Idara za vijana kwenye vyama zimekosa mweleko. UVCCM na BAVICHA hawaeleweki

Matongee

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
1,045
2,664
Ndugu wanaJF huu ni uzi wangu wa kwanza hapa ninaandika nikiwa nina hasira zisizo na mfano dhidi ya hizi idara za vyama vya siasa. Hawa vijana wamekosa mwelekeo na kuishia kuwa vituko tofauti na malengo ya uweo wao. Leo nitatoa mtazamo wangu kuhusu idara maarufu za ACT, BAVICHA na UVCCM kwa sababu vyama vingine ni kama vile hazina idara za vijana. Kuna mtu anajua viongozi wa vijana wa TADEA, PPT Maendeleo, na vingine vidogo vidogo?

Ngome ya vijana ACT
Hii idara ndani ya ACT inayoongozwa na Abdul Nondo bado ni changa ila imekuwa ikiendeshwa kiujanja ujanja na kuishia kutumika na Abdul Nondo kujipatia sifa na umaarufu binafsi. Kwa mara kadhaa wamekuwa wakitishia maandamano ambayo yanaishia getini kwao na kuongea na waandishi wa habari. Nondo na wenzake wakijipanga watakuwa imara. Waache ujanja ujanja wa kiboya.

Baraza la vijana CHADEMA (BAVICHA)
John Pumbulu na wenzake tayari wameshafeli na kukosa mwelekeo mazima. Hakuna namna unaweza ukasema BAVICHA ina jipya. Imefikia wakati BAWACHA wana mvuto kisiasa kuliko BAVICHA. Kina Pumbulu na wenzake wamekuwa bendera fuata upepo kwa vigogo wa chama. Hakuna siku wameibuka na hoja zao binafsi zaidi ya kusapoti kinachotamkwa na Mbowe, Lema na vigogo wengine wa CHADEMA. Kwenye hii ishu inayoendelea ya DP World sijasikia la maana hadi sasa toka BAVICHA. Ninashauri BAVICHA iwekwe chini ya uangalizi wa BAWACHA kwa miaka mitano.

Umoja wa vijana CCM (UVCCM)
Kwanza ninashauri UVCCM ibadilishwe jina na kuitwa Umoja wa watoto wa vigogo wa CCM. Hii idara imetawaliwa na watoto, ndugu na jamaa wa vigogo wa chama. Kama ni kijana ambaye huna mtu kwenye ukoo wako ambaye ni kigogo wa CCM basi fanya shughuli nyingine kwasababu utaishia kuwa chawa tu. Huko Arusha tumeona mwenyekiti wa vijana mkoa ni mtoto wa Meya wa jiji kupitia CCM. Yaani noma sana. Ukifuatilia majina ya wale chipukizi wa CCM ndo balaa zaidi. Watoto wa vigogo watupu.

Kinachokera ni hawa vijana wa CCM kukosa hoja zao binafsi kama ilivyo BAVICHA na kuishia kuwa machawa wa viongozi. Karibu kila kiongozi wa UVCCM ni chawa wa kiongozi fulani wa chama. Kimsingi ni watu wanaotumika na vigogo kwa maslahi yao. UVCCM ibadilike na kurudisha zile enzi za vijana wa TANU kina Seth Benjamin. Au wale vijana wa TANU waliokomaa hadi serikali ya mwalimu Nyerere kukubali hoja ya makao makuu ya nchi kuwa Dodoma.

Huu ujinga wa UVCCM kupoteza muda kutaka kuandamana kuunga mkono mkataba wa DP World ufikie mwisho. Enzi za J Kikwete tuliona UVCCM walitaka kuandamana kuunga mkono hotuba ya rais. What a shame? Kimsingi kwa sasa mtu unaweza ukajisikia vizuri kuitwa mwanaCCM ila sio UVCCM.
 
Uvccm ndio hovyo kabisa,low minded ndio wamejaa humo,wakiwa na matumaini ya kiteuliwa,ni aibu kwa kijana anayejitambua kuwa uvccm,unless aongozwe na njaa ya kifikra. Hopeless kabisa.
 
Back
Top Bottom