Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,255
- 1,563
Ni ukweli mchungu kwa kwa Makamanda wa Chadema, na hakuna Kamanda atakayekubali kuwa Chadema ya sasa imekwisha, haina uwezo wa kuleta upinzani kwa Chama tawala ambacho kimepata Makamu Mwenyekiti mpya.
Kila movement ambayo CHADEMA mnafanya kwa sasa inafeli vibaya saana, Join the chain imefeli vibaya saana, Chadema ya sasa inazidiwa hata na ACT ya bwana yule. CHADEMA ya kweli ilikuwa ile ya Dr Wilbroad Slaa tu, baada ya hapo CHADEMA imekuwa ikijongea kaburini kidogo kidogo na msipo anza upya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 Chama chenu hakitakuwa na utofauti na kile chama cha yule jamaa wa kugawa ubwabwa kwenye mikutano ya kampeni.
Mheshimiwa Freeman Mbowe, kama Mwenyekiti wa CHADEMA kwa sasa ni muda wake wa kupumzika, amekifanyia mambo makubwa CHADEMA na atakumbukwa kwa mchango wake katika siasa za upinzani, lakini Mheshimiwa Mbowe kwa sasa hana jipya la kuweza kuwaambia Watanzania wakakiunga mkono CHADEMA, hakuna Mtanzania atakayeunga mkono siasa za matukio, Vijana wengi sasa ni wasomi wanaotaka sera na sio matukio, Mbowe alikifaa Chama kipindi hicho cha siasa za harakati. CHADEMA mnahitaji Mwenyekiti mpya na hii itakuwa njia bora ya kuonyesha mna demokrasia ya kweli, Mkipata mwenyekiti mpya atajenga CHADEMA ili kuja kushindana na CCM miaka 15- 20 ijayo.
Ndugu John Mnyika , kama katibu wa CHADEMA , najua makamanda wote mnajua ukweli kuwa Mnyika mnamlazimisha tu kuendelea kuwa Katibu wa Chama lakini yeye muda mrefu amekuwa anataka kupumzika, Mnyika si mtu wa siasa za kiharakati wala si muumini wa siasa za matukio. Mnyika yule wa kujenga hoja akili yake sasa iko mapumzikoni mwili tu umebaki CHADEMA, Mnyika hawezi kukisaidia CHADEMA kwa sasa. Mnyika ameamua kukaa kimya, ni bora mkamuacha apumzike tafuteni Katibu mpya wa kuweza angalau kufikia uwezo wa Komredi Chongolo
Ngugu Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama, huyu ni Muumini wa siasa za kiharakati na siasa za matukio ambazo kwa sasa hazina nafasi katika Tanzania inayoendesha Siasa za kistarabu, siasa za utu na kuheshimiana, CCM wamepata Makamu Mwenyekiti hodari na nguli wa siasa za Tanzania, CHADEMA mnahitaji kupata Makamu Mwenyekiti ambaye ana weza fikia hata robo ya uwezo wa Kinana, najua ni ngumu kumpata mtu mwenye uzoefu na uwezo wa Komredi Kinana. Muacheni Ndugu Lissu aendelee na ajira yake UN, kwa aliyopitia ndugu yetu Lissu anahitaji muda mwingi wa kupumzika na kumtumikia Mwenyezi Mungu.
Siasa za kwenye mitandao huko the space na twitter hazitawasaidia kwa sasa.
Kuanza upya haijawahi kuwa vibaya, hata yule ndugu yenu wa ACT alikubali kuanza upya.
MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU MBARIKI RAIS WETU SAMIA SULUHU HASSAN.