Inawezekana lugha inachangia kwa makocha wa kigeni kuwapendelea zaidi wachezaji wa kigeni

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
8,504
13,809
Mara nyingi utasikia watu wanasema "mpira una lugha yake" ila wanachoshindwa kutambua ni kuwa kushindwa kuelewa lugha fulani kunaweza kukupunguzia uwezo wa kuelewa maelekezo kwa haraka na ufasaha na pia kukupunguzia confidence.

Nikiangalia wachezaji wa Simba kama Karabaka, Mashaka, Balua, Chasambi unaona kuwa kutopewa game time ya kutosha na wengine hata kutolewa kwa mkopo kunaweza kuwa kunachangiwa kiasi fulani na kwamba Fadlu Davids na benchi lake wanapata wakati mgumu kuwafundisha na kuzungumza nao ndani na nje ya uwanja.

Watanzania wengi ambao lugha ya kiingereza siyo rafiki sana, wakiwa kwenye mazingira ambayo lugha hiyo ndiyo inatumika zaidi tuna mtindo wa kuwa wanyonge, kujifichaficha na kujitenga tukiogopa "kudhalilika".

Ukifanya hivyo, kocha akasoma "body language" yako kuwa haujiamini, uwezekano wa yeye naye kutokuwa karibu na wewe unaongezeka. Hauwezi hata kupiga naye story mbili tatu mkiwa mnapiga msosi, badala yake muda wote utakaa na washkaji zako mzungumze kimatumbi. Tunashangaa kwa nini Mutale bado anapewa nafasi, hatutambui kwamba lugha inamuwezesha kuchati na mwalimu nje ya uwanja na kujenga ukaribu na ukizingatia ni mtu anayeonekana ni mtu wa matani. Hivi vitu vyote vinachangia katika maisha. Katika maisha, tunashuhudia mara kwa mara watu ambao wanaonekana hawana uwezo wanapewa fursa na wenye uwezo wanaachwa, "social skills" kama hizi zinachangia.

Valentino Mashaka anaweza kuwa msaada sana kwa Simba kipindi hiki ambapo Ateba ameonekana kushuka kiwango kwa kasi. Nawashauri Simba waiombe TFF wamruhusu Mashaka arudi ajiunge na Simba hadi mwishoni mwa msimu kama chaguo la pili baada ya Mukwala.

Edwin Balua angepewa game time ya kutosha angeweza kuwa na ufanisi na mchango sawa au kumzidi hata Ahoua na pia anamzidi mara 100 Ahoua kwenye upigaji wa faulo. Natambua hawa wawili hawachezi nafasi moja ila mapungufu yao ya uchoyo wameonyesha wote wanayo ila Ahoua ameonekana kuvumilika zaidi. Najua Ahoua naye kiingereza hakipandi ila nadhani confidence yake ni kubwa zaidi nje ya uwanja.

Siondoi uwezekano wa upendeleo usiohusiana na suala la lugha ila hilo nalo ni la kuzingatia.

Leo hii watu wanajadili kumuondolea Zimbwe unahodha wake na unakuta sababu kuu ni kushindwa kwake kutimiza majukumu yake ipasavyo kwa sababu ya changamoto ya lugha. Wanasema asilimia kubwa ya mawasiliano ya binadamu ni "body language", hata anapomfuata mwamuzi unaona kabisa hajiamini. Anaenda kinyonge sana.

Wachezaji wa kitanzania, jipigeni msasa, pesa ya kupata walimu wa lugha mnazo, msikae kizembe hadi mnachukuliwa poa. Thamani yenu itaongezeka mara dufu ndani na nje ya nchi mkijiongeza kwenye hili. Ni ushauri tu wa kujenga.

Pia nimewatumia wachezaji hao wa Simba kama mifano, hii inaweza kutumika kwa mchezaji au timu yoyote ile.
 
