Huyu mpangaji mwenzangu nashindwa kunielewa

lusanasaimon

Senior Member
Jan 19, 2023
108
264
habari za leo I hope nyoote hamjambo.

wakuu kwa wale wenzangu na mimi ambao bado tunajitafuta yaani tunaishi kwenye nyumba za kupanga mnawezaje kuishi na wapangaji wenzenu wanaotaka kujua maisha yako kindaki ndaki?

iko hivi mimi ni kijana na nina miaka 26, na nina mke japo hatujapata mtoto na nimejiajiri na vibiashara vidogodogo ambavyo nimeajiri vijana. mimi nikusimamia na kuhakikisha mambo yanakua kwenye mstari kama kufuata bidhaa ambazo zinakua zimekwisha na kwenda kufunga mahesabu. mara nyingi huwa sipatikani sehem husika mimi niki maliza kama ni asubuhi narudi zangu nyumbani kutulia mimi sio yule mtu wakujichanganya na watu sana. kwasababu situmii kilevi kwamba utanikuta bar nk .

mara moja moja huwa tunatoka wikend na wife, sasa hapa tulipopanga tuko wapangaji wa tatu na wote tuna wake japokua kwenye hawa wapangaji kuna jamaa mmoja na yeye anamke lakini na wao hawa jabahatika kupata mtoto. huyu mwingine ndio ana familia na wote (wanaume) huwa wanaamka nakusepa zao. nyumbani kunabaki wake zao sababu mke wangu na yeye nilimfungulia biashara yake ya duka la nguo, so mara nyingi akisha amka akafanya majukumu yake kama mwanamke nyumbani basi huondoka kwenda kwenye mihangaiko yake ya kila siku na huniacha nyumbani. na huwa nina kawaida natoka satatu natembelea biashara zangu na kuwajulia hali vijana basi kama hakuna tatizo na rudi zangu nyumbani kutulia na maisha yanaendelea.

sasa basi kutokana na maisha nimeyokua ninaishi hata hapa tulipopanga hakuna anaejua mimi na fanya kazi gani. wanaonaga ni salam na vijistory vya hapa na pale kama majirani basi sinaga mazoeya ya hovyo na mtu.

sasa leo wakati nimepita naelekea zangu biasharani kuna mama ni wamakamo kidogo na ni jirani yetu nyumba inayofuata ndio kanisimamisha baada yakumsalimia akawa ananipa story wanazokua wana mzungumzia wife hawa wanawake wa wapangaji wenzangu,

ya kwamba mke wangu ni mjinga haiwezekani mtoto mdogo kama yeye awe ndio anatunza mwanaume (mimi sasa) kwa kila kitu, anamvisha na kumlisha, eti mwanaume wake (mimi) hana kazi yupo yupo kazi ni kulala. hajishugurishi na mambo mengine kibao

nimeishia kucheka na nikamjibu yule mama. nikawaida acha waseme wanavyojua wao kwa sababu hakuna anaejua maisha yetu na tunaishije.

na hivi ndivyo ninavyo penda kuishi sipendi majilani wanijue kiundani zaidi

kama na wewe umeshawahi kukutana na wapangaji wafuatiliaji wa maisha yako kama mimi tena wake za watu weka maoni yako
 
Wapotezee kabisa watanzania wanapenda kumjua mtu Sana ,wakiona huna time wanakuwa na maswali na maneno mengi ,

Niliwahi kupata tatizo la moyo so nikaomba rikizo ya matibabu nikapewa nikawa nashinda home watu wakasema nimefukuzwa kazi na make ndio ananilisha na kusomesha watoto nilishangaa , DK alinizuia kunywa pombe kabisa wakasema nimefuria nimefukuzwa kazi Sina hata pesa ya pombe usihangaike na watu wapuuzi hasa hapa dar pamejaa wajinga wengi.

USSR
 
Mkuu, issue ndogo kama hii ndio unaandika kurasa 5,,,!!! mbona kama upo kwa ajili ya kijinadi..
Kufuatiliana kwenye maisha ni mambo za kawaida hata ww hapo ulipo Kuna watu unawafuatilia.. Bila kufuatilia maisha ya watu huwezi kuingia kwenye ushindani wa maisha kuelekea mafanikio.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom