Huyu mganga wa kienyeji amenipa masharti magumu sana kuyatekeleza

very strategic,amejua ukiacha kunywa na ngono saving yako itaongezeka + hiyo 20,000 lazima uwe unahangaika kutafuta hela. ukilala umekaa utakua unawaza mambo mengii na akili itakukaa sawa, fuata masharti pesa yaja
 
Mbona magodo tu dogo hayo?? Nitakuelekeza wengine unachapwa viboko vitatu kila siku usiku,,ukiamka asbhi zimejaa uvunguni.. Kula unavyotaka lala unapotaka,tembea na mabint wote unaotaka,toa msaada unavyotaka,vaa unavyotaka,, ila usiku ukifika unapigwa fimbo tatu pwaaa,pwaaa,pwaaaa,na hata mkeo ulielala nae hawez kusikia wala ukiamka asbhi hakuna maumivu yeyete....
Duh, Haya ndio rahisi mkuu, vp wakati wa kuchapwa unasikia maumivu??
 
Mbona masharti yake mepesi sana , sema ww tu hujawa tiyari, na huwezi kwenda direct kwa Mganga ukafanikiwa unatakiwa upate kinga ya ujasiri kwanza na ya kusogeza nyota ndo uende kwa MTU kama Huyo, tofauti na hapo utateseka sana sababu hadi hapo umevunja masharti mafanikio yako maishani ni kidogo sana kama punje ya haradani.
Salaam wanaJF.

Ugumu wa maisha hupelekea kufanya kila linalowezekana (ukiacha kuua) ili mkono uingie kinywani. Na sasa kuna hawa wataalamu wetu a.k.a waganga wa kienyeji ambao wao wamejaaliwa katika kufanya sayansi ya asili ,sayansi ya kumsaidia mtu utajili ilihali wao wakiwa na maisha magumu, maisha ya kukaa machakani au mapangoni.

Katika pitapita yangu Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, nikafika kijiji fulani kinaitwa Soni.Hapa kuna mganga wa kienyeji matata sana.Jamaa yangu mmoja akashauri tumwone bwana huyu ili tujue kama kuna fursa toka kwake.Basi asubuhi na mapema ya May 19, 2017 tukajongea kwake porini.

Agenda yangu kichwani ikawa ni kupata mapesa mengi ghafla bila kuvuja jasho au kuua binadamu. Tukakubaliana "Terms and conditions". Masharti aliyonipatia ni kama yafuatayo:-

1. Nikitaka kulala, nilale nikiwa nimekaa, kwa miezi 6 mfululizo.

2. Nguo ya ndani (chupi) niliyokuwa nayo ndo niitumie hiyohiyo na haitakiwi ifuliwe kwa miezi 6 mfululizo

3. Popote ninapopishana na mtu, nipite upande wa kushoto kwa miezi 6.

4. Nisifanye mapenzi, kunywa beer wala kuvuta sigara kwa miezi 6.

5. Kila wiki niwe namtumia elfu 20 kwa mpesa

6. Sitakiwi kumwambia mtu siri zote physically.

Ndo haya tu masharti yake.Chaa

Nimejaribu kuyatekeleza ndani ya siku 2 toka aliponoambia, nimeshindwa kabisa. Yaani ni kama aliwasiliana na watu wangu tunaokunywaga nao pombe na kwenda club.Wananipigia simu nijoin toka ile siku amenipa hayo masharti.

Inakuwaje waganga wa kienyeji wanakuwa na masharti magumu sana ile hali wakijua hayatekelezeki? Mbona wao pia wana maisha mbuzi tu?

Karibuni
 
Hivi kuna wanaume bado wanavaa chupi siku hizi?
Au umeambiwa uvae chupi ya wadada Na mganga!?
 
Huyo mganga ana busara kakuona pimbi ndio maana kakupa masharti magumu ilu ujue utajiri hauji bila kutoka jasho
 
mi niliambiwa nifuge njiwa dukani nikashindwa aisee
aisee hii ya kufuga njiwa umenifanya nimkumbuke mzee flan iv nilimkutaga huko huko lushoto Anaitwa katema anauza sana vifaa vya ujenzi, yaaan lile duka limejaa njiwa mwanzo mwisho, soo pengne na yy n hao hao
 
Kama unaamini katika Kristo Yesu basi wasiliana nami nitakusaidia 0686997270
 
Back
Top Bottom