Ikulu yamshangaa Dk. Mahanga

Mimi nimepata mshangao kidogo .ilikua kunahaja gani ya ukulu kumjibu mahanga,ikulu haifanyi kazi kwa magazeti wala mtu mmoja mmoja wala kwa mitandao ya kijamii,sasa kama kila mtu akitoa maoni yake ikulu itamjibu ,basi hii itakua ni wickness kubwa maana kila mtu atasema yake na kila mtu atakosoa kivyake. Au kwa sababu kasema mahanga .kwanza huu ni ubaguzi kama mwananchi wa manzese angekwenda kwenye vyombo vya habari akasema kama alivosema mahanga je sefue angemjibu? Mbona mh. Samuel sitta alisema raisi anasgauriwa vibaya haaa kwenye TRL mbona yeye hakujibiwa? Je kila atae kosoa au kutoa maoni serekali ikiona amepotosha itamjibu?
 
Daaaaaaaaaaaaahhhh... Dr. Mahanga yuko sahihiiiiiiiiii....!!!

Idadi ya wiraza ni OFISI YA KATIBU MKUU.... daaah kamaliza kazi hapa... yuko sahihi hadi kapitilizaaaaaaaa... 1000000% correct...!!!

Kumbe Hakuna kilichopunguzwa... ni ugali wa maharage... wengine kande ya maharage... kitu kile kile... except shape tu.. haaaaaa

So Makatibu wakuu ndio Ofisi ya Wizara... hii ni kweli kweliiiiii kabisa...

Mahanga hongera sana sanaaa... Semfue huwa hawezi kujibu hoja... eti ANASHANGAAA...!!!
 
Mimi nimepata mshangao kidogo .ilikua kunahaja gani ya ukulu kumjibu mahanga,ikulu haifanyi kazi kwa magazeti wala mtu mmoja mmoja wala kwa mitandao ya kijamii,sasa kama kila mtu akitoa maoni yake ikulu itamjibu ,basi hii itakua ni wickness kubwa maana kila mtu atasema yake na kila mtu atakosoa kivyake. Au kwa sababu kasema mahanga .kwanza huu ni ubaguzi kama mwananchi wa manzese angekwenda kwenye vyombo vya habari akasema kama alivosema mahanga je sefue angemjibu? Mbona mh. Samuel sitta alisema raisi anasgauriwa vibaya haaa kwenye TRL mbona yeye hakujibiwa? Je kila atae kosoa au kutoa maoni serekali ikiona amepotosha itamjibu?

Makongoro ameugusa UKWELI mtupu ndio maaana wametikisika

Mwenye akili anaelewa.....Sasa standard Two wa CCM hawaelewi wanapiga porojo tu
 
Makongoro ameugusa UKWELI mtupu ndio maaana wametikisika

Mwenye akili anaelewa.....Sasa standard Two wa CCM hawaelewi wanapiga porojo tu
Serikali ya awamu ya nne makatibu walikuwa 54, awamu ya tano makatibu wapo 49.

Sasa chagadema mnacholialia ni nini??

Kati ya 54 na 49 ipi kubwa??!
 
Serikali ya awamu ya nne makatibu walikuwa 54, awamu ya tano makatibu wapo 49.

Sasa chagadema mnacholialia ni nini??

Kati ya 54 na 49 ipi kubwa??!

Manaibu wangapi?

Alafu weka Organization structure hapa tuone upuuzi wenu

Eti makatibu wakuu wawili...Naibu katibu mmoja...Anaripoti kwa nani

Acheni kuhorojoa nyie Maguruwe
 
sefue analeta blah blah tu,asme katika serikali iliyopita hao makatibu na manaibu katibu wakuu 54 mchanganuo wao uko vipi,usije kukuta kati ya hao 54 makatibu wakuu 40 na naibu ni 14 na hawa 49 wa magufuli 44 ni makatibu wakuu...my point is,makatibu wakuu ndio wanaokuwa na vote(expenditure vote)....something is not clear kwenye kupunguza gharama kwa magu!!!
Nonsense! Jifunze kujenga hoja kwenye mitandao ya kijamii. Taarifa imetolewa na chanzo rasmi cha serikali...Sasa sijui unataka nini cha ziada.
 
