Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Sasa we Barbarosa vp atoe mchango wakati anakatwa kodi kila siku,hizo kodi zilienda wapi?
Nimekwisha jaribu kuliezea na hapa wala sitetei Serikali bali nashindwa kuelewa ni jinsi gani mtu anavyoona ufahari na jambo la kujivunia kupiga picha na kusambaza kwenye internet mateso ya watoto ambao wangeweza pia kuwa wake, ningeelewa kama angeleta hiyo picha na kujaribu kutafuta suluhisho la kuwasaidia hao watoto hata kama ni kutafuta michango ndivyo jamii zinavyoendelea hivyo, na siyo kukebehi kwa kuwa tu Mpinzani huo ni Ujinga na kutokuelewa maana ya upinzani na kamwe upinzani hauwezi kuingia madarakani wa kufanya sabotage kwa maana wananchi siyo wajinga na wanaona!
Wananchi wote wanatambua kwamba kuna matatizo na kwamba Serikali kwa kuondoa Ada imejaribu kutatua tatizo ingawaje changamoto bado ni kubwa sasa, kwa mfano darasa lilikuwa na watoto 40 leo wanakuja mpaka watoto 200 sasa kila Mwananchi anatambua kwamba idadi imeongezeka kwa sababu Serikali imeondoa Ada sasa kukejeli na kupinga hilo hakuwezi kukujenga wewe kama Mpinzani kwani wananchi watakuona mara moja kwa hauna nia njema kwa kuwa unafanya sabotage sasa huwezi kufanikiwa!
Kama nilivyosema kuna mambo mengi sana ambayo hata Serikali iwe nzuri vipi haiwezi kuyafanya yote na hapo upinzani wanaweza kuyachukuwa lkn siyo kufanya sabotage ya kijinga na kitoto namna hii hiyo itaback fire kwa wananchi big time kwa maana wananchi siyo wajinga wanaona kwamba kuna tofauti kati ya kuwa na Ada na kutokuwa na Ada, sasa wewe kupinga hilo hawawezi kukuamini!