Ikulu ya Tanzania

Wadau naomba kuuliza mwenye kujua historia ya ujenzi wa Ikulu yetu na wajenzi (kampuni) waliojenga Ikulu yetu.

Nasikia ilijengwa na wajerumani.Je, ni kweli?

Vile napenda kujua kama huwa kuna tender inayotangazwa na makampuni ya ujenzi ya kimataifa hushindana kupata tender hiyo?

Swali lingine ambalo najiuluza ni kuwa usalama wa Raisi na Ikulu yenyewe kwa ujumla unakuwaje iwapo ramani ya Ikulu imechorwa na watu wa mataifa mengine?!Mtu akijua ramani ya nyumba yako si anaweza kusaidia hujuma yoyote dhidi ya nyumba yako?

Je,ukarabati wa Ikulu hufanywa na makampuni ya wazawa au wageni?

Naomba mwenye ufahamu atujuze.
 
Ninavyojua mimi ni kuwa ilijengwa na Waisrael lakin yote kwa yote tuendelee kusubiria wadau wenye data kamili na za kujitosheleza.
 
Ukijua itakusaidia nini? Badala ya kuwaza lini barabara ya kwenda kwenu ilikarabatiwa na kwa msaada wa nano unauliza juu ya ikulu
 
Ninavyojua mimi ni kuwa ilijengwa na Waisrael lakin yote kwa yote tuendelee kusubiria wadau wenye data kamili na za kujitosheleza.
Muhahahaha wewe kwa sababu umesikia Waisrael wamejenga Ikulu nyingi Duniani na Ambayo ni Maarufu ilikuwa ni ile ya Saadam Hussein.... basi na kwetu wadhania ni vile vile??? kama ndio hivyo basi watakuwa ni Wayahudi maana wajerumani walikuwepo miaka mingi kabla ya Waingereza... na kabla ya Israel haijapata Uhuru.... maana hiyo ikulu lazima itakuwa Imejengwa na Wajerumani kwa Sababu Walikuwa wanapenda kujenga karibu na kingo za Pwani ili kukinuka waweze kimbia fasta kwa usafiri wa Majini.... Tizama Kirwa Boma lipo karibu na Pwani pia lipo Juu ya kilima
 
ya tanganyika bana!!sema nashangaa anakaa rais wa tanzania!
 
Kutoka Wikipedia inasema hivi...:- Ikulu - Wikipedia, kamusi elezo huru


[h=1]Ikulu[/h] Rukia: urambazaji, tafuta
Ikulu (State House) ya nchi ya Tanzania lijengwa kwa namna ya kipekee na Wajerumani mwaka 1891 na gavana wa kijerumani Julius Von Soden na kutumika kama ngome ya gavana. Iliharibiwa wakati wa vita ya kwanza ya Dunia. Baada ya vita ya kwanza ya Dunia Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa kikoloni wa Waingereza na hapo ngome hiyo(state house) iliitwa Government House na ilijengwa tena mwaka 1922 ambapo gavana wa Kiingereza Sir Horace Bytt alipochukua utawala. Majengo hayo yamejengwa kwa ubora wa pekee na ni ya kihistoria kwani yalikuwa ni Ngome za magavana.
 
ikulu ya Dar es salaam ilijengwa na wakoloni wote wawili. Wajerumani waliijenga kwanza ila sehemu ya juu ilipigwa mabomu na waingereza vita ya kwanza ya dunia. hivyo waingereza wakaijenga upya sehemu ya juu kama ilivyo sasa. so ikulu imejengwa na waingereza na wajerumani. kuhusu contractor hayo ni vigumu kuyajua..
 
Ikulu ilijengwa na Wajerumani na hawa jamaa wanapenda sana kujenga underground tunel kwa mfano pale Magereza karibu na idara ya statistics kuna tunel inatokea kisarawe na njia nyingi zimezibwa kwa milango ya chuma mpaka wenyewe waliofunga waje kufungua

Wajerumani wamefunga baadhi ya rooms pale Ikulu na hakuna hata ruhusa ya kufungua kwani kuna hazina kibao walizoweka na kuna mkataba waliwekeana na Mkapa juu ya kuzivuna hazina hizi lakini sijui issue hii iliishia wapi?

Wajerumani wajenga maboma yooote Tanganyika na kufungia hazina kibao sio Ikulu peke yake!
 

pumba hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…