Huu ndio utajiri mkubwa utakaoupata kama utaamua kufanya biashara hii

Tatizo wanaoandika haya sijui kwanini wao hawawi mabilionea wa kwanza....

Hivi wewe unamjua Meshack Maganga kweli au unamsikia tu??? Na huyo wa pili Albert Sanga unawajua kweli?? Au ndo yale yale ya matajiri wa Dar??? Hao jamaa nimesoma nao O level Mazengo Tech School. Na nnawafahamu personally. Na nna shamba Iringa/Njombe na Scania trucks za mizigo. kama Albert
 
Asee, wee jamaa unanipa moyo sana wa kuanzisha upandaji miti uko iringa. Wazo ambalo ninalo tangu mwaka juzi,ila tatizo nipo nje ya Tz na kuja uko ni mara chache sana na kwa short time aseee. Ila wew umelima wapi yaaan wilaya gani? Na je? Nikipata shamba tupu naweza pata kijana wa kulitunza?

Ulishaanza?
 
Nimeelewa kitu apo

U.S. Attorneys » Southern District of Texas » News

Department of Justice
U.S. Attorney’s Office
Southern District of Texas.
Friday, August 9, 2019

11 Sentenced in Transnational Heroin Trafficking Ring

HOUSTON – A total of 11 men from the countries of Tanzania, Pakistan and Iran have been ordered to federal prison for their part in trafficking multiple kilograms of heroin to the United States from abroad, announced U.S. Attorney Ryan K. Patrick.

Ali Khatib Haji Hassan, 49, Makame Haji Mwinyi, 49, Ernest Michael Mbwile, 35, Abdulahtif Juma Maalim, 43, Ibrahim Omary Madega, 52, Tiko Emanuel Adam, 41, Iddy Saleme Mfullu, 46, Mohammed Said Mohammed, 48, Daud Michael Vedasto, 58, all from Tanzania, previously pleaded guilty as did Salim Omar Balouch, 36, from Iran, and Abdul Basit Jahangir, 40, from Karachi, Pakistan.

On Aug. 7, 2019, U.S. District Judge Sim Lake completed two days of hearings and ordered them all to federal prison.

Jahangir received a 151-month term of imprisonment. Mfullu and Mohammed both received terms of 50 months, while Hassan, Mwinyi, Mbwile, Maalim, Madega, Adam and Vedasto, were ordered to serve 99, 62, 52, 46, 87, 37 and 46 months, respectively. The court imposed a 135-month sentence for Balouch. Not U.S. citizens, they are all expected to face deportation proceedings following their sentences.

This case began with the arrest of an internal body carrier at Houston’s Bush Intercontinental Airport June 3, 2012. That defendant had swallowed 1.5 kilograms of heroin packaged in 100 pellets.

The investigation eventually led to the charging of 15 defendants, including two Consolidated Priority Organization Targets, one U.S. Treasury Department designated “King Pin” and seizures of approximately 1,600 kilograms of heroin.

This investigation not only touched the United States, but also Canada, Afghanistan, Pakistan, Iran, South Africa, Tanzania, The Republic of Seychelles, Hong Kong, Australia, Oman, United Kingdom (UK), Italy, Brazil, United Arab Emirates, South Korea, Mozambique, The Netherlands and Saudi Arabia.

Thirteen have pleaded guilty. Two remain fugitives.

Immigration and Customs Enforcement’s Homeland Security Investigations (HSI) conducted the Organized Crime Drug Enforcement Task Force Investigation dubbed Operation Diver Down with assistance from other HSI offices domestic and foreign, Drug Enforcement Administration, South African Police Service, Dubai Police Department, Royal Oman Police, UK National Crime Agency, Royal Canadian Mounted Police and Australian Federal Police.

Assistant U.S. Attorney Richard Magness is prosecuting the case.
 

MAKALA HII IMEANDIKWA NA MESHACK MAGANGA WA IRINGA TANZANIA.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikitoa hamasa kwa vijana wenzangu wa kike na kiume na watu wa kada mbalimbali, wito wangu umekuwa nikuwataka vijana wenzangu kauanza utamaduni wa kuwekeza kwa muda mrefu na kujifunza ujasiriamali. Ninaandika makala hii kutoa ushuhuda wa niliyoyafanya kwa muda wa zaidi ya miaka miwili iliyopita na kuniletea mafanikio makubwa.