Mweeee....a good coach always adapts to an excellent player. Ukiona kocha abadiliki ili aku accomodate kwenye mfumo wake hiyo ni ishara u no an excellent player u r just average
 
Mara nyingi utasikia watu wanasema "mpira una lugha yake" ila wanachoshindwa kutambua ni kuwa kushindwa kuelewa lugha fulani kunaweza kukupunguzia uwezo wa kuelewa maelekezo kwa haraka na ufasaha na pia kukupunguzia confidence.

Nikiangalia wachezaji wa Simba kama Karabaka, Mashaka, Balua, Chasambi unaona kuwa kutopewa game time ya kutosha na wengine hata kutolewa kwa mkopo kunaweza kuwa kunachangiwa kiasi fulani na kwamba Fadlu Davids na benchi lake wanapata wakati mgumu kuwafundisha na kuzungumza nao ndani na nje ya uwanja.

Watanzania wengi ambao lugha ya kiingereza siyo rafiki sana, wakiwa kwenye mazingira ambayo lugha hiyo ndiyo inatumika zaidi tuna mtindo wa kuwa wanyonge, kujifichaficha na kujitenga tukiogopa "kudhalilika".

Ukifanya hivyo, kocha akasoma "body language" yako kuwa haujiamini, uwezekano wa yeye naye kutokuwa karibu na wewe unaongezeka. Hauwezi hata kupiga naye story mbili tatu mkiwa mnapiga msosi. Tunashangaa kwa nini Mutale bado anapewa nafasi, hatutambui kwamba lugha inamuwezesha kuchati na mwalimu nje ya uwanja na kujenga ukaribu na ukizingatia ni mtu anayeonekana ni mtu wa matani. Hivi vitu vyote vinachangia katika maisha. Katika maisha, wanashuhudia mara kwa mara watu ambao wanaonekana hawana uwezo wanapewa fursa na wenye uwezo wanaachwa, "social skills" kama hizi zinachangia.

Valentino Mashaka anaweza kuwa msaada sana kwa Simba kipindi hiki ambapo Ateba ameonekana kushuka kiwango kwa kasi. Nawashauri Simba waiombe TFF wamruhusu Mashaka arudi ajiunge na Simba hadi mwishoni mwa msimu kama chaguo la pili baada ya Mukwala.

Edwin Balua angepewa game time ya kutosha angeweza kuwa na ufanisi na mchango sawa au kumzidi hata Ahoua na pia anamzidi mara 100 Ahoua kwenye upigaji wa faulo. Natambua hawa wawili hawachezi nafasi moja ila mapungufu yao ya uchoyo wameonyesha wote wanayo ila Ahoua ameonekana kuvumilika zaidi. Najua Ahoua naye kiingereza hakipandi ila nadhani confidence yake ni kubwa zaidi nje ya uwanja.

Siondoi uwezekano wa upendeleo usiohusiana na suala la lugha ila hilo nalo ni la kuzingatia.

Leo hii watu wanajadili kumuondolea Zimbwe unahodha wake na unakuta sababu kuu ni kushindwa kwake kutimiza majukumu yake ipasavyo kwa sababu ya changamoto ya lugha. Wanasema asilimia kubwa ya mawasiliano ya binadamu ni "body language", hata anapomfuata mwamuzi unaona kabisa hajiamini. Anaenda kinyonge sana.

Wachezaji wa kitanzania, jipigeni msasa, pesa ya kupata walimu wa lugha mnazo, msikae kizembe hadi mnachukuliwa poa. Thamani yenu itaongezeka mara dufu ndani na nje ya nchi mkijiongeza kwenye hili. Ni ushauri tu wa kujenga.

Pia nimewatumia wachezaji hao wa Simba kama mifano, hii inaweza kutumika kwa mchezaji au timu yoyote ile.
Mpira ni mchezo wa hadharani haiitajiki LUGHA kibu kufanya kile anacho kifanya uwanjani..
 
