Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 2,334
- 3,049
- Huyu mlokole anafanya kazi ya uhasibu kwenye shirika kubwa, lakini hajawahi kuiba hata senti. Eti anasema wezi hawataingia mbinguni. Mtu ana nafasi ya kutajirika haraka kwa pesa za shirika, yeye anakomalia uaminifu. Ujinga mtupu!
- Akipanda magari ya abiria, akizidishiwa chenji, anamrudishia konda pesa iliyozidi. Kweli huyu mtu hana akili! Wengine wangetumia nafasi hiyo kufurahia "baraka za ghafla," lakini yeye anang'ang'ana na uaminifu.
- Ukikutana naye, anajisifia eti hajawahi kuugua kisonono wala kaswende. Hayo magonjwa ndiyo "stori za mjini"! Eti yeye anajivunia maisha ya usafi. Mjinga sana huyu!
- Akikosewa au mtu akimtukana, hajibu matusi wala kupigana. Anaamini eti "kisasi atalipa Bwana," badala ya kujitetea kwa ngumi kama mwanaume. Ujinga mtupu!
- Huyu mlokole tangu aoe hajawahi kumpiga mke wake. Mke akimkosea, anamsamehe badala ya kumpiga na kumfundisha "adabu." Hii kweli siyo mental illness?
- Hawezi kusema uongo hata kidogo, hata kama uongo unamsaidia kukwepa matatizo. Eti anasema waongo watatupwa motoni. Huyu amewehuka!
- Akipata mshahara wake, anatoa fungu la kumi na kuwasaidia maskini. Jamani, badala ya kujilimbikizia mali yake, anawaza kusaidia wengine! Kweli huyu hana akili.
- Ana watoto wazuri, eti anawalea kwa maadili ya Kikristo badala ya kuwaacha "waende na wakati." Anawazuia wasitazame picha chafu kwenye mitandao, eti Mungu hapendi. Huyu mtu amepitwa na wakati!