Nilianza kujishighulisha na ujasiriamali nilipokuwa chuo kikuu mwaka wa pili, kwa kuuza vocha na kazi ya ‘steshenari’ na uuzaji wa laptop, sikuendelea nazo sana kwa sababu ya kubanwa na masomo yachuo. Nilipomaliza chuo 2010, nilianza kilimo cha mboga na kufuga kuku hapa Iringa mjini, baada ya hapo kaka yangu alianza kunihimiza kuhusu kilimo cha miti ambacho yeye mwenyewe anafanya.

Na baadaye nikakutana na rafiki yangu Albert Sanga ambaye pia anajishughulisha sana na kilimo cha miti. Tangu 2011 nilinunua shamba la ekari 10 na kuzipanda miti hela ambayo niliipata baada ya kuuza matango niliyolima kijijini Kalenga, nikaongeza bidii zaidi ya kulima matango na kununua mashamba, leo nina ekari nyingi.

Albert sanga, mjasirimali na mwekezaji alipata kuandika haya kuhusu mimi:- “UNASUBIRI UPATE MTAJI? OPSss! UNAWEZA KUFA MASIKINI! Nina rafiki yangu mpambanaji kweli kweli na msomi wa chuo kikuu wa mambo ya maendeleo na elimu; na mtaalamu wa IT, anaitwa Meshack Maganga. Wakati fulani huko nyuma alinifuata na kuniambia, "Sanga nimeamua kuanza kui-invest katika mashamba ya miti; mtaji wa kuanzia nina tsh elfu ishirini na tano, (25,000?/=).

Nikamwambia "Kupata ekari moja si chini ya laki sita na wewe una tsh 25,000/= utawezaje?" Akanijibu "Nitaweza!", Sikumwelewa! Kumbe alikuwa anaona mbali! Alichofanya alichukua hiyo 25,000/= akaenda nayo eneo moja linaitwa Kalenga (km 20 kutoka Iringa mjini) huko akalima matango. Angalia mchanganuo: Shamba nusu eka akakodi kwa tsh 10,000/=, mbegu za matango akanunua Tsh. 7,000/=.

Kwenye kulima akalima kwa mikono yake akisaidiana na kibarua mmoja. Fedha iliyobaki 8,000/= akalipa kibarua na kununulia dawa ya kuua wadudu. Alipokuja kuvuna akapata tsh 800,000/= (laki nane). Alipokuja na fedha hii tukaenda kutafuta shamba la miti akaanza na ekari moja huku pesa nyingine akairudisha shambani.

Hivi leo Bw. Maganga ana ekari zisizopungua hamsini za mashamba ya miti na anaendelea na kilimo cha umwagiliaji. Lakini HAPO amefika kwa kutumia tsh 25,000/= tu. Tunaposema hauhitaji mamilioni kujiajiri tunatamani ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa kama Bw. Maganga. Unaweza kumwandikia” Akaendelea kwa kusema:-

Kuhusu kilimo cha miti ninacho kifanya mimi na nimepania kwelikweli ndani ya nchi yangu niipendayo Tanzania ni kwamba, kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya mazingira. Katika Tanzania mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya kupandwa.

Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea pamoja na utengenezeaji wa karatasi. Ukiacha mahitaji haya tuliyoyazoea; hivi sasa kumeibuka fursa nyingine mpya ambapo mashirika ya kimazingira kutoka Magharibi yananunua hewa ukaa. Kwa maana hiyo unaweza kupanda shamba la miti halafu ukawa unakusanya dola kwa kuuza hewa ukaa wakati ukisubiri miti ikomae uvune mbao, nguzo ama miti ghafi ya kutengenezea karatasi.

Hii ni sawa na kutegeneza hela ukiwa umelala. Mbali na kuuza hewa ukaa, vile vile unaweza kufuga nyuki na kuendelea kuvuna asali wakati unasubiri kukusanya mamilioni kwa kuuza miti ya nguzo, karatasi ama mbao.Kilimo hiki cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (middle& long term investments). Kiutamaduni watanzania wengi huwa hawavutiwi na uwekezaji wa muda mrefu.

Hata hivyo kama una mpango wa kuwa na “financial freedom” usikwepe kufikiria uwekezaji wa muda mrefu. Waingereza husema “Information is power”. Wengi hawajachangamkia fursa hii kwa kukosa taarifa tu. Kazi yangu leo ni kukupa taarifa hizi za utajirisho. Miti ya mbao inatumia wastani wa miaka sita hadi 8 au saba, tangu kupandwa hadi kuvunwa kwake.

