Ili kuwa na uchumi imara fursa ya kipekee ni kilimo, ufugaji na biashara

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
20,616
22,512
Gas ya kupikia kwisha wakati huna jambo lolote mfukoni, au Gas iishe wakati una njaa na ndio tu ameanza kupika na wewe ndio uko njiani unatoka kwenye marejesho ya mkopo?

Mbaya zaidi, store hakuna mkaa na mara ya mwisho ulimkopa mangi na hujamlipa mpaka sasa...

Wajemeni, kuna afadhalli yoyote kati ya haya? unaweza kweli kuepuka kuota mvi katika umri huo ndrugu zango?

Sawa una kazi, Lakini Fursa ya kipekee sana kuepukana na yote hayo ni kilimo, ufugaji na Biashara...
jitahidi sana kua na vyanzo mbadala vya kujiongezea kipato, kutegemea chanzo kimoja ni hatari sana kwa afya yako, furaha na uhai wa familia yako.

Karibu sana Kilingeni huku shamba, siasa ni maisha ya ziada tu, huto juta na wala huna haja kunishukuru baadae ukifanikiwa.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Siasa ni ziada kivip ? Kwamba nikiwa chawa sitaishiwa na gesiii🤔
ni kazi rahisi sana kuipata na kuifanya baada ya kuwa umejiimarisha, umejizatiti vizuri sana kiuchumi mathalani kwenye kilimo, biashara au ufugaji 🐒
 
Back
Top Bottom