Ijue Mahakama ya Afrika Mashariki, Kwanini Hukumu Zake Hazina Rufaa na Kwanini Zina Puuzwa na Baadhi ya Nchi Washirika Sisi Tanzania Tukiwemo?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
53,337
120,836
Wanabodi,
Hii ni makala ya Jumapili ya leo, kazi inaendelea...
Screen Shot 2022-09-25 at 6.35.46 AM.png
Screen Shot 2022-09-25 at 6.36.15 AM.png

Kwa Maslahi ya Taifa, inaendelea na makala elimishi za kuijua Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambako mwanasheria wako, Wakili Pascal Mayalla, anakuzamisha kwenye Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sura kwa sura. Leo tunaenda SURA YA NANE: IJUE MAHAKAMA YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI ambapo makala hii itaelimisha kuhusu kuijua mahakama ya Afrika Mashariki, kwanini hukumu zake hazina rufaa na kwanini hukumu hizo zina puuzwa na baadhi ya nchi washirika nchi yetu sisi Tanzania tukiwemo?.

Sura hii inajumuisha Ibara ya 23 mpaka Ibara ya 47 kuhusu Mahakama ya Afrika Mashariki. Chanzo chake ni makubaliano ya Nchi Wanachama kuainisha na kuoanisha mifumo ya sheria ya nchi zao ifanane ili wakati Mtangamano utakapo kamilika, hii ndio itakuwa mahakama ya juu ya Afrika Mshariki. Kwa kuanzia, mahakama hii imepewa uwezo wa kupokea na kusikiliza mashauri yatokanayo na mgongano katika mkataba huu wa ushirikiano wa Afrika Mashariki tuu. Mahakama hii pia inapokea pia mashauri ya masuala ya haki za binadamu.

Hata hivyo, kuwepo kwa Mahakama hii hakutaondoa uwezo wa mahakama za kitaifa katika Nchi Wanachama, ila itatumika kama sehemu ya rufaa, isipokuwa pale ambapo imetajwa waziwazi kuwa jambo fulani litakuwa chini ya Mahakama hiyo tu. Mahakama hii ndiyo pekee yenye haki zaidi ya kutafsiri Mkataba huu wa Afrika Mashariki kuliko mahakama za kitaifa.

Very unfortunately, ule ukoloni mambo leo wa kutumia lugha za wakoloni, pia umebebwa na mahakama hii. Mahakama ya Afrika Mashariki itatumia lugha ya Kiingereza. (Ningefanikiwa kuingia kwenye EALA, hii ya matumizi ya lugha adhimu ya Kiswahili ndio ingekuwa ajenda yangu kuu ya kuipigania!. Wakati Jumuiya ilipoanzishwa nan chi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda, kwa vile zote pia zinatumia lugha ya Kiingereza kama official language, hili la kutumia Kiingereza lilikuwa sawa, lakini sasa jumuiya imetanuka, Rwanda, Burundi na DRC zenyewe zinatumia Kifaransa na Kiswahili, hazitumii Kiingereza, hivyo Tanzania lazima tujifunze ku set baadhi ya agenda na kuzipigania. Kukipigania Kiswahili kiwe lugha rasmi ya Mahakama hii ni jambo la maana sana.

Mahakama hii makao yake makuu yako Arusha, Tanzania.

Ibara ya 24 inahusu uteuzi wa Majaji wa Mahakama.

Majaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki watateuliwa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi. Kimsingi, wanapaswa kutoka katika Nchi Wanachama wa Jumuiya, yaani Kenya, Tanzània na Uganda. Majaji hawa wanapaswa kuwa waadilifu na kutopendelea upande wowote na hapa sasa ndipo umuhimu wa kutumia lugha ya Kiswahili unapozidi, huwezi kupata Jaji kutoka Rwanda, Burudi na DRC anayezungumza Kiingereza, ila Kiswahili wanazungumza.

Nchi zilipokuwa tatu, idadi ya majaji ilikuwa sita kwa kila nchi mwanachama kuteua majaji wawili. Mahakama itaongazwa na Rais wa Mahakama na Makamu Rais wa Mahakama. Urais huu utakuwa wa mzunguko kati ya Nchi Wanachama.

Ibara ya 28 mpaka 30 zinahusu Malalamiko kwenye Mahakama.

Mtu yeyote kutoka Nchi Mwanachama anaweza akapeleka malalamiko yake katika Mahakama hii.

Hata hivyo, malalamiko haya ni yale tu yenye nia ya kuhoji uhalali wa kanuni, agizo, uamuzi au kitendo chochote cha Nchi Mwanachama au chombo chochote cha Jumuiya na kutaka kuonyesha kuwa, kitendo kilichofanyika ni kinyume cha vifungu vya mkataba wa ushirikiano wa Afrika Mashariki. Malalamiko mengine yatakayoweza kupelekwa kwenye Mahakama hii ni yale yanayohusu migogoro kati ya wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya yenyewe.

Ibara ya 31 -37 zinahusu Mashitaka.

Mashitaka yanaweza kupelekwa katika Mahakama hiyo kwa maandishi au kwa mdomo. Walalamikaji katika Mahakama hiyo wanaweza kusimama wenyewe mahakamani au wakawakilishwa na mawakili au washauri wa kisheria. Mshauri huyo wa kisheria atakuwa na haki ya kufika mahakamani kila wakati shauri linapotajwa au kusikilizwa.

Ibara ya 38 mpaka 40 zinahusu Hukumu

Moja ya hatua za kwanza ambazo Mahakama inaweza kuchukua katika uwezo wake wa hukumu ni kutoa amri za muda. Amri za muda au maagizo yoyote vinatumika kuzuia jambo fulani kuendelea kufanyika hadi Mahakama itakapotoa amuzi wa mwisho Pia, Nchi Wanachama zinaagizwa kuwa, mara mashauri yapelekwapo katika Mahakama hiyo, Nchi Wanachama zitaacha kushiriki katika kitendo chochote kile ambacho kinaweza kuharibu usuluhishi wa ubishani huo, au hata kuukuza zaidi.

Katika kutoa hukumu, Mahakama inaweza kutoa uamuzi au maamuzi ya awali ambayo hutangulia hukumu. Maamuzi ya awali sio hukumu kwa maana halisi ya hukumu, bali ni hatua ya Mahakama kueleza msimamo wake juu ya kipengele fulani ambacho kinabishaniwa, na ambacho ni sehemu ya kesi nzima.

Baada ya kutolea Maamuzi vipengele vyote vinavyobishaniwa, na baada ya kupokea hoja za pande zote mbili, Mahakama itatao hukumu yake. Hukumu hii itakuwa ndiyo msimamo uliafikiwa na wengi wa majaji. Baada ya hukumu kutolewa, Nchi Mwanachama au Wanachama au vyombo husika vitakuwa na jukumu la kutekeleza maagizo ya hukumu hiyo. Katika utekelezaji wa hukumu za mahakama hii, kuna tatizo la kisheria na kimfumo, hakuna taka lolote la kisheria huku za mahakama hii kusajiliwa na mahakama husika, ili zisipotekelezwa zitolewe amri za kukazia huku hizi, matokeo yake ni nyingi ya hukumu za mahakama hii kupuuzwa nan chi husika!. (Mimi pia kama mwanasheria, kule EALA, ningesaidia kufanya marekebisho hukumu za mahakama hii zisajiliwe na mahakama za nchi husika ili ziwe binding!.

Kwa mujibu wa tovuti ya mahakama hii, hizi ni hukumu za mashauri 23 kuihusu Tanzania, yaliyopelekwa kwenye mahakama hii
  1. FREEMAN MBOWE & 3 OTHERS, LEGAL HUMAN RIGHTS CENTRE v. THE ATTORNEY GENERAL OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA - East African Court of Justice
  2. M/S QUICK TELECOMMUNICATION SERVICES v. THE ATTORNEY GENERAL OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA - East African Court of Justice
  3. EAST AFRICA LAW SOCIETY v. THE ATTORNEY GENERAL OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA & ANOTHER - East African Court of Justice
  4. OLOLOSOKWAN VILLAGE COUNCIL & 3 OTHERS v THE ATTORNEY GENERAL OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA - East African Court of Justice
  5. https://www.eacj.org/?cases=ololoso...ey-general-of-the-united-republic-of-tanzania
  6. https://www.eacj.org/?cases=paul-jo...-general-of-the-united-republic-of-tanzania-2
  7. https://www.eacj.org/?cases=the-man...ey-general-of-the-united-republic-of-tanzania
  8. https://www.eacj.org/?cases=paul-jo...ey-general-of-the-united-republic-of-tanzania
  9. https://www.eacj.org/?cases=christo...al-of-the-united-republic-of-tanzania-another
  10. https://www.eacj.org/?cases=applica...-general-of-the-united-republic-of-tanzania-2
  11. https://www.eacj.org/?cases=applica...ey-general-of-the-united-republic-of-tanzania
  12. https://www.eacj.org/?cases=referen...ey-general-of-the-united-republic-of-tanzania
  13. https://www.eacj.org/?cases=applica...ey-general-of-the-united-republic-of-tanzania
  14. https://www.eacj.org/?cases=referen...ey-general-of-the-united-republic-of-tanzania
  15. https://www.eacj.org/?cases=referen...general-of-the-united-republic-of-south-sudan
  16. https://www.eacj.org/?cases=antony-calist-komu-vs-attorney-general-united-republic-tanzania
  17. https://www.eacj.org/?cases=african...-vs-attorney-general-united-republic-tanzania
  18. https://www.eacj.org/?cases=anthony-calist-komu-vs-the-attorney-general-of-the-republic-of-tanzania
  19. https://www.eacj.org/?cases=african...ey-general-of-the-united-republic-of-tanzania
  20. https://www.eacj.org/?cases=eacj-application-no-8-of-2007
  21. https://www.eacj.org/?cases=referen...cretary-general-of-the-east-african-community
  22. https://www.eacj.org/?cases=modern-holdings-ea-limited-v-kenya-ports-authority
  23. https://www.eacj.org/?cases=rashid-...revolutionary-government-of-zanzibar-2-others
Udhaifu Mkubwa wa Mahakama ya Afrika Mashariki, ni Haina Rufaa ila review

