Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 25,434
- 18,874
Ndugu zangu Watanzania,
Sasa mnaweza kuelewa ni kwanini Edwin Odemba alilia na kububujikwa machozi hadharani kama mtoto mdogo pale alipoona Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi ameshindwa kufika na kuhudhuria kwenye mdahalo kutokana na kutingwa na majukumu ya chama ,ambapo alikuwa anaendesha vikao vya Secretarieti katika maandalizi ya vikao vya kamati Kuu.
Mnaweza sasa kuelewa ni kwanini na wengine waliokuwepo wa CHADEMA na Act Wazalendo waligoma kuendelea na mdahalo bila uwepo wa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi.mnaweza kuelewa kiu na shauku kubwa ya washiriki kutamani uwepo wa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi.
Siyo kwamba washiriki na waandaaji walitaka kwenda kufanya mdahalo na Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi. Bali waandaaji walitaka kwenda kujifunza na kupata ufafanuzi wa Masuala mbalimbali,walitaka kwenda kuuliza mambo mbalimbali yanayowasumbua akili zao,walikuwa na maswali ya kuuliza na siyo hoja za kwenda kujadili na kujadiliana na Katibu mkuu wa CCM.
Ndio maana baada ya kukosekana kwake Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi waliamua na kuona hakuna sababu ya kuendelea na mdahalo,maana wao wanajuwa uwezo mkubwa wa kiakili,uzoefu wa kiuongozi,umakini ,utulivu na maarifa makubwa aliyonayo Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi ,na ndio sababu waliona ni nafasi ya kipekee kwa wao kwenda kujifunza na kuongeza maarifa . na hivyo kukosekana kwake kukawa hakuna sababu ya wao kuendelea na mazungumzo kwa sababu mwenye majibu na Mkata kiu yao na wakuwasaidia hayupo.
Kwa hiyo siku nyingine waandaaji wasiseme na kuita mdahalo bali waseme maswali mbalimbali kwenda kwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi juu ya masuala mbalimbali.kwa sababu simuoni mwenye uwezo wa kufanya mdahalo na Katibu mkuu wetu kwa makatibu wakuu wa vyama vya upinzani vilivyopo hapa Nchini.
Kinachopaswa kufanywa na makatibu wakuu wa vyama vya upinzani ni kuendelea kujifunza kutoka kwa katibu mkuu wa CCM. Kwa hakika Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi ni hazina kwa CCM na Taifa letu kwa ujumla wake.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.