasikia watu wanasema "mpira una lugha yake" ila wanachoshindwa kutambua ni kuwa kushindwa kuelewa lugha fulani kunaweza kukupunguzia uwezo wa kuelewa maelekezo kwa haraka na ufasaha na pia kukupunguzia confidence.
Nikiangalia wachezaji wa Simba kama Karabaka, Mashaka, Balua, Chasambi unaona kuwa kutopewa game time ya kutosha na wengine hata kutolewa kwa mkopo kunaweza kuwa kunachangiwa kiasi fulani na kwamba Fadlu Davids na benchi lake wanapata wakati mgumu kuwafundisha na kuzungumza nao ndani na nje ya uwanja.
Watanzania wengi ambao lugha ya kiingereza siyo rafiki sana, wakiwa kwenye mazingira ambayo lugha hiyo ndiyo inatumika zaidi tuna mtindo wa kuwa wanyonge, kujifichaficha na kujitenga tukiogopa "kudhalilika".
Ukifanya hivyo, kocha akasoma "body language" yako kuwa haujiamini, uwezekano wa yeye naye kutokuwa karibu na wewe unaongezeka. Hauwezi hata kupiga naye story mbili tatu mkiwa mnapiga msosi, badala yake muda wote utakaa na washkaji zako mzungumze kimatumbi. Tunashangaa kwa nini Mutale bado anapewa nafasi, hatutambui kwamba lugha inamuwezesha kuchati na mwalimu nje ya uwanja na kujenga ukaribu na ukizingatia ni mtu anayeonekana ni mtu wa matani. Hivi vitu vyote vinachangia katika maisha. Katika maisha, tunashuhudia mara kwa mara watu ambao wanaonekana hawana uwezo wanapewa fursa na wenye uwezo wanaachwa, "social skills" kama hizi zinachangia.
Valentino Mashaka anaweza kuwa msaada sana kwa Simba kipindi hiki ambapo Ateba ameonekana kushuka kiwango kwa kasi. Nawashauri Simba waiombe TFF wamruhusu Mashaka arudi ajiunge na Simba hadi mwishoni mwa msimu kama chaguo la pili baada ya Mukwala.
Edwin Balua angepewa game time ya kutosha angeweza kuwa na ufanisi na mchango sawa au kumzidi hata Ahoua na pia anamzidi mara 100 Ahoua kwenye upigaji wa faulo. Natambua hawa wawili hawachezi nafasi moja ila mapungufu yao ya uchoyo wameonyesha wote wanayo ila Ahoua ameonekana kuvumilika zaidi. Najua Ahoua naye kiingereza hakipandi ila nadhani confidence yake ni kubwa zaidi nje ya uwanja.
Siondoi uwezekano wa upendeleo usiohusiana na suala la lugha ila hilo nalo ni la kuzingatia.
Leo hii watu wanajadili kumuondolea Zimbwe unahodha wake na unakuta sababu kuu ni kushindwa kwake kutimiza majukumu yake ipasavyo kwa sababu ya changamoto ya lugha. Wanasema asilimia kubwa ya mawasiliano ya binadamu ni "body language", hata anapomfuata mwamuzi unaona kabisa hajiamini. Anaenda kinyonge sana.
Wachezaji wa kitanzania, jipigeni msasa, pesa ya kupata walimu wa lugha mnazo, msikae kizembe hadi mnachukuliwa poa. Thamani yenu itaongezeka mara dufu ndani na nje ya nchi mkijiongeza kwenye hili. Ni ushauri tu wa kujenga.
Pia nimewatumia wachezaji hao wa Simba kama mifano, hii inaweza kutumika kwa mchezaji au timu yoyote ile.