Manaibu wangapi?

Alafu weka Organization structure hapa tuone upuuzi wenu

Eti makatibu wakuu wawili...Naibu katibu mmoja...Anaripoti kwa nani

Acheni kuhorojoa nyie Maguruwe
Chagadema wakati wanateua viongozi Wa ccm kuwa viti maalumu chadema ulikuwa wapi kuwashauri !?! Mpaka uje kumshauri Magufuli?!?


Tangu lini ukaitakie mema ccm mpaka uipe ushauri
 
Kimahesabu 54 ikikadiriwa ni 50 na 49 ikikadiriwa ni 50...huyo aliesema makatibu wakuu wamepungua hakusoma hesabu.
 
Chagadema wakati wanateua viongozi Wa ccm kuwa viti maalumu chadema ulikuwa wapi kuwashauri !?! Mpaka uje kumshauri Magufuli?!?


Tangu lini ukaitakie mema ccm mpaka uipe ushauri


Wale hawakuwa viongozi wa CCM...Nikueleweshe mara ngapi?

Wale ni wanachama wakongwe wa CHADEMA tuliowatuma Huko CCM kwa kazi maalum waliyoimaliza

CCM ndio mmetuweka kwenye Mess kama taifa...hamuwezi asilani kututoa kwenye mess mliyoitengeneza nyie

Hapa CCM mnanufaika na ujinga wa babu yako huko kijijini Mpitimbi
 
HOJA SI UKUBWA WA BARAZA, HOJA NI UKUBWA WA GHARAMA ZA KUENDESHA SERIKALI

Nimefuatilia jinsi ambavyo hoja yangu niliyoitoa juzi kwa nia njema ilivyojadiliwa nchini kwa kuungwa mkono na wengi na wengine kuipinga. Mimi nadhani hoja yangu isijadiliwe au kukanushwa kisiasa, bali iangaliwe tu kiuhalisia ili kusaidia Serikali ya Rais Magufuli.

Aidha najua sana kwamba katibu mkuu siyo mjumbe wa baraza la mawaziri. Lakini najua vile vile kwamba jina au cheo tu cha uwaziri si kila kitu kwenye kupunguza gharama za kuendesha serikali. Gharama za kuendesha serikali ni idadi ya mawaziri, makatibu wakuu na wakurugenzi wa idara mbalimbali za serikali, na gharama zingine za kuendesha idara zao.

Na wala sijapinga mazuri anayofanya rais hadi sasa. Mbona pale rais alipofanya vizuri tumempongeza? Kwa mfano kutumbua majipu ambayo yaliivishwa tayari na serikali ya awamu ya nne. Vile vile alipopunguza idadi ya wizara na idadi ya mawaziri kutoka 29 kufikia 19 mbona tulipongeza? Na hapa tuliamini ni mwanzo wa kupunguza ukubwa na gharama za kuendesha serikali. Nasema mwanzo kwa sababu ukubwa na gharama za kuendesha serikali si kupunguza tu idadi ya wizara na mawaziri, bali kupunguza pia idadi ya makatibu wakuu ili kulingana na idadi ya wizara....ni kupunguza na kuunganisha idara mbalimbali za serikali na wakurugenzi wake. Ukifanya hivyo ndiyo unapunguza gharama za kuendesha serikali. Na hii ndiyo ilikuwa ahadi ya Magufuli kwenye kampeni.

Lakini kama ameona kwamba kuleta ufanisi serikalini lazima ajaze watendaji wengi kwenye wizara, kama anavyoendelea kufanya, aseme tu hivyo, lakini akijua hatua hiyo haitapunguza gharama za kuendesha serikali ambazo wabunge, hasa wa upinzani, wamekuwa wakipigia kelele kwenye serikali ya awamu ya nne.

Hata hivyo hili la kuleta ufanisi pamoja na kuteua makatibu wakuu wengi wanaoonekana wazuri kwa utendaji, kuna wizara ambazo hakushauriwa vizuri na akateua makatibu wakuu wale wale na kuwarudisha pale pale wakati walikuwa "mizigo" na walikwamisha mno sekta husika katika awamu ya nne. Hawa ni watu ambao rais au katibu mkuu kiongozi angeenda kwenye wizara zao leo na kuitisha kura ya siri ya wakurugenzi na wafanyakazi wote, asilimia 90 ya watumishi wote wangewakataa makatibu wakuu hao. Ni heri kukosea kuteua kwa mara ya kwanza kuliko kukosea kuteua "mizigo" iliyokuwepo.

