Huwa naepuka kabisa kusikiliza umbea wa mwanamke wangu, juzi niliusikiliza umeniweka njia panda

Teslarati

JF-Expert Member
Nov 21, 2019
2,384
9,556
Kama kuna kitu huwa sipendi nikiwa na mwanamke ni pale anaanza kunipa umbea. Hii inatokea sana baada ya game nono (CHAPUTA hamtojua hili)

Sasa bwana, usiku wa juzi kwenye kutuliza kichwa huyo akaja na story, mie nikawa namuitikia tu kutokumkatisha (hapa ndo nilifanya kosa maana huwa namkatisha akianza story za umbea). Si akaniambia fln na fln wanatembea, huyo fln wa kike ni dem wa rafiki yangu damu damu, lkn huyo fln wa kiume alishatambulisha kwa rafiki yangu kwamba ni bamdogo mtu. Nilivuopata hizo taarifa nikastuka kdg, nikamuuliza una uthibitisho, akasema ngoja nikuhakikishie.

Yule mwanamke kwa kuwa ana kiu ya kunihakikishia umbea wake si akampigia simu pale loudspeaker yule fln wa kike, akaanza kumuuliza, "Lile gari shem (fln wa kiume) alosema atakununulia limefika? Binti akacheka akasema amekataa gari ila amaomba awe anachukua kodi ya nyumba ya huyo jamaa iliopo mbezi.

Shida wife hajui undani wa urafiki wangu na huyu jamaa anaeibiwa, sasa najiuliza hapa nimsanue jamaa kama anaibiwa au vp. Jamaa ameshamvisha hadi pete ya uchumba huyo binti na tulilewa balaa kwenye engagement party yao. Niko njia panda kiukweli.
 
Huo msala siyo wako.
Jali mambo yako.
Unaweza kumtaarifu akamsamehe na urafiki wenu utaishia hapo , utamtazamaje usoni shemeji yako akijua wewe ndiye uliye msagia kunguni ?
Si unajua mwanaume akipewa ile kitu anaweza kuulizwa msaga kunguni akamwambia ukweli?
 
Huo msala siyo wako.
Jali mambo yako.
Unaweza kumtaarifu akamsamehe na urafiki wenu utaishia hapo , utamtazamaje usoni shemeji yako akijua wewe ndiye uliye msagia kunguni ?
Si unajua mwanaume akipewa ile kitu anaweza kuulizwa msaga kunguni akamwambia ukweli?
Mjinga namba tatu wewe .

Keshakuambia Rafiki wa Damu Damu, Hawa ni zaidi ya Ndugu, wanapeana deals , wanashaurisna, wanakunywa pamoja.

Wewe ni rafiki au mdananda??
 
Huo msala siyo wako.
Jali mambo yako.
Unaweza kumtaarifu akamsamehe na urafiki wenu utaishia hapo , utamtazamaje usoni shemeji yako akijua wewe ndiye uliye msagia kunguni ?
Si unajua mwanaume akipewa ile kitu anaweza kuulizwa msaga kunguni akamwambia ukweli?
Hahahahahaa, ile kitu ile inavunjaga urafiki kabisa.
 
Mjinga namba mbili wewe.

Kwann akaushe?.

Rafiki yako akijua unamfukuzia Demu mwenye Ukimwi ... Ungependa akushtue au akae kimya??.


Kama ni wewe, na huyo ni mwanamke ulomviaha Pete tayari Kwa Ndoa.


Lipo lilosahihi kwako??.
Ndo maana nasema ni dillema hata kwangu.
 
Si huwa mna msemo wenu "bros before hoes", msanue tu huyo mwanao wanawake si ni wengi sana, asijali atapata tu huyo malaika anayemtaka
Shida haya mambo hujui jamaa anapewa style gn. Zisije zikawa ni zile style hatari ww ndo ukaonekana mmbaya, wakati huohuo namuonea sana huruma jamaa
 
Kuna vitu as a man, hutakiwi kuvishadadia hasahasa umbea! Fanya kama hujui kitu mpk atakapo sanuka mwenyewe. Ila wanawake washenzi sana
Kuna setup nataka niiweke ili ajionee mwenyewe na maamuzi atayafanya yeye baada ya kuona, nitakaa pemben kama sijui kitu
 
Back
Top Bottom