IGP Mangu: Sina taarifa juu ya agizo la Rais kumpandisha cheo askari

Amesema hajapewa taarifa za Rais Magufuli kuagiza koplo Deogratius Mbango kupandishwa cheo baada ya kumdhibiti mke wa mmoja wa mawaziri wa serikali yake kwa kosa la kukiuka sheria za usalama barabarani.

" Bado hajapandishwa cheo kwa sababu sijapewa taarifa hizo na nitakapopewa taarifa atalazimika kwenda kwenye mafunzo kwanza, sisi jeshi la polisi tuna taratibu zetu" alisema IGP Mangu .

Chanzo: Nipashe

MyTake - ng'ombe wa masikini hazai .
Alipaswa Kujua Zaidi - Zipo Lugha za Kujibu Vizuri Jambo Hilo Bila Kuonesha Insurbodination maana hapo alikua kama anamjibu Rais. Ni maoni yangu
 
Nadhani wewe inawezekana hujamwelewa Mangu, hujamwelewa kabisa...na pia nadhani hilo gazeti limetia ka-chumvi kidogo kwa habari hiyo...Halafu sina kumbukumbu nzuri kuhusu kauli ya JPM siku ile akizungumza na Polisi... Mimi nilisikia tofauti kidogo (mtanisahihisha) kwa hili. Mimi nilisikia kama Magu anasema angalieni uwezekano wa kumpandisha cheo huyo...Sasa hili lina maana kubwa kwa maana, jeshini (sina hakika sana na polisi) lakini katika JWTZ vyeo vinapandishwa kwa kozi... Haiwezekani itokee tu, unaamka halafu unaambiwa wewe ni SAJENTI, haiwezekani...kuna kozi zake za uongozi...Hata hao majenerali wanapandishwa cheo baada ya kupita kozi mbalimbali, ingawa unaweza kwenda kozi hizo na usipandishwe cheo, kutokana na nafasi...Ila kwa huyo kijana wa polisi kama ataenda kozi basi hilo ni moja kwa moja atapanda cheo, kwani ni agizo. Halafu upo wakati inawezekana mtu kwa maana ya askari amefanya jambo kubwa kitaifa Amiri Jeshi anaweza kwa mamlaka yake akampandisha mtu cheo, kwa utaratibu uliowekwa.
Sasa angeeleza hvyo, ila inaonekana alijibu kw jeuri....
 
Back
Top Bottom