Mweeee....a good coach always adapts to an excellent player. Ukiona kocha abadiliki ili aku accomodate kwenye mfumo wake hiyo ni ishara u no an excellent player u r just average
Ni mpaka sasa uwe "excellent" ila kama bado unajitafuta halafu una ushindani wa namba, kocha ataangalia pale palipo na unafuu kwake kutoa maelekezo na yule anayechangamana naye kwa urahisi zaidi nje ya uwanja. Ni wazi Mutale anajichanganya na kila mtu ndani ya timu zaidi ya Balua na Chasambi. Haya mambo yanachangia sana.
 
Sidhani sana!, ila wachezaji nao wasisite kujitoa kimasomaso kama lugha ni sakata basi watumie mishahara yao kujipiga msasa uzuri walimu wapo!, si lazima sana kujua ile deeply!.
sema huwa kunakuwa tu na ile saikolojia ya uoga na sisi wenyewe tu ndo tumeijenga!. ila haohao wazungu wapo wengi tu English inawakung'uta mwengine anakuambia kabisa no English!.. sasa hapo ni mwendo wa ishara lkn mtaelewana tu!..😂
 
Ndiyo ninachosema, kwamba kama tusingejenga huo unyonge na woga kutokana na kutojua lugha mbona isingekuwa tatizo.

Kwa hiyo ni rahisi na haraka zaidi kukabiliana na hili suala kwa kujifunza lugha kuliko kusema uondoe woga bila kujua lugha wakati ni suala la kisaikolojia na lipo ndani yetu.
 
Ni ngumu Sana kujifunza lugha mpya ukiwa above 18yrs.. kichwani huwaga Kuna LANGUAGE ACQUIRING DEVICE INAFUNGAGA ukifikisha above 18yrs ndio maana watoto wanajifunza kwa haraka LUGHA MPYA KULIKO MTU MZIMA

Huwezi kua mbobevu kwenye hiyo lugha..
 
Mbona mbwana Samantha aliweza kumudu yoteee na kuja kua CHAMPION wa soka la BONGO
 
Inategemea na ubongo wa mtu watu wote hatupo sawa!.
 
Mbona mbwana Samantha aliweza kumudu yoteee na kuja kua CHAMPION wa soka la BONGO
Mkuu, mbona unaleta ubishi na kushindwa kuelewa kitu simple kama hiki. Kama alivyosema mwenzangu hapo juu ukiwa "excellent" au "exception" ni lazima mwalimu atatengeneza mazingira ya kukutumia ila kama bado unajitafuta huku una ushindani wa namba, ukichangia na kutojiamini, usishangae mwalimu kukuweka pembeni.

Samatta anajulikana hata nidhamu na juhudi zake za mazoezi zilikuwa za juu sana toka yupo Mbagala huko. Alikuwa anafika mazoezini kabla ya mtu yoyote. Hizo ni factors zinazotosha kumtenganisha na average players waliokuwa wanashindana naye. Pia sina uhakika wa ufahamu wake wa lugha alipokwenda DRC na baadae Ubelgiji ila kwa nidhamu yake sitashangaa kama alifanya juhudi binafsi za kujifunza.
 
Mkuu, mbona unaleta ubishi na kushindwa kuelewa kitu simple kama hiki. Kama alivyosema mwenzangu hapo juu ukiwa "excellent" au "exception" ni lazima mwalimu atatengeneza mazingira ya kukutumia ila kama bado unajitafuta huku una ushindani wa namba, ukichangia na kutojiamini, usishangae mwalimu kukuweka pembeni.

Samatta anajulikana hata nidhamu na juhudi zake za mazoezi zilikuwa za juu sana toka yupo Mbagala huko. Alikuwa anafika mazoezini kabla ya mtu yoyote. Hizo ni factors zinazotosha kumtenganisha na average players waliokuwa wanashindana naye.
Hii mada ni Pana Sanaa pia watu wanapishana kwenye vitu vingi hata lugha ya mpira uliyo ieleza ni tofauti kidogo na lugha yakuzungumza kiingereza kingi.

Pia hata hizi timu zimeajili watu wa kutafsiri lugha so Kuna kua na MEDIUM.. pia kwa Sasa wachezaji wengi at least wengi angalau Wana elimu ya form four.
 
Back
Top Bottom