Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 4,122
- 7,392
Shirika la Fedha Duniani (IMF) limetangaza kuwa limefikia makubaliano ya awali na serikali ya Tanzania ambayo yakipitishwa rasmi, yataiwezesha nchi hiyo kupata takriban dola milioni 441 kwa ajili ya kusaidia uchumi wake.
Fedha hizi ni sehemu ya mapitio ya tano ya mpango wa mikopo ya muda mrefu (ECF) na mapitio ya pili ya mpango wa Uhimilivu na Ustahimilivu (RSF).
Makubaliano haya yamefikiwa baada ya timu ya IMF ikiongozwa na Nicolas Blancher, kufanya mazungumzo na viongozi wa Tanzania kati ya Aprili 2 hadi 17, 2025. Ujumbe wa Tanzania uliwakilishwa na Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, viongozi wengine wakuu, washirika wa maendeleo, wawakilishi wa sekta binafsi na mashirika ya kiraia.
Kwa ujumla IMF imesema kuwa hali ya uchumi wa Tanzania ni nzuri, na ukuaji wa pato la taifa (GDP) ulikuwa asilimia 5.5 mwaka 2024 na unatarajiwa kufikia asilimia 6 mwaka 2025.
Mfumuko wa bei umedhibitiwa, ukiwa asilimia 3.3 mwezi Machi chini ya lengo la asilimia 5 lililowekwa na Benki Kuu. Hata hivyo, IMF imeonya kuwa kuna changamoto zinazoweza kuathiri uchumi, ikiwemo hali ya sintofahamu kimataifa, mizozo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na uchaguzi mkuu unaotarajiwa nchini ambao unaweza kuongeza matumizi au kuchelewesha utekelezaji wa mageuzi ya kiuchumi.
======== For English Audience =====
WASHINGTON, April 17 (Reuters) - The International Monetary Fund on Thursday said it had reached staff-level agreement with Tanzanian authorities that, once approved, would give the East African nation access to some $441 million in financing.
The agreement was reached on a fifth review under its Extended Credit Facility (ECF) and a second review under its Resilience and Sustainability Facility (RSF), the IMF said.
SOURCE: REUTTERS