IGP Mangu kajitofautisha na wengine

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,846
730,319
Ni jambo ambalo linaweza kumgharimu lakini at least amesimamia utawala wa sheria
Kwenye sakata la askari aliyedai kutukanwa na mke wa waziri Mahiga, Magufuli aliuagiza uongozi wa jeshi kumpandisha cheo mara moja askari huyo kama morali kwa wengine
Lakini IGP Mangu amekosoa kiaina uamuzi huo kwa kusema kwamba hana taarifa rasmi lakini hata hivyo atakapozipata itabidi askari mhusika aende mafunzoni kwanza
Hapa maana yake ni kwamba huko mafunzoni akifeli asahau kupanda cheo cha matusi! Mangu amesimamia taratibu na kanuni hii itampa heshima kubwa...nimejaribu kujiuliza ingekuwa ni Makonda Magesa na wengine wangeweza kufanya hivi kweli? Jibu ni hapana kwakuwa wamepewa vyeo kama zawadi, Mangu ni professional na kaitendea haki profession yake
 
Mkuu kwenye majeshi hakuna mihemko kule..unakumbuka Waziri Kitwanga alipoliagiza jeshi kufanya operesheni ya kusafisha majambazi kwa kuvamia mapori ya Mbagala..Siku iliyofuata Kamati ya Ulinzi na Usalama ikamuambia hakunaga amri kama hizo kwenye mambo kama hayo kuna taratibu zake..Lile agizo lilifia palepale. Kwenye Majeshi huwezi kupanda cheo bila ya kurudi kozi na kuburuzwa upya..
 
Ni vizuri kusimamia sharia...kuna kitu kinaitwa precedence...akimpandisha huyu cheo atakuja mwingine kesho na kudai kupandishwa cheo kwa vile naye katukanwa...ukikataa unakuwa hauko fair kwa taratibu za kazi...kwa uufupi ni kama ku redefine vigezo vya kupandishwa vyeo...je itakuwa sahihi? ha ha ha tutaanza kuona kila askari na recorder....
 
Haitatokea tena IGP keshamaliza kila kitu na pia ni salamu kwa Magu
 
Hapa naona Baba ndevu, Mtoto ndevu....

Anyway...
Naona sasa umefika wakati wetu sisi waTanzazia tujue namna ya kutofautisha mambo ya jukwaani na utaraibu wa sheria ya kupandishwa vyeo.
Kimsingi IGP yupo sahihi, na kimtazamo Mr President alitoa tamko kwa kusukumwa na mihemko kwa kutokujiwekea mipaka ya jinsi ya kuzungumza na yapi yazungumzwe kwa wakati gani.
 
Mangu is not a good person, Ana tabia ya upendeleo hata akiwa kazin, mwaka 2013 akiwa RPC, mwanza Kuna askari aliua raia kwa makusudi, lakin sisi Kama wanahabari tulihitaji kujua msimamo wake kwa askari yule lakin alipiga kimya Ili kulinda jeshi lake, angeangalia upande wa pili wa haki za binadamu
 
Ulichokisema Mshana ni sahihi kabisa, angekua IGP mwingine au tuchukulie mfano mzuri , KOVA ndio angekua IGP yule askari angepandishwa cheo siku ile ile na kuwa RTO dar.. Hongera Mangu na washauri wako.
 

Ni kweli huenda asiwe good person kwa mambo mengine lakini kwa hilo sakata LA mke wa waziri na tamko LA JPM naungana na mshana jr kwamba ameonyesha ukomavu.
 
Mkuu,
Unaposema Mangu is not a good person hapa naona kama kidogo umepotoka, kwasababu unaweza tu kusema he is not a good person iwapo umewahi kuishi nae, kufanya kazi pamoja nae, au kama una ukaribu sana na yeye.
Na kuhusu kunyamaza kwake, huo ni mtazamo wako aiseeee....
Nijuavyo mimi Mangu ni kiongozi, na sio bosi. Hapa ifike kipindi tujue namna ya kutofautisha haya mambo.
Naweza sema IGP Mangu sio mtu wa kukurupuka na husimamia zaidi misingi ya uongozi na sheria za kazi yake.
 
Lakini IGP Mangu amekosoa kiaina uamuzi huo kwa kusema kwamba hana taarifa rasmi lakini hata hivyo atakapozipata itabidi askari mhusika aende mafunzoni kwanza

JF noma sana!
Unajua kilichomkuta Kamanda mmoja wa USA kwa kupishana Kauli na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama!
Tangazo la Raisi ni Amri hali hitaji taarifa ya Kimaandishi na hasa hili la majeshi ya Ulinzi na Usalama!
 
JF noma sana!
Unajua kilichomkuta Kamanda mmoja wa USA kwa kupishana Kauli na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama!
Tangazo la Raisi ni Amri hali hitaji taarifa ya Kimaandishi na hasa hili la majeshi ya Ulinzi na Usalama!

Kiswahili sanifu ni AMIRI JESHI usiweke tena neno MKUU kwasababu neno AMRI ni neno la kiaraabu likimaanisha neno MKUU, kwa hiyo ukisema AMIRI JESHO MKUU ni sawa na kusema BARABARA YA MOROGORO ROAD
 
Watu wa sheria ebu tufafanulieni kidogo je ni sahihi mangu kupishana na amiri jeshi? muongozo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…