kambagasa
JF-Expert Member
- Aug 18, 2014
- 2,261
- 1,785
Wanaume wa Dar na wanawake lenu moja.Habari zenu wapendwa,
Mimi mwenzenu sijui nina balaa au gundu au mkosi yani hata sijui niseme nini kitu gani, maana kila mwanamke ninayempata ana visa vyake pia, huyo wa juzi nimemuacha kwasababu ya kuomba hela sana, hadi nikaanza mbele kimyakimya.
Nimempata huyu dada mwingine ambaye tulitongozana Facebook huyu sasa raha yake ni moja tu ni kwamba haombi hela wala nini, ila ukiwa nae inabidi ujiandae kisaikolojia, yaani demu anapokea simu kila wakati, mbaya zaidi anapokea simu za wanaune tu na muda mwingi yupo bize na kujibu msg za watsap na za kawaida.
Yaani hana raha ukiwa nae kinachonikera ni kwamba akipigiwa na hao wanaume wengi wao wanamuuliza "upo wapi" utakuta yupo kwangu ila anawambia nipo Ubungo,au nipo kwa ma mdogo Gongo la mboto ila narudi.
Sasa hii kwangu imenishinda kwa kweli,maana ananipa jaka moyo sana kwa kweli hadi karaha,wadada kwanini mpo hivyo siku hizi? Kuwa na wanaume wengi ni raha au sio?