Hii ina maana inapofikisha umri wa miaka sita huwa tayari kwa kuanza kuvunwa kwa mbao ndogo. Ekari moja ya shamba inachukua wastani wa miti mia sita (600). Wastani wa chini wa mti mmoja kwa sasa uliokomaa ni shilingi elfu ishirini (30,000 hadi 60,000,inategemea na ukubwa wa mti). Ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa unakusanya jumla ya shilingi milioni kumi na nane (18,000,000).

Fedha hiyo (kadirio la chini kabisa) utaipata ikiwa unaamua kuuza kwa bei ya jumla miti ikiwa shambani. Lakini kama ukiamua kupasua mbao wewe mwenyewe unaweza kuvuna mbao hadi za milioni thelathini na mbili (32,000,000) kwa ekari moja. Hadi sasa uhitaji (demand) wa mbao katika soko ni mkubwa kuliko ugavi (supply) hivyo kwa miaka 10 ijayo hatutarajii kushuka kwa soko la mbao, nguzo ama malighafi za karatasi.

Gharama ya kununua shamba tupu ni kati ya shilingi laki moja na 20 elfu (120,000) na laki moja, kutegemea na maeneo husika unayotaka ama kupata. Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni kati ya shilingi laki moja na nusu,na laki moja. Hii ina maana unaweza kumiliki ekari moja ya msitu wa miti kwa hadi shilingi laki sita tu! Kutegemea na umri wa miti unayotaka.

Mtu unaweza kuona kuwa pengine kununua shamba tupu na kuanza kuhangaika na upandaji miti itakuwa ni mlolongo mkubwa; kukusaidia katika hilo nimekuwa na utaratibu wa kumilikisha mashamba yenye miti (kuuza) kwa bei nafuu sana. Yapo mashamba yenye miti ya kuanzia mwaka mmoja, miaka miwili, miaka mitatu na miaka minne.

Uponunua mashamba haya kutoka kwangu, mimi naendelea na upandaji wa mashamba mapya kupitia fedha hizo. Kilimo cha miti ni rahisi sana kwa sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi mkubwa sana na wala hauhitajiki uwe karibu na shamba/mradi muda wote. Kuna kazi chache ambazo zinahitajika ukishapanda shamba lako.

Mvua inyeshe ama isinyeshe mti wa mbao, nguzo ama karatasi ukishachipua huwa haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini. Kazi namba moja unapokuwa umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba; ni kutengeneza njia za kuzuia moto walau mara moja kwa mwaka, kazi ya pili ni kufyekea miti inapokua walau kwa mwaka mara moja (prooning).

Gharama zote hizo yaani kutengeneza njia za moto, kufyekea na kulinda moto haizidi laki mbili kwa mwaka mzima. Kwa maana hii gharama za kuhudumia shamba la miti ekari moja kutoka kupandwa hadi kuvunwa ni wastani wa shilingi milioni moja tu. Gharama hizi ninazopiga ni ikiwa utaamua kununua shamba leo na kama ungekuwa tayari una shamba ambalo unalihudumia leo.

Hata hivyo nadhani wote tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda thamani kila siku. Vile vile tunatambua kuwa suala la mazingira ni tete kwa sasa na katika karne zijazo kama wataalamu wanavyotuthibitishia. Hii ina maana kuwa ukiwa na shamba la miti leo; thamani ya ardhi hiyo inazidi kupanda kila siku na miti uliyopanda inazidi kupanda thamani kila kukicha.

Jambo la uhakika ni kuwa hata kama bei ya miti, mbao, nguzo itayumba hutaweza kupoteza mtaji uliotumia na wala hutakosa kuzalisha faida kwa shamba utakalokuwa umemiliki, iwe ni eka moja, kumi, mia ama elfu moja. Mbali na hivyo unaweza ukaona, ahaa, miaka sita hadi kumi ni mingi mno; bado una nafasi ya kupata faida hata ndani ya mwaka mmoja, miwili au mitatu.

Ukishapanda shamba la miti ekari moja kisha baada ya mwaka mmoja ukaamua uuze utauza si chini ya milioni mbili hadi nne. Kukusanya milioni nne kwa mtaji wa laki sita, pasipo kutumia muda mwingi ama usumbufu wa kusimamia; hakika ni faida nono.

