Bila shaka ni kwa maana ya uigizaji wa kuburudisha watazamaji!Wanaigiza ili kitokee nini?
Taratibu, tutaanza kuzoea mambo haya ya utekaji na kuyachukulia kama burudani.
Hii inanikumbusha mambo ya kivita siku hizi.
Wakati ule Iraq ikishambuliwa (Desert Storm), watu baada ya kurudi majumbani kwao toka maofisiini waliwahi nyumbani kutazama jinsi Bagdad ilivyo kuwa ikichakazwa kwa mabomu. Vimulimuli ikawa ni burudani kwenye television; lakini upotevu wa maisha uliokuwa ukiambatana na burudani hiyo halikuwasumbua watazamaji hao!
Hali sasa imekuwa ni hivyo hivyo, hata hapo Gaza, au Irani anapo rushiwa, au na yeye anapo mrushia Israel. Washangiliaji na mashabiki kama wa Yanga na Simba hujigamba jinsi timu yao ilivyo wachakaza wenzao!
Hayo ndiyo maisha sasa, nasi taratibu tunaingia taratibu kwenye mangilio huo.