Tukirudi kwenye hoja ya msingi ya gharama za kuendesha serikali, nimesema na ninarudia kusema: bila kutakiwa kutoa takwimu hapa, gharama za waziri mmoja na ofisi yake ni ndogo sana kulinganisha na gharama za katibu mkuu mmoja na ofisi yake, kwani waziri tayari analipwa sehemu kubwa ya mshahara na marupurupu kutokana na yeye kuwa mbunge (na hapa niwajuze baadhi ya walionipinga kwamba waziri halipwi mishahara miwili - ya ubunge na ya uwaziri).

Na hapa hatujajadili mikanganyiko mingine ambayo haijawekwa wazi hadi sasa. Kwa mfano kutakuwa na afisa masuhuli mmoja wa wizara au maafisa masuhuli wawili au watatu kwenye baadhi ya wizara? Kwa kawaida wizara inakuwa na fungu (vote) moja; sasa katika hali hii kila idara ya wizara itakuwa na fungu (vote) tatu (ukiacha idara zinazojitegemea)? Je hili la afisa masuhuli mkuu wa wizara kutokuwepo haitaleta shida katika uwajibikaji? Na vipi katika kusimamiwa na bunge na kamati zake? Nani hasa mtendaji mkuu wa wizara atakayewajibika kwa bunge kwa mambo ya kisera ya wizara nzima? Wote watatu?

Hatua hii ya rais magufuli ya kuwa na makatibu wakuu wa vitengo (na siyo wa wizara) ingesubiri hoja ya kikatiba ya mawaziri kutokuwa wanasiasa (wabunge) ili wawe watendaji wakuu na wawajibikaji wakuu wa wizara (cabinet secretaries) kama ilivyo nchi ya jirani ya Kenya.

Lakini kwa sasa ningeshauri hoja hii iahirishwe halafu turudi tena kuijadili baada ya "taasisi" ya makatibu wakuu wapya kupangwa - kwa maana ya kila mmoja kupangiwa idara na wakurugenzi chini yake (na ninahisi kutakuwa na nyongeza ya idara). Na baada ya hapo uchambuzi wa gharama za kuendesha serikali hii ufanywe na ulinganishwe na gharama za uendeshaji wa serikali ya mwisho ya JK ambayo tayari ilikuwa inalalamikiwa kwa ukubwa wake.

Dr. Milton Makongoro Mahanga
 
Kama vijana Wa chadema uelewa wao ndio huu basi tena hiki chama hakitakaa kichukue dolla
Kwani wewe mwalimu wako wa darasa la tano alikufundishaje kuhusi hizo hesabu? Kati ya 40 na 50 kwenye 49 ipi iko karibu. Na kati ya 50 na 60 kwenye 54 ipi iko karibu!?
 
Inawezeka JPJM amepunguza garama za serikali kwa kupunguza mawaziri ambao ni wanasiasa wenye mishahara mikubwa na kuingiza makatibu wakuu wengi wenye mishahara midogo zaidi. Ngoja tuone atafika wapi lakini Sefue angeipinga hoja Mahanga kwa kuchanganua gharama za wizara/baraza la mawaziri ya JPJM na kuilinganisha na gharama wakati wa JK.
 
Endapo Katiba haitabadilika hakuna chama chochote kingine inaweza kutawala Tanzania zaidi ya CCM
Slaa aliposhindwa mkasingizia ni kwa sababu matokeo ya urais hayakubandikwa ukutani.

Mwaka huu yamebandikwa mkapigwa ,mmekeukia tena katiba!?!?!

Katiba itabadilishwa na mtapigwa sijui mtasingizia nini.

Hivi huko Pemba, Moshi, Arusha ikitumika katiba gani vile
 
Ni mapema sana kumkosoa magu vile vile ni mapema mno kusifia sarakasi zinazoendelea kwa sasa hivi.
 
Back
Top Bottom