Mwizukulu mgikuru
JF-Expert Member
- Oct 21, 2021
- 5,928
- 14,158
Katika moja ya mambo ambayo nchi yetu imerithi kutoka kwa wakoloni ni hili la kuwalipa mishahara mapema watumishi wa majeshi hasa JWTZ na kuwaacha watumishi wengine wakisota kwa muda inatakiwa ukomeshwe kama sio kupigwa vita kabisa. Sote tunafahamu kuwa katika nchi yetu kumeundwa vyama mbalimbali vinavyojiita eti ni vyama vya wafanyakazi kama trade union congress of Tanzania (TUCTA), Chama Cha waalimu Tanzania (CWT) na Tanzania union of industrial and commercial workers( TUICO) vyama hivi vimekuwa mstari wa mbele hasa katika kukusanya michango ya kila mwezi kwa wanachama wake ambao ndio hao watumishi. Na ukiangalia moja ya malengo ya kuanzishwa vyama hivi ni kupigania maslahi ya watumishi, lakini vyama hivi vimekuwa ni mbadala mwingine wa kuwanyonya watumishi..