Huenda hadi kufika hapa unaweza ukawa umeshavutiwa na biashara hii. Wengi wenu mnaweza kujiuliza maswali mkubwa mawili; “Ninatamani nifanye mradi huu lakini Iringa sikufahamu na hata kama nakufahamu nitaanzia wapi kupata hayo maeneo?” Pili: Niko mbali na sina muda wa kushinda Iringa, Je, ni nani atanisaidia kupanda, kusimamia na kuendesha hayo mashamba?

Ili kutimiza ndoto yangu hiyo nimeweka utaratibu ufuatao utakaohakikisha kila mwenye ndoto, kiu na hamasiko la kuwekeza kwenye kilimo cha miti anafanikiwa. Jisikie huru wakati wowote kuwasiliana nami kwa ufafanuzi na msaada wa fursa hii. Natamani watanzania tuache kulalamika kuhusu wageni kuvamia ardhi yetu, badala yake tuchangamke kumiliki na kufanya uzalishaji katika ardhi yetu.

Inawezekana! Kwa kutumia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 sheria namba 5 utapata documents za umiliki; kwa kuzingatia taratibu na tamaduni zote za wenyeji zinazohusiana na umilikaji ardhi nitahakikisha nakusaidia ili ndoto yako itimie.

Yupo Baba yangu anaishi Mafinga ambae siku za karibuni amepewa Tuzo ya Rais kwa kuwa mpandaji namba moja wa miti na utunzaji wa mazingira, ameahidi kutoa msaada kwa Mtanzania wa ndani na nje ya Tanzania kumsadia kupata eneo la kupanda miti na kauli ya siku zote ni “USIKUBALI KUWA MNYONGE WA KIUCHUMI NDANI YA TANZANIA.
Hii makala imenigusa sana. Ni baada ya kuona potential inayoambatana na mradi huu wa miti, lakini hapo nikawa sina muda wa kuweza kutekeleza mradi wa aina hii
 
Huwa nikiona maelezo jinsi ya kupata pesa kwa kufanya biashara fulani,kengere za hatari huwaka kichwani,na hapo bongo yangu huwa makini kutafuta element za kitaperi zilizojificha,
Kwenye maelezo yako,unataka tununue mashamba kwako,why?hapo ndio utaperi unapoanzia,
Kwa hulka ya binadamu,aone dhahabu,harafu akuite mwende mkaibebe wote mtajirike?!!hiyo ni nadharia.
Kwenye maelezo yako,sema Kama umewalenga vijana waliozaliwa Dar,Arusha,ambao hawajuhi Iringa/Mafing/Niombe,hizo taarifa unazosema,unazo mtu yeyote akizitaka ni kwenda Mafinga,Niombe,Kuna wenyeji wanafsnya biashara hizo,watakupa taarifa bila mbwembwe,
Kuna sehemu Kanda ya ziwa,inaitwa Kalumwa,Kahama,Nilienda kule,wenyeji walinipa A to Z,jinsi ya kukodisha mashamba ya mpunga,
Acha utaperi Kama unataka kusaidia,usilete story,Kama vile kilimo Cha miti ni sawa na kutengeneza bomu la nyuklia,

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
 
Naanza kwa kuunga mkono hoja kuwa kweli huu ni uwekezaji wa kudumu na itakufaidisha zaidi ukiwa na eneo kubwa ambapo utaanza kuuza miti kwa mkupuo.

LAKINI NAPINGA VIKALI UPOTOSHAJI WA TAKWIMU ULIOUFANYA.

Haiwezekani hata kidogo ekari 1 ya miti yenye umri wa kati ya miaka 6-8 iuzwe kwa millioni 18,it is too much overrated my boy,i say is impossible,impossible over impossible.

Una dhamira njema ya kuwainspire watu wafanye uwekezaji ila kwa takwimu zako nakutilia shaka kuwa una maslahi binafsi nyuma ya pazia.

Ukweli ni kwamba miti ya umri wa miaka 6-8 hutoa mbao nyingi za size ya 2*4 na 2*6 na kiduchu 1*8 ambapo kwa ujumla mti mmoja average huuzwa 6000 * 600=3,600,000.

Endapo utataka uuze ekari 1 kwa m18 itakubidi usubiri kati ya miaka 15-20,ambapo mti huo utakuwa na uwezo wa kutoa mbao size kubwa za 1*10 kwa pingili hadi 2 hadi 3.

Kuweni makini na elimu hizi wana jf and i will stand to be correct.
15-20 unasubiri 18M tu?? Kwa hekari moja..

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom