Ijue Katiba ya JMT kwa Jicho la Mtunga Katiba: Watanzania Tusishabikie Uhaini. Hukuna Uhaini wa Kauli na Maneno, Uhaini ni Mipango na Matendo

Ahsante kwa darasa.
 
Naunga mkono hoja!, watu wanatishika sana na maneno maneno, neno Samia must go sio uhaini kwasababu haijasemwa she must go how and when, hivyo kwa mujibu wa katiba ya JMT, muda wa mwisho wa Rais Samia madarakani ni October 29, 2025, ila akichaguliwa tena, anaendelea. Sasa kwa vile mwisho wa Urais wa Samia kwa awamu ya kwanza ni 2025, hakuna jinai yoyote mtu akisema 2025 Samia must go, ili asichaguliwe!, sio jinai mtu yoyote kutaka mgombea yoyote wa chama chochote asichaguliwe!.

Na hata ukisema Samia must go now, ili iwe ni uhaini lazima useme how?, kusema tuu Samia must go, sio uhaini, ila kuhamasisha watu waandamane huku wana chant "Samia must go" bila kusema when and how, bado sio uhaini, ila maneno hayo yanakuwa ni sedition!.
Uhaini ni mipango na sio maneno!.
P
 
Yaani makala zako huwa ni PhD tosha kabisa, sema vijana wengi wavivu kusoma, lakini una madini balaa, vijana wengi tulionao hapa jamiii forum kwa sasa ni wahuni, wavivu kusoma, halafu elimu sifuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…