Dar: Inasemekana tukio hili la utekaji limetokea Kiluvya, kutokana na uzito wa jamaa walishindwa kumchukua. Hakuna aliyetoka kumsaidia

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,137
3,212

Wakuu,​


Nimekutana na video hii duniani huko, pamoja na kujaribu kupiga kelele watu waliuchuna. Angalu video hii imepatikana, kama ni tukio la kweli wasiyojulikana wataanza kujulikana.

=====

Screenshot_20241112_234419_Instagram.jpg


IMG_20241112_224611_737.jpg
Kumbusho Dawson kaandika haya kupitia ukurasa wake akisindikiza video hiyo;

"Tukio hili la utekaji limetokea jana Rovvenpec Resort, Kiluvya madukani, kutokana na nguvu za mwamba aliwashinda watekaji.
"Inasikitisha Sana kwamba hakuna pamoja Na kwamba kulikuwa na watu wanashuhudia hakuna mtu aliejitokeza kutoa msaada inasikitisha.

Pia soma: Kupambana na watu wasiojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi

"Mstari unaotofautisha akili za nyumbu na Watanzania ni ndogo kama punje ya haradali. Mtu anakamatwa watu wanashangàa kama kundi la nyumbu porini. Shame be upon you."

Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Yawezekana kabisa kutokana na dhana kwamba usanii walipa pengine watu walidhani wasaniii walikuwa kazini.

Kumbe kiuhalisia mtu atekwa hadharani. Pia kuna jamaa hapo kapita tu bila hata kuangalia kinoendelea.

Mzee Ali Kibao (RIP)alitekwa kutoka kwenye basi na abiria wengine wakiwa hawana cha kufanya na kwenda kuteswa kisha kuuawa.
 
Mungu Kampa Mwili Wake Mkubwa Kama Kinga Ya Kuuliwa Na Wapumbavu kama hawa na Bado Watanzania Tunawacheki tu.

Nchi gani hii

Na Ajabu Utasikia Kimya

Hawajulikani

Na Kunakauli ya mwisho hapo Tutakupata/ Tutakufuata hawa Tunaomba Majina yao Yasambae tujue hawa ndio Wauwaji
 
hao watekaji wanaonekana kabisa. ndio maana marekani trump alisema kila mtu amiliki silaha, ila kama zinapigwa muwe kwenye level sawa.

Hao wanaringa kwa sababu wana silaha, ila wangejua jamaa naye ana silaha wasingemuonea hivyo. nchi imefika pabaya sana.
 

Wakuu,​


Nimekutana na video hii duniani huko, pamoja na kujaribu kupiga kelele watu waliuchuna. Angalu video hii imepatikana, kama ni tukio la kweli wasiyojulikana wataanza kujulikana.

=====

View attachment 3150653

Kumbusho Dawson kaandika haya kupitia ukurasa wake akisindikiza video hiyo;​


"Tukio hili la utekaji limetokea jana Rovvenpec Resort, Kiluvya madukani, kutokana na nguvu za mwamba aliwashinda watekaji.​

"Inasikitisha Sana kwamba hakuna pamoja Na kwamba kulikuwa na watu wanashuhudia hakuna mtu aliejitokeza kutoa msaada inasikitisha.​


Pia soma: Kupambana na watu wasiojulikana: Ukija kukamatwa na polisi bila uniform na hajaambatana na kiongozi wa eneo husika piga firimbi, kusanya nzi

"Mstari unaotofautisha akili za nyumbu na Watanzania ni ndogo kama punje ya haradali. Mtu anakamatwa watu wanashangàa kama kundi la nyumbu porini. Shame be upon you."​


Kupata matukio ya nyuma kuhusu watu wasiyojulikana ingia hapa: Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
Nimpe pole jamaa kunasuka hapo, maana wange mu RIP, pili inasikitisha sana wabongo hawasaidii wanamuangalia mtu akiwa matatizoni, baadae watume RIP

Aisee jamii inahitaji revolution , hii ni zaidi ya ukondoo
 
Back
Top Bottom