Mahakama ya Afrika Mashariki haina utaratibu wa kukata rufaa kwenda mahakama nyingine yoyote, Hata hivyo, upande ambao haujuridhishwa na uamuzi uliutolewa unaweza kutoa maombi ili Mahakama ifanye mapitio ya uamuzi wake wa awali.

Hata hiyo, msingi mkubwa wa kupitia upya shauri fulani ni kupatikana kwa taarifa mpya na za kuaminika ambazo zingeweza kuathiri hukumu kama zingekuwa zimefahamika mahakamani kabla wakati wa kusikilizwa shauri. Hii inaifanya hukumu za mahakama hii kupuuzwa na nchi husika, kwa hoja kuwa hata zikipuuzwa, hakuna pa kwenda!, hii inaifanya mahakama hii kuwa a toothless dog!.

Mfano mzuri wa toothless dog wa mahakama hii, utashuhudiwa mwakani, baada ya wakili fulani kupeleka shauri la mgombea binafsi kwenye mahakama hii. Wakili huyo, licha ya kufahamu this is a toothless dog, bado atafungua tuu shauri hilo just for the record ili sasa kupata uhalali kwa maamuzi ya mahakama hii yasajiliwe mahakama za nchi washirika, ili kuzipa nguvu hukumu hizi kutekelezwa na ikibidi kukaziwa.

Hoja ya mgombea binafsi kwa Tanzania
  1. Ibara ya 5 ya katiba ya JMT, ya mwaka 1977, inatoa haki ya kupiga kura kwa kila Mtanzania aliyetimiza umri wa miaka 18. Haki hii ilipaswa kwenda sambamba na haki ya kupigiwa kura!.
  2. Ibara ya 21, ikatoa haki kwa kila mtanzania kugombea nafasi yoyote ya uongozi toka serikali ya mtaa hadi serikali kuu.
  3. Ule uhuru uliotolewa na Katiba wa kila mtu kuwa huru kushiriki shughuli za uongozi, kupitia ibara ya 21, umekuja kunyofolewa na ibara ya 39 na 67 (b)(c) kwa kuweka sherti, ili mtu kuweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, ni lazima awe ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa hivyo lazima adhaminiwe na chama cha siasa!, Haki zinatolewa na ibara moja halafu zinaporwa na ibara nyingine ya katiba hiyo hiyo!.
  4. Nchi za EAC zinajiandaa kuunda shirikisho la kisiasa, ambapo raia wa nchi hizo watakuwa huru kugombea nafasi za uongozi wa shirikisho, raia wa nchi za wenzetu watakuwa huru kugombea, lakini raia wa Tanzania hawatakuwa na uhuru huo kwasababu uhuru huo umepokonywa kinyume cha katiba na kinyume cha sheria, lakini ubatili huo umekuja kuchomekewa ndani ya katiba yetu kiubatili hivyo kuinajisi katiba yetu.
  5. Ili nchi za EAC kuunda shirikisho la kisiasa, lazima pia demokrasia za uchaguzi za nchi hizi zifanane.
Ili hoja hii iweze kusikilizwa, lazima kwanza kuipigania hii mahakama iwe na meno.
Wiki Ijayo tutaliangazia Bunge la Afrika Mashariki na madhara makubwa ambayo Tanzania tumeyapata kwa kupeleka wabunge mabubu kule EALA.

Paskali
 
Tukiwagusa Acacia tutashitakiwa MIGA alisikika Lisu msomi aliyesomeshwa kwa kodi za watanzania lakini badala yake tukaja kulipwa billion 700 na Acacia ikafutwa na ikaundwa kampuni mpya ya Twiga ambayo Tanzania tuna hisa 16% na kwenye top management ya kampuni wapo watanzania. Kupitia kampuni mpya ya Twiga watanzania wameendelea kupata gawio la mabilioni ya fedha kila mwaka zinazotokana na mauzo ya madini.
Lisu alilipwa na nani kuwadanganya watanzania?
------------ ------- ---------- --------
 
Huu uzi mzuri sana lakini ulipuuzwa, wanasheria mko wapi kutetea taaluma? iweje Mahakama iundwe halafu isiheshimike?
 
Back
Top Bottom